HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Tuesday, August 28, 2012

WALIOVAMIA PORI TENGEFU LA KILOMBERO WATAKIWA KUONDOKA IFIKAPO TAREHE 31 AGOSTI 2012

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bibi Maimuna Tarishi
Watu waliovamia na kuishi katika Pori Tengefu la Kilombero wametakiwa kutoka kwenye eneo hilo kwa hiari yao kabla ya tarehe 31 Agosti 2012. Watu hao ni wale ambao hawajaondoka baada ya kutakiwa kufanya hivyo mara kwa mara.

Azimio hilo lilifikiwa katika kikao cha pamoja kati ya uongozi wa Wilaya za Kilombero na Ulanga na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bibi Maimuna Tarishi kilichofanyika Kilombero tarehe 14 Agosti 2012. 

Nia ya kikao hicho ilikuwa ni kuweka mikakati ya kutekeleza azama ya Serikali ya kuwataka wavamizi katika Pori Tengefu la Kilombero kuondoka katika eneo hilo.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Francis Miti, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Evarist Mmbaga, Mtendaji wa Wilaya ya Kilombero, Azimina Mbilinyi na watendaji wengine kutoka Wilaya za Kilombero na Ulanga.

Kikao hicho kiliamua kuwa ifikapo tarehe 8 Septemba, 2012 kazi ya kuwatoa wavamizi ambao bado watakuwepo katika pori hilo itaanza. Kazi hiyo ya kuwaondoa itatekelezwa kwa pamoja na Kamati za Usalama ngazi ya Mkoa na Wilaya za Ulanga na Kilombero, Kikosi Dhidi ya Ujangili, Askari Polisi na Askari kutoka Pori la Akiba Selous.

Hadi sasa wanachi wameelimishwa kuhusu umuhimu wa Pori Tengefu la Kilombero na manufaa yatakayopatikana kama litaachwa wazi. Wanavijiji wanaopakana na Pori hilo wameonyeshwa mipaka baina ya vijiji vyao na Pori.

Aidha mipango imekamilika ya kuiwekea mifugo alama (brandas) kwa lengo la kuweka mipango bora ya matumizi ya ardhi katika vijiji vilivyoko katika Bonde la Kilombero. Kazi hii inaratibiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Vilevile kazi ya kutambua mipaka, kufyeka, na kuweka alama (beacons) zinaendelea kwa pamoja katika vijiji 105 vya Wilaya za Ulanga na Kilombero na zinategemewa kukamilika tarehe 27 Agosti, 2012. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii aliahidi kuwa Wizara itachangia Shs. 106,500,000 ili kuharakisha utekelezaji wa kazi hiyo ya kuimarisha mipaka.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amevitaka Vijiji vinavyopakana na Pori hilo kuanzisha Jumuiya za Kuhifadhi Wanyamapori (WMA) ili kuimarisha ulinzi wa hifadhi hiyo dhidi ya wavamizi. 

Pia, kupitia WMA jamii husika zitapata manufaa kiuchumi kutokana na matumizi ya rasilimali za wanyamapori zilizopo.

Vilevile kila kijiji kimetakiwa kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi ambao, pamoja na mambo mengine, utaonyesha maeneo ya malisho ya mifugo.

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

 

Kuna haja ya kutoa Elimu kwa watu wa Ulanga

Wandugu ndo nimerudi tu toka Mtimbira tarehe Agosti, 2012

Na Francis Uhadi


Hali ya Mazao

Kiufupi mwaka huu mavuno ni hafifu sana kutokana hasa na ukosefu wa mvua. Watu walilima hadi heka 10 lakini utakuta wamerudi na gunia 8- 12 kwa hiyo mnaweza kuona hali si nzuri kabisa. Mbaya zaidi kwa kweli maisha ya Mtimbira yamepanda sana pengine naweza kusema zaidi ya Dsm kwa baadhi ya vitu. Mtakubaliana na mimi hapa Dar mpaka sasa Kilo ya nyama maeneo mengi bado inauzazwa Tsh. 5000-5500 lakini Mtimbira bei ya kawaida tu ni Tsh. 6000 ile minofu pori uliyokuwa mnakula zamani imebakia historia. Ukienda kwa upande wa samaki ndo hugusi kabisa ukubwa wa kiganja cha motto ni Tsh. 3000 wanaenda hadi 10000. Kuku (jogoo) 15000- na kuendelea. Kwa jumla maisha yamepanda sana.

Huduma za Afya

Kama kawaida yangu huwa siondoki bila kufuatilia masuala yanayogusa jamii. Malalamiko ya Watu wengi ni juu ya huduma duni za Afya katika kituo chetu. Hadi sasa Madaktari wote wana maduka ya Dawa ambayo wameanza kuyageuza kuwa hospitali kwa kuwaduhumia watu vizuri zaidi wakiwa Madukani mwao au kuwa-refer ( kuwaeleza waende dukani jioni ) kwa huduma bora zaidi za kulipia. Kilichowasikitisha zaidi wananchi ni kuwa hadi mtu wa kupima Maabara naye ameanzisha Baabara yake binafsi.

Kinachotokea sasa ni kwamba kila mwananchi anayeenda kwa vipimo anambiwa hospitali haina kemikali (Reagents) na kumtaka aende maabara ya nje akiwa na Tsh. 5000 kwa ajili ya vipimo ambako pia ni mtu yule yule wa Maabara ya Kituo cha Afya anashughulika na vipimo hivyo.

Kwa maoni yangu hapa pana mgongano mkubwa sana wa maslahi unaofifisha ubora wa huduma katika Kituo cha Afya na hii pia ni njia rahisi sana ya kujipatia wateja kwa Watumishi wa Hospitali ambao wameajiriwa na wanalipwa mishahara.

Elimu

Mtakumbuka kuwa Shule za Tarafa ya Mtimbira zimefelisha sana katika matokeo ya Kidato cha Nne wa Mwaka jana. Kwa uchunguzi wangu wa muda mfupi nimegundua kuwa pamoja na changamoto za uhaba wa Walimu Wenye weledi wa kufundisha, zipo pia changamoto kubwa kwa wazazi na wanafunzi wenyewe. Chidabaga kimekuwa kingi kulizo kupenda shule. Kufeli kwa wanafunzi wa Madarasa yaliyopita pia kumechangia kuwakatisha tamaa wazazi na wanafunzi kwamba hata ufanyeje utafeli tu. Nimegundua pia hata wale wanafunzi wanaowaongoza wenzao wanaongoza katika hali za kufeli pia kwa kuwa nao maksi zao ni za chini sana. Mwamko tu wa elimu na tama ya kujiendeleza hazipo badala yake kumekuwa na majungu zaidi na kuchapa kidabaga. Maoni yangu ni sisi tunaoishi hapa Dar es Salaam pamoja na vijana ambao wamesoma na kujifunza toka kwa wengine tuwe chachu ya mabadiliko kule Mtimbira. Lazima kitu fulani kifanyike ili vijana na wazazi waamke.

Ukiukwaji wa Haki za Binadamu, Uhasama na Mauaji

Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la uhasama miongoni mwa jamii, mauaji kwa sababu mbalimbali zikiwemo suala la wivu wa Kimapenzi kwa mfano yupo mtu aliyepigwa Mkuki tumboni na kufa maeneo ya Munga kwa karibu na Maganga. Ipo pia migogoro mingi ya ardhi n.k. Kilichonisikitisha pia watu wamezidi kushitakiana kwa case ambazo kwa miaka ya zamani zingetatuliwa tu kijamii. Kwa hiyo kumekuwa pia na ongezeko la watu wanaofungwa kwa kesi za ajabu ajabu tu. Kwa jumla Mtimbira imebadilika sana, yale yaliyofahamika kama Social Cohesion – Umoja wa Kijamii na kusaidiana yamepotea sana.

Kivuko na Barabara

Barabara si mbaya sana, ingawa tatizo kubwa naliona kivukoni. Kivuko kilichopo kimechoka sana na ni kidogo. Pengine itufundishe kuelemisha zaidi wananchi wa kwetu kudai uboreshwaji wa miundombinu katika eneo hilo.

Nafikiri kuna haja ya kujadili haya.

OBJECTIVES OF ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga District and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources.

Major aims of UCRC:-

1.   To carry on activities which influence and advocate for good governance, accountability, transparency and promotion of the fight against all forms of discrimination by advocating for change of practices, policies and laws.

2.   Promote the protection and sustainable use of natural resource for the benefit of current and future generations.

3.   To promote and facilitate education on land rights, human rights and gender issues and strengthen local governance and accountability systems.

4.   To promote educational activities through initiation of community libraries and study centers.

5.   To work in the area of land law and land legislation, including lobbying for legislation related to the protection of resident communities’ land as a necessary economic assert and right. 

6.   Provision of legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.