HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Thursday, September 27, 2012

Wanafunzi watakao faulu Sekondari Uchindile kusomeshwa BURE

Na Senior Libonge,Kilombero
MKUU wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema kuwa atamlipia gharama ya masomo na malazi kwa muhula wa kwanza mwanafunzi yeyote atakaemaliza kidato cha nne mwaka huu na kufaulu kwa kupata daraja la 2 ama 3 kutoka katika shule ya sekondari ya kata ya Uchindile.
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari ambayo ipo pembezoni mwa wilaya ya Kilombero ambayo kwa kiasi kikubwa ukimbiwa na walimu pamoja na wanafunzi kutokana umbali wake.
Masala ameamua kujitolea kumsaidia mwanafunzi yeyote atakaefaulu baada ya kusomewa risala ya shule hiyo na kuelezwa kuwa kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ni mwanafunzi mmoja tu ndiye aliyefaulu kwa kupata daraja la 4.
Katika kuwatia moyo wanafunzi watakaomaliza mwaka huu Masala amesema yeyote atakaepata daraja hilo yupo tayari kumlipia ada na malazi kwa muhula wa kwanza ili mradi mwanafunzi huyo amletee barua ya mahitaji ya shule(Join Instruction).
Amesema ameamua kutoa ofa kwa shule hiyo kutokana na mazingira ya shule yenyewe hasa baada ya kuona wanafunzi wake wakijitahidi kusoma licha ya mazingira yake kuwa pembezoni mwa kata hata wilaya na pia wengi wa wanafunzi wakiwa wametoka nje ya kata hiyo.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka wanafunzi wengine kusoma kwa bidii na kuheshimu walimu wao huku pia akiwataka walimu kuwafundisha wanafunzi hao kwa bidii licha ya kuwa na changamoto mbalimbali ambazo ameahidi kuzishughulikia baadhi yake.
Awali akisoma risala ya shule hiyo mkuu wa shule Januari Mkoba amesema shule iliponzishwa ilikuwa na wanafunzi 59 ila sasa ina wanafunzi 120 na walimu 8 huku wanafunzi wengi wakitoka katika tarafa ya Ifakara baada ya shule za msingi katika kata hiyo kushindwa kufaulisha wanafunzi wake.
Mkoba amesema changamoto kubwa ni wakati wa likizo wanafunzi wengi kuchelewa kurudi shule kutokana na umbali wanapotoka huku pia ushindwa kukutana na wazazi kutokana na tatizo hilohilo la umbali na hali hiyo upelekea wanafunzi kushindwa kusoma masomo yote kwa wakati unaotakiwa.
Pia mwalimu huyo alisema shule hiyo haina mwalimu wa masomo ya hisabati na fizikia na hali hiyo upelekea wanafunzi kutaka kuhama kwa kukosa masomo hayo na pia shule kukosa usafiri ambao ungesaidia walimu kurahisisha kudurufu hata karatasi za masomo mbalimbali.
Akijibu hoja za jumla,Masala alisema atakutana na mkurugenzi mtendaji wa wilaya ili kufanikisha shule hiyo kuwa na walimu wa masomo ya fizikia na hisabati na pia atajitahidi kupigania ili shule hiyo ipate pikipiki moja ambayo itawasaidia walimu waliopo kurahisisha shughuli mbalimbali ukizingatia lengo la halmashauri ni kusaidia walimu wote waliopo pembezoni mwa wilaya.

Mbuge Mteketa awataka wananchi Kilombero kuwajibika

Na Senior Libonge, Kilombero
MBUNGE wa jimbo la Kilombero Abdul Mteketa amewataka wakazi wa wilaya ya Kilombero kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuachana na zana kuwa serikali itashughulikia kila kitu.
Sambamba na hilo Mteketa pia amewaambia wananchi hao kuwa wawapuuze viongozi wa kisiasa wanauzunguka katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hiyo kwa kuwarubuni wananchi kuwa wasichangie fedha za miradi mbalimbali na kusema kuwa watu hao wamefilisika kisiasa.
Akizungumza na wananchi wa kata za Mngeta na Mbingu wilayani humo,Mteketa amesema kuwa wakati wa kutegemea bure bure hivi sasa umekwisha ni wajibu wa kila mwananchi kuchangia maendeleo yake na serikali itasaidia pale inapoona inabidi kusaidia.
Ametolea mfano kuwa huduma za msingi kama ujenzi wa shule na zahanati ni wajibu kwanza wananchi kuchangia nguvu zao na shughuli ya umaliziaji inafanywa na serikali na hiyo ipo hata katika nchi zilizoendelea.
Amesema kuwa mwananchi ama kikundi kitakachokuwa tayari kuchukua mkopo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya jamii yeye yupo tayari kusaidia ila wahusika wawe tayari kuchangia angalau nusu ya gharama ya mkopo huo.
Kauli hiyo ya Mteketa ameitoa baada ya wananchi wa kijiji cha Mkangalo kata ya Mngeta kushindwa kumalizia kukusanya tofari za ujenzi wa nyumba ya daktari wakati zahanati ya kijiji ikiwa imekamilika huku madawa toka serikalini yakiwa yamekwisha letwa.
Pia wananchi hao walimshangaza mbunge huyo kwa kushindwa kulima nyasi zilizozunguka zahanati hiyo kwa madai kuwa serikali ndiyo inapaswa kufanya usafi katika eneo hilo licha ya diwani wa kata ya Mngeta  Felician Kigawa kuwataka wakazi hao kufanya usafi huo.
Kuhusu baadhi ya wananchi kuzunguka na kuwadanganya wananchi,Mteketa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu hao kwani uwaongopea mambo mengi kwa kuona kama wananchi wa jimbo hilo sio waelewa.
Amesema wakati wa siasa kwa sasa umekwisha na yeye ni mbunge halali wa jimbo hilo hadi mwaka 2015 na kuwataka wananchi kuwaogopa wanasiasa hao kama ukoma kwani hawana jipya badala ya kumwaga sera za vyama vyao wao umwaga matusi kwa lengo la kujenga chuki kati ya wananchi na serikali.
Katika ziara zake jimboni humo licha ya kutoa shukrani na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi pia mbunge huyo amekua akitoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali na pia utoa vitabu vya masomo ya sayansi.

Monday, September 24, 2012

MATOFALI 175,000 YAKUSANYWA KWA SHUGHULI ZA MAENDELEO MNGETA

Henry Bernard Mwakifuna, Mngeta,Kilombero

JUMLA ya Matofali 175,000 yamekusanywa na Wanachi wa Kata ya Mchombe, Tarafa ya Mngeta Wilayani Kilombero  kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata hiyo.

Shaban Mgaya, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mchombe amesema Matofali hayo yanatumika kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa katika shule mbili za sekondari za Kata ambazo ni Mchombe na  kiburubutu.

Amesema kuwa kati ya Matofali hayo, Matofali 40,000 yametumika katika ujenzi wa sekondari hizo mbili akichanganua Matofali 23,000 yametumika katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya Mchombe na Matofali 17,000 yametumika Sekondari Kiburubutu.

Zaidi ya Matofali 50,000 yametumika katika ujenzi waMsingi wa Ghala na kukamilisha boma la nyumba katika kijiji cha Ikule na Matofali 60,000 yametumika katika kijiji cha Mkangawalo Ujenzi wa Ghala na Madarasa ya shule ya msingi
..

Moto wateketeza mali ya zaidi Mil. 2 Chita Kilombero

Henry Bernard Mwakifuna, Chita, Kilombero

Mabanda Sita yenye Mali zenye Thamani ya Shilingi Milioni 2 na Elfu 95 yameteketea katika ajali ya moto uliotokea  Katika Kijiji cha Merera kilichopo Kata ya Chita Wilayani Kilombero.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Merera Bwana Odwin Mafulu amesema kuwa mabanda ya Migahawa, mabanda ya kuoneshea Video Magenge, kushonea nguo na yakuuzia vitu mbalimbali yameteketea kwa moto ulioanza saa Sita mchana.

Chanzo cha Ajali hiyo ya Moto hakijafahamika ambapo Afisa Mtendaji amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji hicho inaelendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mbali ya hapo amesema kuwa kumekuwepo na Taarifa za awali  ambazo  hazina uhakika  juu ya chanzo cha moto huo kuwa ni Mtoto Mdogo kuchezea Kiberiti katika banda moja na kusababisha mabanda mengine kuungua.

Asasi ya Kiraia yapania kukomesha ongezeko la Yatima Kilombero

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero

JUMLA ya Watu 120 wanataraji kupata Mafunzo ya Haki Elimu kwa Watoto Yatima na Wale Wanaoishi katika Mazingira Magumu katika Eneo la Kibaoni, Makero na Michenga Wilayani Kilombero.

Evenita Chamanga, Katibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women and Children Group amesema kuwa watakaopata Mafunzo hayo ni Wananchi na Viongozi wa Serikali kutoka katika maeneo hayo.

Amesema kuwa wameamua kufanya Mafunzo kwa maeneo ya Kibaoni, Makero na Michenga kwa kuwa asilimia 10  tu ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu ndiyo wamepata Elimu katika maeneo hayo.

Wakati huo huo Taasisi hiyo ya Women and Children Group Tarehe 24 Septemba 2012 itaanza mafunzo ya kuhusu haki elimu kwa Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu.

Mafunzo hayo yanataraji kufanyika katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni Ifakara Mjini na yamefadhiliwa na  Foundation for Civil Society.

Friday, September 21, 2012

Mkuu wa Mkoa Morogoro apania kutokomeza "Hati Chafu"

Na Senior Libonge,Kilombero

MKUU wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera amesema kuwa hataki kusikia tena katika mkoa huo wilaya yoyote inalalamikiwa na mkaguzi wa mahesabu kwa kupata hati chafu na ikifanya hivyo uongozi wote wa wilaya utawajibika.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na madiwani na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero na kusema kuwa kwa kuanzia sasa atafanya uchunguzi kila mwezi ili kugundua halmashauri ipi inaurudisha nyuma mkoa wa Morogoro katika ukusanyaji wa mapato.

Bendera ameuagiza uongozi wa wilaya zote kwa kushirikiana na madiwani kuhakikisha kuwa watendaji wote wanaosababisha uzembe wa kula fedha za halmashauri wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

“Kuna watendaji wanafanya mambo watakavyo kwa kula fedha za halmashauri na kumaliza hadi mbegu sasa nyinyi viongozi wa wilaya mna majukumu ya kuwashughulikia na mkishindwa mniambie mimi niwashughulikie lengo ni kuona halmashauri zote zinapata hati safi,”alisema.

 Mkuu huyo wa mkoa amesema halmashauri nyingi hazisimamii miradi ya maendeleo ipasavyo kwani miradi mingi haiendani na thamani halisi ya fedha kwa watendaji kufanya mambo wafanyavyo huku wakiachwa bila kuchukuliwa hatua na hatimaye wananchi kuichukia serikali kwa upuuzi wa watu wachache.

Amezisifu wilaya mbili za Kilombero na Ulanga kwa kufanya vizuri katika mahesabu ya mkaguzi kwa kupata hati safi zenye mashaka kwa miaka miwili mfululizo na kuchukizwa na wilaya za Kilosa na Moro vijijini kwa kutafuna fedha za umma na hatimaye kupata hati chafu.

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa ametaja changamoto zinazosababisha kusuasua kwa miradi kuwa ni wananchi kutoshirikishwa ipasavyo katika miradi huku baadhi ya wanasiasa kushawishi wananchi kutochangia miradi na uwajibikaji mdogo katika ngazi za usimamizi wa miradi.

Ameziagiza halmashauri zote kujipanga na kuzingatia  hoja za mkaguzi na maagizo ya Tamisemi,taarifa za mradi zijadiliwe katika menejimenti na madiwani na kutoa elimu na uhamasishaji kwa wananchi punde unapotokea mradi.

Aidha Bendera amezitaka halmashauri zihakikishe zinaheshimu maamuzi ya vikao vyao na wasiwe vigeugeu na wananchi wahamasishwe ili waweze kuchagia huku pia serikali za wilaya.




MKUU WA MKOA ASISITIZA USIMAMIZI KATIKA MIRADI

Henry Bernard Mwakifuna, Mlimba-Kilombero

Madiwani, Watendaji wa Halmashauri, Watendaji wa Vijiji na Kata na Wataalamu katika Wilaya ya Kilombero wamehimizwa  kusimamia Miradi inayohudumia Wananchi kutengenezwa kwa kukidhi Viwango.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Joel Nkaya Bendera amesema kuwa thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali ilingane na Miradi husika.

Amesema kumekuwa na ubadhirifu wa fedha katika miradi ya kijamii ambapo thamani halisi ya fedha hailingani na Miradi husika.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amewahimiza Wananchi kushiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo na hususani ujenzi wa Madarasa.

Amesema kwa Mwaka huu Mkoa wa Morogoro unahitaji Madarasa 288 kwa ajili ya kadirio la Wanafunzi 33,000 wanaotaraji kufaulu, kwa Wilaya ya Kilombero Jumla ya vyumba vya Madarasa 27 vinahitajika kwa ajili ya wanafunzi watakaofaulu kwa mwaka huu.

Mheshimiwa Bendera alikuwa akiongea na Wananchi wa Kata ya Mlimba katika Ziara yake Wilayani Kilombero, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Mlimba

Wananchi Kjiji cha Kivukoni wataka mapato ya Geti za mazao

Na Senior Libonge,Ulanga

WAKAZI wa kijiji cha Kivukoni wilayani Ulanga wameiomba halmashauri ya wilaya kukipa upendeleo kijiji hicho kwa kuwapatia asilimia ya mapato ya kizuizi cha wilaya kilichopo katika kijiji chao ili kufanyia shughuli mbalimbali za maendeleo.

Rai hiyo wameitoa juzi wakati wa mafunzo ya ufuatiliaji wa matumizi ya rasilimali za umma sekta ya kilimo wilaya ya Ulanga yanayotolewa na asasi isiyo ya kiserikali ya kikundi cha wanawake wa St.Maria Magdalena ya mjini Ifakara.

Wananchi hao wamesema kuwa hivi sasa kijiji hicho kinapata asilimia chache ya mapato licha ya kizuizi hicho kuwepo kwenye kijiji chao na wao kuendelea kuwa maskini huku wakishindwa kujiendesha ikiwemo wenyeviti wa vitongoji kukosa fedha za shajala.

Wamesema kwa hivi sasa hawaoni faida ya kuwepo kizuizi hicho katika kijiji chao kwani wamekuwa wakijichangisha wao wenyewe michango mbalimbali ya maendeleo bila kupata msaada wa kutosha katika halmashauri ukizingatia kuwa sehemu nyingine zenye kitegauchumi cha wilaya kijiji husika upata mafanikio ya mradi uliopo.

Aidha wananchi hao wamewaomba wabunge wa majimbo yote ya Ulanga mashariki na magharibi kufanya mikutano kwenye kijiji chao kwani wao ukipita tu kijiji hicho punde waingiapo katika ziara zao kwenye majimbo yao ukizingatia kuwa kijiji hicho ndiyo mlango wa wilaya ya Ulanga.

Kuhusu pembejeo za ruzuku za kilimo wananchi hao wamesema kuwa licha ya kuchelewa kufika kwa wakati pia pembejeo hizo zimekuwa bei ghali na hali hiyo umfanya mkulima wa chini kushindwa kuipata na kutimiza malengo yake katika kilimo..

Kwa upande wake afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Josephat Masanyoni ili kupata ukweli kuhusu malalamiko ya wananchi ambapo alikiri kweli kuwa malalamiko ya wananchi hao ni ya msingi na kuelezea suala la mbolea kuwa kweli ilichelewa kufika na licha ya kufika baadhi ya wananchi walikosa na tatizo kubwa ni uchangiaji wa fedha toka kwa wananchi.

Masanyoni akielezea suala la mapato ya kizuizi alisema kweli hawana asilimia wanayopata kutoka kwenye kizuizi hicho licha ya wao kupeleka malalamiko kwa viongozi wa wilaya na hata wananchi kutoa malalamiko yao punde wanapokuja viongozi mbalimbali.

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo  Christina Kulunge amesema mafunzo hayo ni ya siku 5 yanafanyika katika kata za Kivukoni,Minepa na Lupiro na lengo lake ni kuwajengea uwezo wananchi kuhusu ufuatiliaji wa pembejeo za ruzuku katika sekta ya kilimo.

Amesema pia wananchi wanatakiwa kuwa na ufahamu wa uchangiaji wa serikali katika mbolea za ruzuku na maadili ya utawala bora.

Christina amesema mradi huo ni wa mwaka mmoja na una gharama ya shilingi milioni 43 ambazo zimefadhiliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya The Foundation for civil society

Tuesday, September 18, 2012

Ujenzi wa Daraja la Mto Kilombero kuanza rasmi


Na Senior Libonge,Ulanga

Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa daraja la mto Kilombero ambalo linaunganisha wilaya za Kilombero na Ulanga katika Mkoa wa Morogoro  katika kipindi cha  mwaka huu wa fedha wa  2012/2013 

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejiment ya utumishi wa Umma  Celina Kombani, alitangaza kuanza kwa ujenzi huo  wakati akizungumza na wananchi wa kata za Ketaketa,Mwaya,Ilonga na Ruaha zilizopo katika jimbo la Ulanga mashariki mkoani Morogoro.

Alisema  kuwa tayari Serikali imeshapata fedha za kuanza ujenzi huo kinachofanyika hivi sasa ni kumpata mkandarasi ambaye atakamilisha ujenzi wake unatarajia kuanza katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha .

Waziri huyo alisema kuwa tayari  Serikali ilishafanya upembuzi yakinifu katika mto kilombero kwa kutumia kampuni moja kutoka nchini Kenya ambayo ilitumia zaidi ya shilingi bilioni moja katika kazi hiyo.

Kutokana na hali hiyo Waziri  Kombani aliwataka wakulima kuanza kuzalisha mazao kwa tija na kuweza kuyaweka sokoni ili kukabiliana na ushindani kipindi daraja hilo litakapokamilika.

Katika hatua nyingine huo huo Waziri  Kombani amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuacha kuuza chakula walichokipata katika msimu wa kilimo uliopita ili kiweze kuwasaidia katika kipindi cha msimu wa masika ambao mara kadhaa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa chakula.

Alisema katika kipindi hiki ni vema wananchi wakaelewa kuwa ni kipindi cha kujiwekea akiba ya chakula ili ije iwasaidie katika kipindi cha masika

Mashindano ya kugombea Kombe la Celina Kombani yapamba moto Ulanga

Na Senior Libonge,Kilombero

MASHINDANO ya mchezo wa soka na netball ya kuibua vipaji ya Mbunge wa jimbo la Ulanga mashariki Celina Kombani yameanza kurindima  katika tarafa mbili za mwaya na Vigoi katika jimbo la hilo  mkoani Morogoro.

Katika michezo ya ufunguzi timu ya soka ya Usalama imeweza kuifunga timu ya UDC kwa mabao 5-1 katika kituo cha Vigoi wakati kituo cha Mwaya Moro stars iliweza kuifunga Cameroon ya Iputi kwa mabao 3-0.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo katibu wa chama cha soka wilayani Ulanga Joseph Mkude ambaye ni mratibu wa mashindano hayo alisema kuwa jumla ya timu 52 zimejitokeza kushiriki michuano hiyo ambapo zitachujwa na kubaki timu nane zitakazocheza hatua ya robo fainali.

Alifafanua kuwa katika kituo cha mwaya timu 36 zimejitokeza kushiriki wakati kituo cha vigoi timu 16 zinashiriki mashindano hayo.

Aidha alisema jumla ya timu nane za mpira wa pete zitashiriki michuano hiyo kwa kituo cha vigoi na nne kwa kituo cha mwaya.

Akizungumzia michuano hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Celina Kombani amesema anaamini kupitia michuano hiyo watapatikana wachezaji mahiri ambao wataweza kupiga hatua ya michezo na kufikia katika ngazi ya kitaifa.

Alisema anajivunia michezo hiyo kutoa wachezaji ambao wameweza kucheza mashindano mbalimbali akitolea mfano mchezaji Godfrey Albino ambae alianzia katika michezo hiyo na sasa ameweza kuwakilisha nchi katika michezo ya umoja wa shule za sekondari kwa nchi za afrika mashariki.

Mashindano ya Celina Kombani mwaka huu yamefadhiliwa na NSSF, Quality group na DDC Kariakoo ambapo mshindi anatarajia kujinyakulia zawadi ya kikombe,seti ya jezi,fedha taslimu na kutembelea katika jimbo jirani la Ulanga magharibi katika sehemu ya kuhamasisha michezo.

Mbuge Kilombero agawa vitabu 500 kuboresha elimu

Na Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero

Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Abdul Mteketa anatarajia  kugawa Vitabu Vya Masomo ya Sayansi na Vifaa vya Michezo vyenye Thamani ya Shilingi Milioni Kumi na nane na Laki nane pindi atakapomaliza Ziara yake Jimboni mwake.

Akiongea na Redio Pambazuko Mheshimiwa Mteketa amesema ameleta vitabu  500 vyenye thamani ya  Shilingi Milioni Kumi na Tano  (15,000,000/) Amesema kuwa vitabu hivyo ni vya masomo ya  Biolojia, Fizikia, Hisabati na Kemia ambapo tayari ameshaanza kuvigawa katika Shule ya Sekondari ya Mofu.

Kwa upande wa Vifaa vya Michezo ameleta Jezi seti 20 Mipira 20 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni TATU NA Laki Nane (3,800,000/) na tayari vifaa hivyo vimeanza kugawiwa kwa vilabu mbalimbali vya mpira wa Miguu Wilayani Kilombero.

Monday, September 17, 2012

Migogoro ya Ardhi yazidi kupamba moto Mofu

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero

Wananchi waliovamia eneo la Hifadhi katika vijiji vya Mofu,Ihenga,Ikwambi Wilayani Kilombero  wametakiwa kuhama katika maeneo hayo  na kusitisha kufanya shughuli  zozote za kiuchumi.

Abdul Mteketa, Mbunge wa Jimbo la Kilombero (CCM) amesema kuwa wale wote waliovamia eneo hilo waliache na kuendelea kubaki eneo hilo ni kusababisha Uharibifu mkubwa wa mazingira na kukaidi agizo la serikali lililotaka wakazi wote waliopo eneo la hifadhi kuondoka ifikapo Septemba 7 mwaka huu.

Bwana Mteketa alikuwa akiongea na Wananchi wa kata ya Mofu katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mofu Kata ya Mofu akiwa na lengo la kuwashukuru Wananchi kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero.

Katika Ziara hiyo Mheshimiwa Mteketa ametoa Vitabu  80 vya masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari ya Mofu na vifaa vya Michezo Jezi pamoja na Mipira Mitatu katika Vijiji vya Mofu na Idete. 

Saturday, September 15, 2012

SERIKALI WILAYA KILOMBERO KUPITIA UPYA MIKATABA YA UWEKEZAJI

Henry Bernard Mwakifuna- Ifakara                                 

Serikali Wilaya ya Kilombero imesema itafanya Utaratibu wa Kupitia Mikataba  yote ya Wawekezaji.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amesema suala la msingi ni kujiridhisha na aina ya Mikataba iliyofanywa, kulinda Rasilimali zetu na Kusaidia kuepusha Migogoro kati ya Wawekezaji na Wanachi.

Amesema Mikataba iliyosawa na iliyoridhiwa itaendelea kuwa kama ilivyokubaliwa lakini ile ambayo ina mashaka taratibu zikifuatwa yaweza kusitishwa.

Bwana Masala ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Wananchi wa Mwaya Mang’ula katika mkutano wa hadhara ambapo amesema Wananchi wanapaswa kunufaika katika ajira zinazotokana na Wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amewapongeza Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji katika Wilaya ya Kilombero kwa kushiriki na Kusimamia vilivyo Zozi la Sensa ya Watu na Makazi.

Amesema ingawa kuna mapungufu ya hapa na pale lakini zoezi la sensa kutokana na usaidi mzuri wa Wenyeviti hao limeenda vizuri ndani ya Wilaya yake.

Baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza ni pamoja na uhaba wa Dodoso na baadhi ya Makarani kupangiwa maeneo makubwa ya kuhesabu watu.


Thursday, September 13, 2012

Wananchi Ifakara watakiwa kuchangia ujenzi wa Sekondari

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.

Diwani wa Kata ya Ifakara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Bwana Ramadhani Kiombile amesema suala la  kuchangia  shilingi Elfu Tatu Ujenzi wa Sekondari ni la Lazima na siyo la Hiyari.

Amesema kuwa Maendeleo ya eneo lolote yanaletwa na Kodi na Michango kama hiyo huku akiwataka Viongozi kuwajibika ili kufikia malengo waliyojiwekea.

Mchango wa Sekondari kwa Hiyari katika Kata ya Ifakara Mwisho kwa Shilingi Elfu Tatu ni Septemba 30 ambapo kuanzia Oktoba Mosi yeyote atakayebainika hajalipa atatozwa Faini ya Shilingi Elfu Kumi na Fedha halali Elfu Tatu jumla ikiwa ni Elfu Kumi na Tatu.

Kauli ya Bwana Kiombile aliitoa katika Kikao cha Baraza la Maendeleo la Kata ya Ifakara liliokaa katika Ukumbi wa Kantini Ifakara mbele ya Viongozi wa Vitongoji na Vijiji ambapo Diwani huyo amesema kuwa Wananco bado hawajaonesha Ushirikiano wa Dhati katika suala la Uchangiaji wa Mchango huo.

Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum Tarafa ya Ifakara Bi,Nasra Ngwega amewataka Watendaji na Wenyeviti wa Vitongoji kuwahamasisha wananchi mapema ili kuwaepusha na suala  kutozwa faini. Amesema hamasa inatakiwa ili Wanachi watoe Michango yao kwa Hiyari ili kuwaepusha na kukamatwa na Kutozwa Faini kitu ambacho kinawezekana kufanyika kabla ya Tarehe ya Mwisho ya Kuchangia kwa Hiyari.

 

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero

KASIMU HASSAN NJOHOLE (70), aliyekuwa Mmiliki wa Bendi ya NJOHOLE JAZZ BEND amefariki Dunia  hana katika Hospitali ya  Rufaa ya Mtakatifu Fransis Ifakara saa nanane Septemba 11 na anataraji kuzikwa leo.

Kwa muujibu wa Tarifa ya Hawa Njohole ambaye ni Dada wa Marehemu amesema kuwa Marehemu amekutwa na Mahuti baada ya kuugua kwa muda mrefu hi mbalimbali ambapo alikuwa amelazwa katika Hospitali hiyo  tangu majuzi.

Kasimu Njohole aliwahi kuimiliki Bendi yake iliyojulikana kwa jina la New Ifakara Jazz Band ambapo mashabiki kutokana na umahiri wake wakaibadilisha jina na kuuita Njohole Jazz Bendi mwaka 1960.

Mbali ya kumiliki Bendi Kassimu Njohole aliwahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kati ya  mwaka 2000 hadi mwaka 2005.

 Hawa amesema mwaka 1984 hadi mwaka 1988 Marehemu alikuwa anaonesha sinema sehemu mbalimbali nchini Tanzania, na mwaka 1988 hadi mwaka 1990 alijiunga na Siasa na Mwaka 1994 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Lipangalala. Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Ifakara na alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kiolmbero hadi Mwaka 2005.

Mwaka 2006 alichaguliwa na uongozi wa CCM ngazi ya Wilaya kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilombero kwa muda wa miaka miwili badala ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilombero Bwana Kassimu Kulolela kufariki dunia. Bi Hawa Njohole amesema Mwaka 2008 aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Maji  Wilaya ya Kilombero hadi kifo chake. Marehemu ameacha Watoto Sita wakiume  watatu na wakike watatu.

Marehemu Kassimu Hassan Njohole atazikwa leo Septemba13 majira ya saa kumi jioni katika Makabuli ya ukoo waNjohole yaliyopo nyumbani kwake.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU, MAHALA PEMA PEPONI- AMINA

Makundi makubwa ya Mifugo yaondoka Ulanga/Kilombero

Na Senior Libonge,Kilombero

MAKUNDI makubwa ya  mifugo yameanza kuondoka katika bonde la Mto Kilombero wakitekeleza agizo la serikali la kutaka mifugo yote iliyovamia katika bonde hilo kutolewa kwa hiari kabla ya nguvu za dola kuanza kutumika hapo Septemba 7 mwaka huu.


Nimeshuhudia malori makubwa yakiwa yamebeba mifugo huyo katika mji wa Ifakara tayari kwa safari ya kusafirisha mifugo hiyo na kuipeleka kusini mwa Tanzania kwenye mkoa wa Lindi ambapo serikali imetenga eneo maalum la kuishi mifugo.

Juzi viongozi wa wilaya zote mbili za Kilombero na Ulanga walikuwepo mjini Ifakara tayari kwa kuruka na ndege ndogo iliyoletwa na serikali kwa ajili ya kukagua mifugo ama wakulima waliobaki katika maeneo yaliyopigwa marufuku kuwepo na kweli zoezi hilo lilifanyika kwa umakini.

Katika ziara hiyo timu hiyo iliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala na yule wa Ulanga Francis Miti walitembelea bonde lote la Kilombero ili kujionea uharibifu uliofanyika na kwa kiasi kikubwa walibaini kuwa mifugo mingi imeondoka katika bonde hili isipokuwa kwa wafugaji wachache ambao wamejifanya kuificha mifugo yao katika baadhi ya misitu ndani ya bonde hilo.

Baada ya kumaliza kuzungukia bonde hilo wakuu hao wa wilaya walisema kuwa operesheni ya kuwaondoa wafugaji hao imekwisha anza na zoezi linalofanyika hivi sasa ni viongozi wa vijiji na vitongoji kuwahamasisha wafugaji wote waliokuwepo maeneo hayo kuondoa haraka mifugo yao na kubakia ile mifugo halali inayotakiwa kubaki maeneo hayo.

Mifugo halali ni ile iliyowekwa alama na ambayo imekubalika na wananchi wa kijiji husika kuwepo maeneo hayo hasa kwa kuzingatia ukubwa wa eneo husika na mahitaji halisia ikiwemo ya ng’ombe wa kilimo(maksai).

Kwa sasa mifugo mingi imebainika ipo pembezoni mwa milima ya Udzungwa katika tarafa ya Mlimba ambapo haijajulikana kuwa wafugaji hao wameificha mifugo yao maeneo hayo ama wapo njiani kuisafirisha kuipeleka mikoa ya Iringa na Mbeya.

Hata hivyo wafugaji hao wavamizi sambamba na wakulima walioingia katika maeneo ya hifadhi wamepewa tahadhari kuwa kauli ya serikali ipo palepale ya kutaka wote watoke maeneo hayo ukizingatia kuwa serikali haitaki kutumia nguvu kuwaondoa ukizingatia kuwa ni wananchi halali wan chi hiyo.


Ila taarifa imesema kuwa serikali haitashindwa kutumia nguvu kuwaondoa wavamizi hao kama wakiendelea kukaidi agizo la kutaka kutoka eneo hilo ukizingatia mpango wa serikali hivi sasa ni kuliona bonde la Kilombero likirudi katika hali yake ya zamani ya kuwa na ardhioevu kwa ajili ya kilimo na hifadhi tofauti na hivi sasa ambapo asilimia kubwa ya bonde hilo limeharibika kutokana na uvamizi wa mifugo na wakulima.

Wanakijiji Ruaha waangua Kilio mbele ya Waziri

Na Senior Libonge,Ulanga

KATIKA kuonyesha kuwa amekerwa na uharibifu mkubwa wa mazingira kwa ukataji na uchomaji ovyo misitu ya asili mwananchi wa kijji cha kituti tarafa ya Ruaha wilayani Ulanga,Metrucy Albert,ameangua kilio  mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejamenti ya Utumishi wa Umma,Celina Kombani wakati akimuelezea kukithiri kwa vitendo hivyo katika kijiji chao .
Albert aliangua kilio hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho baada ya kumalizika kwa hotuba  Waziri Kombani ambaye ni mbunge wa jimbo la Ulanga mashariki (CCM) baadaye na kuruhusu wananchi wa kijiji hicho kutoa kero zao mbalimbali zinazowakabili .
Baada ya kupewa nafasi hiyo kutoa kero hiyo,Albert alieleza kuwa hivi sasa kijiji hicho kimevamiwa na maharamia mbalimbali ambao wamekuwa wakikata misitu na kuchoma moto ovyo kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ya kijiji hali ambayo imekuwa ikitishi ukame na kuathiri upatikanaji wa mvua.
Alisema licha ya jitihada mbalimbali wanazofanya za kuhakikisha wanadhibiti uharibifu wa maliasili hizo ikiwemo uvunaji wa mbao na wanyama wanaotoka pembezoni ya mbuga ya Serue zimeshindikana kutokana na mbinu mbalimbali zinazotumiwa na mahalamia hao kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ya kijiji hicho.
Naye Lucas Talimo,alisema kuwa maliasili hizo ambazo ni pamoja na madini wao kama wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakishindwa kufaidika nazo licha ya kuzilinda na badala yake wageni ndio wamekuwa wakijinufaisha nazo kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo.
Aliomba Serikali kuingilia kati vinginevyo malisili hizo zinaweza kutoweka wakati wowote kutokana na vitendo vinavyofanywa na mahalamia hao katika kata hiyo .
Akizungumzia hilo,Waziri Kombani aliagiza Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Ulanga kupitia ofisi ya Maliasili wilaya kulishughulikia suala hilo mara moja ili kuzuia kutoweka kwa maliasili hizo zinazockuliwa kinyemela na mahalamia hao.


Wednesday, September 12, 2012

Jumuia ya Wazazi Kilombero yapata viongozi

Na Henry Bernard Mwakifuna- Ifakara

Bwana Julius Ngerangera  amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kilombero katika uchaguzi ulioamua matokeo jana Jioni.

Bitheobista Rivumbi amechaguliwa kuwa Katibu wa Halmashauri huku Wajumbe  wawakilishi taifa ni Benjamini Masepo, Cyprian Kifyoga na Mariam Matalasa.

Wajumbe wa Baraza la Wazazi Wilaya  ni Ally Bendera ,Catheline Singundali na Hassan Goa Goa .
 Uchaguzi wa jumuiya ya wazazi uliofanyika September 11 katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni  Ifakara-Kilombero .

Uchaguzi huo ulianza na ufunguzi wa  uliofanywa na Bw.Cyprian Kifyoga ambaye aliyekuwa mwenyekiti aliyemaliza muda wake ambaye aliwataka wa wanachama kudumisha mshikamano huku akisema aliipokea Jumuiya  ikiwa na wanachama Elfu nne na mia tatu mpaka anapotimiza muda wake amefanikiwa kuwapata wanachama Elfu kumi na mbili

Tuesday, September 11, 2012

Mahenge wapata Tsh. 42 Mil kwa ajili ya Mradi wa Maji

Na Senior Libonge, Mahenge


WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ameahadi kutoa kiasi cha shilingi milioni 42 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji katika Mji wa Mahenge uliopo katika tarafa ya vigoi  wilayani ulanga mkoani Morogoro.

Mji wa Mahenge  unakabiliwa na uhaba wa  maji kutokana na kutokana na miundombinu yake kuchakaa ulihaidiwa kumalizika kwa tatizo hilo  na Rais Jakaya Kikwete alipotembelea wakati wa ziara yake mapema mwaka 2009.

Katika kutatua tatizo hilo la maji,Rais Kikwete alitoa kiasi cha shilingi milioni 200 ili kujengwa kwa miundombinu ya maji ambapo ilibainika ili kukamilisha mradi huo kulikuwa kunahitajika kiasi hicho cha fedha.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Ulanga, iliyosomwa na kaimu mkuu wa wilaya hiyo  Prisca Shewali,Mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Mashariki  Celina Kombani alisema  kuwa wizara ya maji imeahidi kulimaliza tatizo la maji kwa kuleta fedha za kumalizia  mradi wa ujenzi

Alisema pamoja na mradi huo kuongezeka gharama lakini waziri wa maji Profesa  Jumanne Maghembe amuahidi kuwa mara fedha zitakapoingia wizarani kwake kipaumbele kitakuwa ni katika mji wa mahenge.

Kombani ambaye pia ni Waziri wa  nchi, Ofisi ya Rais Menejamenti ya Utumishi wa Umma,alisema kuwa kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha kukamilisha kabisa mradi huo mkubwa wa maji na hivyo kumaliza kabisa tatizo hilo la ukosefu wa maji.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya maji ambayo inaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali ya tarafa ya vigoi mhandisi wa maji wilaya ya ulanga  Patrice Jerome, alisema mpaka sasa wameshafikia katika hatua ya usambazaji wa mabomba ambayo yamekamilika katika maeneo mbalimbali.

Mradi huo wa maji uliahidiwa na Jakaya Kikwete wakati wa ziara zake alizofanya wilayani Ulanga ambapo awali mradi huo ulikuwa ulikuwa na gharama ya shilingi milion 200 ambapo kwa sasa inadaiwa kupanda na kufikia shilingi milioni 300.
Mwisho.

Monday, September 10, 2012

MKUU WA WILAYA AWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA SAHIHI

Na Henry Bernard Mwakifuna- IFAKARA


Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassani Masala amewataka wakazi wa Kilombero kuacha kutoa taarifa zisizo na ukweli kuhusu uhamaji wa maeneo Tengefu ya Bonde la Kilombero na  atakaye kamatwa  anatoa taarifa za uongo kuhusiana na kuhama kwa wavamizi atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Bwana Masala amesema hayo wakati akifunga  Mdahalo wakukuza uwajibikaji wa Viongozi na Wawakilishi  wa Wananchi kwa Jamii  ulioandaliwa na Mtandao wa Azaki Mkoa wa Morogoro {UNGO}kwa kushirikiana na The Foundation for Civil Society uliofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Vijana(John Paul II ) uliopo mjini Ifakara.

Ametoa tahadhari hiyo kwa baadhi ya wananchi na viongozi wanaowapotosha wananchi juu ya zoezi la kuhama kwa wavamizi wa maeneo ya hifadhi na kuondolewa kwa mifugo vamizi.

 Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilombero amewapongeza UNGO kwa kutoa Elimu kupitia mdahalo huo na amewaomba  kuzidi kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuleta maendeleo na kutoa Elimu kuhusu utawala bora kwa viongozi na wananchi.

Wakitoa mada ya utawala wa uwajibikaji katika  Usimamizi na Menejimenti ya Rasilimali katika sekta ya Maliasili Bwana Masanja Joram na Christer Njovu wamesema kuwa katika utawala na uwajibikaji kiongozi anatakiwa kuwa mvumulivu wakati watu wanatoa maoni katika mkutano au vikao na pia anatakiwa kukosoa au kukosolewa bila ya kuoneana aibu. Wawezeshaji hao pia wamewataka wananchi kujihusisha kusimamia maeneo ya Uvuvi ili kuzuia uvuvi haramu katika sekta ya maliasili.

Uchaguzi Jumuiya ya Wazazi Kilombero leo

Henry Bernard Mwakifuna, Kibaoni-Ifakara.
 
Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kilombero unatarajifanyika Kesho katika Ukumbi wa Mazingira Kata ya Kibaoni mjini Ifakara baada ya kuahirishwa kutokana na ukata.Katibu wa Elimu,Malezi,Uchumi na Mazingira wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kilombero  Bwana Benjamini Masepo amesema uchaguzi huo Septemba 11 na uliahirishwa toka Septemba 6 kufuatia  ukata ambao kwa sasa wamefanikiwa kuweka mambo sawa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya Wajumbe watakao toka nje ya Mji wa Ifakara.Ametaja baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo watatoka Kata za Mlimba,Mngeta,Mang’ula na Kidatu.

MTENDAJI MACHIPI- IFAKARA MBARONI KWA UBADHIRIFU


Shule ya Sekondari Ifakara (Machipi), ikionekana kwa mbali




















Na Henry Bernard Mwakifuna, IFAKARA

Bwana  Ally Mahachi, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Machipi Kata ya Michenga Wilayani Kilombero  anashikiliwa na  Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa tuhuma   ya wizi wa fedha za Wananchi Shilingi Milioni Saba na Elfu Arobaini(7,040,000). 

Mtendaji huyo anashikiliwa na jeshi hilo tangu sept 4mwaka huu baada ya wananchi kuunda tume ya uchunguzi wa fedha za miradi iliyopo na inayotarajiwa kuanza na kugundua baadhi ya miradi mtendaji amewadanganya Wajumbe fedha zilizolipwa.

Baadhi ya wajumbe wa Serikali ya kijiji hicho wameeleza kuwa  kuna  Fedha zilitolewa na Mfuko wa Jimbo la Kilombero  kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima vya Maji na uuzwaji wa eneo la ujenzi wa  Mnara tangu mwaka 2011, hata hivyo hadi sasa fedha hizo hazijulikani zilipo.



Njia ya kuelekea Mnarani

Wajumbe hao wamesema kuwa  Bwana Mhachi alifanya udanganyifu alipokuwa anatoa taarifa katika kijiji hicho cha Machipi kuwa amepokea shilingi laki saba(700,000) kwa ajili ya eneo la mnara hali ambayo siyo kweli. Uchunguzi wa Tume hiyo umegundua kuwa fedha zilizolipwa ni shilingi milioni 5,290,000/=na fedha zilizotolewa na mfuko wa jimbo ni shilingi milioni 1,750,000/= Jeshi la Polisi limethibitisha kukamatwa kwa Mtendaji huyo Bwana Mahachi akituhumiwa kula fedha za wananchi na upelelezi utakapo kamilika atafakishwa Mahakamani

Sehemu iliyouzwa kwa ajili ya ujenzi wa Mnara


MALALAMIKO 35 YAFIKISHWA TAKUKURU

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Wilayani Kilombero imepokea  jumla ya malalamiko 35 kutoka sehemu mbalimbali za Wilaya hiyo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu ambayo hadi sasa yanaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi.                                                                                          

Taarifa  iliyotolewa  kwa Waandishi wa Habari na Afisa wa Takukuru Bw.Festo Mdede  imeeleza kuwa  hadi  sasa kuna kesi tano [5]za kukamatwa na Rushwa ambazo bado zinaendelea kusikilizwa Mahakamani.

Mbali ya Kesi hizo Afisa huyo amesema kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [w]Kilombero inatarajia kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea ujasiri wa kutoa ushirikiano katika suala la kuzuia na kupambana na Rushwa ndani ya Wilaya hiyo.
  
Hata hivyo amesema kuwa mbali na kutoa elimu kwa wananchi taasisi imejiwekea mikakati ya  kufanya Warsha fupi ili  kupokea mawazo na ushauri  kutoka kwa wananchi kwa lengo la  kujenga ushirikiano utakao- saidia kurahisisha kazi ya kuzuia na kupambana na Rushwa .

Ametoa Wito kwa Wafanyakazi wa nyanja mbalimbali kufuata sheria za kazi  na kutoruhusu kutoa wala kupokea Rushwa bali ni kupambana kikamilifu  kuzuia Rushwa  ili wawe mfano mzuri na wa kuigwa katika jamii.

KUNDI MATANO YATUPWA NJE NGOMA ZA UTAMADUNI

Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.

Makundi matano kati ya 17 yaliyokuwa yakishiriki Ngoma za Utamaduni yametolewa na Majaji kufuatia kupata alama chache.

Baadhi ya vigezo vilivyotumika katika Tamasha hilo ni pamoja na Ujumbe, Mpangilio wa Sauti, uchangamfu wa Wachezaji, Sare na Matumizi ya Muda.

Mratibu Pacha wa Tamasha hilo Joseph Mlango amevitaja Vikundi vilivyotoka ni Segere cha Machipi, Tupendane cha Michenga, Kasi Mpya cha Mlabani, Libeneke cha Lipangalala na Kinyago cha Viwanja Sitini vyote Wilayani Kilombero.

vikundi vilivyobaki ni Gunia Tupu Halisimami cha Mlabani,Ya kale Dhahabu cha Miomboni-Mofu, Lumumba cha Mangwale,Toma Toma cha Kikwawila, Twitange cha Mangwale, Maji Marefu cha Katindiuka na Saga na Kukoboa cha kibaoni.

vingine Vilivyobaki ni Sega Dansi cha Mlabani, Fuka Fuka, Lizombe cha Machipi na Iragua Group kikundi pekee kutoka Wilayani Ulanga.

Tamasha hilo lililoandaliwa na Tumaini Development and Counseling Trust (TUDECO) wakishirikiana na Makutano Club Ifakara lilianza Septemba ya Pili na Fainali yake inatarajiwa kufanyika Septemba ya 30 Mwaka huu.