HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Wednesday, January 9, 2013

UBORESHAJI WA KILIMO CHA MPUNGA ULANGA/KILOMBERO


Na Senior Libonge,Kilombero

KITUO cha Utafiti wa Kilimo(KATRIN) kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro kimeamua kuboresha  mbegu ya mpunga aina ya Saro 5 kutokana na mbegu hiyo kupendwa zaidi na wakulima wengi nchini hasa kutokana na mchele wake kunukia vizuri.

Akizungumza na mkuu wa wilaya ya Kilombero baada ya kutembelea kituo hicho,Kaimu afisa mfawidhi wa kituo Dk Jerome Mghase amesema wakulima wengi wa mpunga nchini wanapendelea mbegu za Saro 5 kutokana na mchele wake kuwa na uhakika wa soko na wao kwa kutambua hilo wameamua kuboresha mbegu hiyo.



AKINA MAMA WAKIPALIA MPUNGA KATIKA ENEO LA IGAWA, Picha kwa Hisani ya Juma Mtanda Blog Archieve 


Dk Mghase amesema hiyo yote inatokana na mafanikio ya utafiti wa zao la mpunga ambapo licha ya kuboresha mbegu aina ya Saro 5 pia kituo kimewezesha upatikanaji wa mbegu nyingine zilizoboreshwa zikiwemo TXD 85,TXD 88 na NERICA za ukanda wa juu na milima zikiwemo Nerica 1 hadi 7 na pia WAB 450-12-2BL1-DV4.

Amesema pia kituo kimefanikiwa katika upatikanaji wa mbegu zenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa kimyanga ambazo ni Kalalu na Mwangaza huku pia teknolojia mbalimbali za uzalishaji wa mpunga zimetolewa kwa wakulima  zikiwemo kupanda kwa nafasi,matumizi bora ya mbolea,kiwango cha mbegu za kupanda,udhibiti wa magugu na muda muafaka baada ya kuvuna.



Kaimu afisa mfawidhi wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Katrin Dk Jerome Mghase akimpatia maelekezo mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala jinsi mbegu ya mpunga zinavyokubaliana na aina mbalimbali za udongo kabla ya kupelekwa mashambani.

Kaimu afisa mfawidhi huyo ameendelea kusema kuwa kituo hicho kwa sasa ni taasisi mahiri ya mpunga kwa ukanda wa afrika mashariki baada ya kuteuliwa mwaka 2008 kupitia mpango ujulikanao kama Eastern Africa Agriculture Productivity Program(EAAPP) na mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia.

Amesema katika mradi huo nchi ya Tanzania unahusisha zao la mpunga,Kenya(Maziwa),Uganda(Mihogo) na Ethiopia(Ngano) na mradi huu ulizinduliwa rasmi April 2010 na hadi sasa zaidi ya tafii 20 za kikanda zinaratibiwa na KATRIN.

Kwa mujibu wa afisa huyo amesema kuwa kituo hicho kwa sasa kinazalisha mbegu za mpunga ambazo huuzwa kwa wakala wa mbegu wa Taifa(ASA) ambao huzizalisha kwa wingi na kuuza kwa wakulima nchi nzima na pia kituo kinawapatia wakulima mmoja mmoja au kupitia vikundi kadri ya mahitaji yao.

Aidha kituo mbali ya utafiti wa zao la mpunga pia wamepewa jukumu la kutafiti aimba mbalimbali za mazao ya viungo kama vile Vanila,Tangawizi,Pilipili manga,Iliki,Mdalasini na Kokoa na utafii huo utawezesha wakulima kupata mazao mbadala ya biashara mbali na mpunga ambao hautoshelezi mahitaji yao ya kiuchumi.

Hata hivyo Dk Mghase amesema licha mafanikio hayo pia kituo hicho kina changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo ni idadi ndogo ya watafiti na watumishi wengine,uchakavu wa miundombinu na vifaa,uvamizi wa maeneo ya kituo na wanajamii wanaokizunguka na ukosefu wa huduma muhimu hasa afya.



Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala(mwenye suti)akimsikiliza mkufunzi wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Katrin Benjamin Mfupe juu ya uboreshaji wa mbegu za mpunga ili kufanikisha dhima ya taifa ya  uzalishaji wa chakula mkoani Morogoro na jicho lipo wilayani Kilombero


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema kuwa nchi nyingi zimeendelea kutokana na utafiti na wao kama serikali wana jukumu kubwa la kuzalisha katika kilimo ila hawataweza kufanikiwa bila kuona wataalamu wanashughulikiaje kilimo hicho.

Masala amesema serikali bado ina mkakati wa kuboresha taasisi zake ikiwemo Katrin na kwa kuona hilo wameamua kukiteua kituo hicho ili kufanya utafiti na kuzalisha mbegu bora zaidi ili kufanikisha mipango ya Famoghata na Sagcot huku pia akiwataka wataalamu hao kuwapatia elimu wakulima ili waweze kuzalisha mazao bora zaidi na kukuza vipato vyao.

No comments:

Post a Comment