HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Thursday, January 31, 2013

JESHI LA POLISI YASUSIWA MAITI YA MFUGAJI MOROGORO.


MAUAJI YA MFUGAJI ULANGA MOROGORO

Habari yote kwa Hisani ya Juma Mtanda, Morogoro




 Mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti kushoto akizungumza na wafugaji (hawapo pichani) baada ya wafugaji hao kususia maiti kwa siku mbili wakidai mpaka serikali itimize masharti yaliyowekwa na familiakushoto ni Kamanda wa polisi Morogoro Shilogile na katikati ni Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ulanga Halidi Nalyoto.
 Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Francis Miti kulia akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kushoto baada ya kamanda huyo kukataliwa na familia ya marehemu Baya Kidinga (20) kutambua mwili wa marehemu kisha kukubali kuupokea na kwenda kuuzika.



Sehemu kubwa ya wafugaji wilaya ya Ulanga wakimsubiri mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti baada ya familia ya marehemu kukataa kutambua mwili wa marehemu ndugu yao anayedaiwa kupigwa risasi na askari polisi waliokuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatilia wa mifugo katika hifadhi ya bonde la mto Kilombero kuupokea na kwenda kuulizika yaliyotolewa na kamanda wa polisi ya mkoa Morogoro huo. 



 Mmoja wa wafugaji akizungumza jambo mbele ya Kamanda wa polisi hayupo pichani. 


 Kitambulisho cha marehemu Baya Kidinga (20) cha kuhitimu mafunzo yaMgambo mkoa wa Morogoro.



 Marehemu Baya Kidinga (20) enzi za uhai wake.


 Eneo ambalo linadaiwa marehemu Baya Kidinga (20) alipigwa risasi na kufariki dunia baada ya askari polisi kumfyatulia na kupoteza maisha damu ikiwa imetapakaa chini, picha iliyopigwa januari 27/ 2013.

 Sehemu ya wafugaji wa jamii ya wasukuma wakimsikiliza kamanda wa polisi Morogoro (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo. 


Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jidai mkoa wa Morogoro Hamis Seleman kulia akimsihi ndugu wa marehemu,Baya Kidinga (20), Madaha Shirinde baada ya kususia maiti mpaka serikali itimize mashrti yaliyowekwa na familia hiyondipo wakulibali kuchukua mwili na kuuzika.



Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile kushoto akimsikiliza Manogeleku Kisandu kulia ambaye ni shahidi aliyeshuhudia tukio la kupigwa risasi marehemu Baya Kidinga (20) na askari polisi januari 31/ 2013 katikaKitongoji cha Lugangeni Kijiji cha Ipera Asilia Tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.




 Baba mzazi wa marehemu, Baya Kidinga (20), Katambi Jidiga (katikati) akibembelezwaa na mtoto wake Madaha Shirime kushoto na afisa mtendaji kijiji cha Ipera Asilia, Zikeni Magoha kulia.

JESHI LA POLISI YASUSIWA MAITI YA MFUGAJI MOROGORO


 Baba mzazi wa marehemu, Baya Kidinga (20), Katambi Jidiga kulia akimsikiliza Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile kulia akimweleza jambo juu ya tukio la mauaji ya mtoto wake lililotokea januari 26/ 2013 baada ya kudaiwa askari polisi waliokuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatilia kumpiga risasi.

HABARI KAMILI HII HAPA.


JESHI la polisi Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro limelazimika kurudisha jumla ya sh 10 milioni zinazodaiwa kuporwa kwa mfugaji wa jamii ya kisukuma baada ya kumuuwa kwa kupigwa risasi mdogoni hatua hiyo ilikuja baada ya kususiwa maiti hiyo kwa siku mbili.

Hatua ya utekelezaji wa urudishaji wa pesa hizo zilizokuwa zikilalamikiwa na ndugu wa mfugaji huyo aliyefahamika kwa jina la Baya Katambi Kidiga ni sehemu ya makubaliano yaliofikiwa mbelee ya Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Francis Mitti na Mkuu wa jeshi la polisi Mkoani hapa Faustine Shilogile, Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoani hapa Hamisi Selemani, Mkuu wa polisi Ulanga.

Sakata hilo la mauaji na uporaji linaloendelea kulichafua jeshi la polisi Mkoani Morogoro limetokea tarehe 26, January 2013 katika Kitongoji cha Lugangeni Kijiji cha Ipera Asilia Tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.

Awali polisi hao walidaiwa kutekeleza mauaji hayo majira ya saa 4 kwa kumpiga risasi marahemu huyo na kuuchukua mwili wake na kuupeleka kituo cha afya Mtimbira haraka haraka kwa kutumia gari la polisi linalodaiwa likishiriki katika operationi ya kukamata mifugi wilayani humo kutoka kwenye hifadhi ya bonde la mto Kilombero.

Baadhi ya masharti ambayo polisi walitakiwa kutekeleza ni kutoa ripoti ya kina ya uchunguzi wa kifo kutoka kwa daktari ambao utabainisha kuwa marehemu Baya Kidinga (20) amefariki dunia kwa kupigwa kwa risasi.

Hatua ambayo jeshi hilo lilitekeleza kwa kutoa ripoti daktari alitoa riporti ya mauaji hayo yaliodhibitisha bila shaka kuwa ameuwawa kwa kupigwa risasi ambayo ilikubaliwa.

Sharti la pili ambalo polisi walitakiwa kutekeleza ni kujua ni kwanini mwili wa marehemu ulihamishwa toka katika eneo la tukio kwa haraka bila hata kutoa fursa ya ndugu zake kuwepo na baadhi ya ndugu na majirani waliokuwa waliotaka kufuatilia juu ya mkasa huo walizuiwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alikuwa wa kwanza kuonja makali ya wananchi ambapo aliwasili majira saa saa 5 asubuhi siku ya tukio na jopo la maafisa wa jeshi hili huku idadi ya wafugaji wakiendelea kukusanyika kwa kuulizwa maswali yaliomshinda ikiwemo kutakiwa kueleza kama operationi ya kuwaondoa wafugaji katika hifadhi ya bonde la mto Kilombero ipo au imekwisha na eneo ambalo marehemu ameuwawa ndani ya hifadhi ama laa.

Shilogile akijibu maswali hayo alisema kuwa operationi anachojua yeye ilisitishwa katika wilaya ya Kilombero lakini kwa wilaya ya Ulanga hilo hatakuwa na jibu la swali hilo lakini swahili litajibiwa na mkuu wa wilaya ya Ulanga pindi atapofika.

“Poleni kwa msiba huu mimi nimekuja na timu ya wenzangu akiwemo mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wetu lakini natumaini kila kitu kitaenda sawa na kingine mimi nimekuja eneo la tukio kutaka kujua ukweli wa tukio hili ili kubaini ukweli wenyewe ikiwemo nani amefanya kosa na mpaka sasa askari wetu waliohusika katika tukio hilo tayari tunawashikilia kwa ajili ya uchunguzi wa awali na wakibaini sheria itachukua mkondo wake” alisema Shilogile.

Kamanda huyo ambaye alikabiliwa na maswali mengi kutoka kwa wafugaji hao likimwemo la msemaji wa familia hiyo ya marehemu, Baya Kidinga (20), (Madaha Shirinde) aliyeuliza kwa kutaka ufafanuzi wa kina kwa kuuliza swali je askari aliyepata mafunzo anapaswa kufanya nini pindi anapokabiliana na mtu mwenye silaha za asili ikiwemo fimbo ? ama kutuliza ghasia au vurugu anapaswa kutumia bunduki kwa kupiga mwananchi katika eneo gani ?.

Akijibu maswali hayo Kamanda wa polisi Morogoro, Shilogile alijibu kuwa anapaswa kumpiga mtu risasi kwa kutumia bunduki kwenye miguu na kueleza kuwa yeye amefika eneo hilo na timu yake kwa lengo la kujua mazingira ya tukio lililivyofanywa na askari baada ya kufanya uchunguzi na kuwahoji walioshuhudia.

Majibu hayo ya kamanda yalizusha mzogo mkali kutoka kwa wananchi hao na kuzalisha maswali mengine likimo la kuhoji kwanini askari wako ametumia silaha kwa kumpiga marehemu risasi mdogoni kama amepata mafunzo ?.

Kamanda huyo alieleza tena kwa umati wa wafugaji hao kwa kusema kuwa kwa wakati huo atakuwa na jibu la swali hilo na kuongeza hawezi kujua kilichompata askari huyo mpaka ametumia silaha kwa kumpiga risasi marehemu jambo hilo tutalifanyia kazi baada ya kukabilika kwa uchunguzi wao. 

Maswali hayo hayakuweza kuwaridhisha umati wa wananchi na upande wa familia ya marehemu na kumtaka kamanda huyo awasiliane na mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti kwa kuhoji kwa nini wewe Kamanda umetembea umabli mrefu kufika eneo la tukio na mkuu wako wa wilaya ambaye yupo jirani ameshindwa kufika eneo la tukio ?.

Mzozo huo ulidumu kwa muda wa masaa mawili bila kufikia muafaka katika siku ya pili baada ya tukio kutokea ambayo kamanda wa polisi alishindwa kutimiza malengo yake, likiwemo kuwashawishi ndugu wa marehemu wakubali kuutambua mwili wa marehemu, kupokea uchunguzi wa daktari na kuchukua mwili wa marehemu jambo ambalo alilazimika kuwasiliana na mkuu wa wilaya ili kufika eneo la tukio.

DC ULANGA.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti aliwasili katika eneo la tukio la mjira ya saa 10:30 alasiri na kuanza kuwapa pole umati uliokuwa ukimsubiri ili kutatua kero za wananchi hao.

Miti baada ya kutoa pole kwa wafiwa alianza kutoa ufafanuzi juu ya zana iliyojengeka kwa wananchi hao kuwa marehemu amepigwa risasi katika zoezi la operesheni na kuwa askari hao hawakuwa katika operesheni bali walikuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto wa Kilombero na kuwa wanaobainika hukamatwa na kutozwa faini kisha kuwapa ovyo waliende tena katika bonde la mto Kilombero.

“tukio hili hakuna anayefurahia hata kidogo niwaeleze kuwa operesheni haipo kilichopo sasa ni udhibiti na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto wa Kilombero na operesheni tayari ilishaisha tangu januari mosi mwaka huu” alisema Miti.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya naye alikumbana na maswali juu ya watendaji wake waliokuwa katika operesheni na udhibiti na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto Kilombero na kuwa daktari wa mifugo wilaya Ulanga, Fredrick Sagamiko amekuwa akidaiwa kukiuka utaratibu wa faini.

Mselengeti Mipawa (41) alimweleza mkuu wa wilaya katika tukio hilo kuwa daktari huyo amekuwa akitoza faini kati ya sh60,000 hadi 100,000 pindi anapokamata mifugo badala ya faini iliyoidhinishwa na serikali ya kiasi cha sh44,000 kwa ng’ombe mmoja jambo ambali wamekuwa wakilipia na kuwarudisha nyumba katika harakati za maendeleo.

Mipawa alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa daktari huyo wa mifugo wilaya ya Ulanga, licha ya kukiuka utozaji wa faini pia amekuwa akimakata na mifugo ambayo haiku kwenye listi ya ukamataji wa operesheni hiyo wakiwemo kukamata mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na punda na kutozwa faini kubwa kuanzia kiasi cha sh 700,000 na kuendelea kulinagana na uwingi wa mifugo hiyo.

Miti alisema kuwa baada ya kupata tuhuma zinazo mwelekeza daktari wa mifugo wilaya Ulanga, Fredrick Sagamiko yeye atawasilisha tuhuma hizo kwa mwajili wake ambaye ni mkurugezi wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga ili uchunguzi ufanyike na kama itabainika sheria itafuata mkondo wake.

Aliwaeleza umati huyo kwa kuwataka wafugaji waache tabia ya kuwashambulia askari na kuwataka askari nayo kutotumia nguvu kubwa wakati wa vurugu pindi inapotokea hiyo itasaidia kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya jeshi la polisi na wananchi.

Mkuu huyo alilazimika kuwashawishi ndugu wa marehemu wakubaliane na ombi lao la kutaka wakatambue mwili wa marehemu na kupokea uchunguzi wa daktari kisha kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi jambo ambalo lilishindikana kukubali ombi hilo kutokana na kutotimiza madai yao.

Baada ya Kamanda wa polisi na mkuu wa wilaya Ulanga kushindwa kuwashawishi ndugu wa marehemu kuchukua mwili wa ndugu yao msafara wao uliondoka eneo hilo majira ya saa 12:30 jioni na siku ya pili ya januari 28 mwaka huu ikifuatiwa na kutokubaliana hadi gazeti hili liondoka katika eneo la tukio.

Awali Baba wa marehemu Katambi Jidiga alisema kuwa marehemu alitokea mkoani Songea kuuza baadhi ya ng’ombe kwa ajili kulipa madeni ya mifugo iliyokamatwa katika operationi, awali imetajwa mbuzi 100 alilipa lakini saba, ngombe inadaiwa akikuwa akidaiwa 10 milioni na mara ya tatu ngombe wake waliokamatwa na askari hao alikuwa akidaiwa sh milioni 3.



Thursday, January 17, 2013

IFAKARA yamlilia Regia Mtema


Senior Libonge,Ifakara


WAKAZI wa mji wa Ifakara wilayani Kilombero jana wamefanya maandamano ya amani ya kumkumbuka ya mwaka mmoja tokea kitokee kifo cha aliyekuwa mbunge wa viti maalum katika jimbo la Kilombero Regia Mtema ambapo maandamano hayo yalipokelewa na mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala.

Maandamano hayo yalianzia katika kituo cha mafuta cha Ester kisha kumalizikia katika makaburi ya Lipangalala ambapo marehemu ndipo alipozikwa na baada ya kufika hapo shughuli za kuweka mashada ya maua na kuwasha mishumaa zilifanyika na zote hizo ziliongozwa na Masala na famila ya marehemu kupitia Regia Mtema Foundation.





MKUU wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala akiwasha ishara katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum jimbo la Kilombero Regia Mtema ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kwa kifo chake

Licha ya kufanya maandamano hao ya amani Regia Mtema Foundation siku moja kabla ya maandamano hayo kwa kushirikiana na wananchi mbalimbali walipanda miti katika shule mbalimbali za msingi zilizopo katika mji wa Ifakara na zoezi la mwisho kufanyika ni kutoa misaada mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto wenye matatizo ya akili cha Bethlehem kilichopo Kibaoni mjini Ifakara.

Shughuli za kumkumbuka marehemu Regia Mtema zilifanyika pia jijini Dar es Salaam hapo Januari 14 katika hoteli ya Peacock ambapo  mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia marehemu ikiwemo historia ya Regia iliyowasilishwa na Mbunge David Kafulila,mada juu ya rushwa iliyowasilishwa na Takukuru na Ulemavu sio kutoweza iliyowasilishwa na Shida Salum mwenyekiti wa CHAWATA

MKUU wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa viti maalum jimbo la Kilombero Regia Mtema baada ya kupokea matembezi ya mshikamano yaliyofanywa na wananchi wa Kilombero katika kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo chake

Pia Mh January Makamba aliwasilisha mada ya nafasi ya kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia,makala za Regia na pia nasaha kutoka kwa wabunge  Mh Zito Kabwe na John Mnyika,Hussen Bashe na mzee Mtema zilitolewa.

WAKAZI wa mji wa Ifakara wakiwa katika matembezi ya mshikamano ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kitokee kifo cha mbunge wa viti maalum jimbo la Kilombero Regia Mtema.(Picha zote na Igamba Libonge).


Marehemu Regia Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu Januari 14 mwaka jana baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupinduka na kusababisha kifo chake na baadaye kuzikwa mjini Ifakara katika mazishi yaliyokusanya watu wengi na kuongozwa na Rais Jakaya Kikwete

Sunday, January 13, 2013

Tamasha kubwa kumuenzi Regia Mtema laja


Na Senior Libonge, Ifakara

WAKATI familia ya aliyekuwa mbunge wa viti maalum jimbo la Kilombero marehemu Regia Mtema ikiandaa tarehe 14 Januari mwaka huu kuwa ni siku ya Regia kwa kuandaa hafla kubwa jijini Dar es Salaam,pia shughuli maalum zitafanyika wilayani Kilombero ambapo ndiko marehemu alipokuwa akitumikia wananchi wa jimbo hilo.


Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero (Viti Maalum CHADEMA) Marehemu Regia Mtema

Akizungumza na Blog blog hii mjini Ifakara,mratibu wa shughuli hizo wilaya ya Kilombero Antony Kamonalelo amesema kuwa amepewa jukumu hilo kutoka kwa famila ya marehemu ambao wameanzisha Regia Mtema Foundation na shughuli kubwa zitakayofanyika wilayani hapa ni zoezi la upandaji miti,usafi wa mazingira na matembezi ya mshikamano.

Kamonalelo amesema kuwa shughuli hizo zitaanza tarehe 16 mwezi huu kwa wananchi kupanda miti na shughuli itaanza katika shule ya msingi Maendeleo na siku inayofuata litafuatia zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mji wa Ifakara na viunga vyake hasa katika vituo vya kuhudumia watoto wenye matatizo mbalimbali,hospitali ya rufaa ya Mt.Francis na soko kuu la Ifakara.

Kwa mujibu wa Kamonalelo tarehe 18 ndio itakuwa mwisho wa shughuli hiyo ambapo kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoanzia katika mzunguko wa Kibaoni na kuelekea katika makabuli ya kwa Mkuya katika kijiji cha Lipangalala ambako ndiko alipozikwa na wakishafika hapo shughu itakayofuatia ni kufanya usafina kisha kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kumkumbuka kipenzi cha wana Kilombero.

Amesema shughuli zote hizo zitaongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala hivyo kutoa wito kwa wananchi wote wilayani Kilombero bila kujadi itikadi za kisiasa na kidini kujitokeza kwa wingi katika shughuli zote za siku tatu kutokana na marehemu alikuwa mtu wa watu.

Huku shughuli za kumkumbuka marehemu Regia Mtema zikitarajia kufanyika hivyo wilayani Kilombero jijini Dar es Salaam shughuli maalum itafanyika Januari 14 katika hoteli ya Peacock ambapo Regia Mtema Foundation wamesema kuwa kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia marehemu.

Taarifa zilizosambazwa kwa vyombo vya habari na familia ya marehemu zimeeleza kuwa katika siku hiyo maalum wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki na hafla itaanza saa 9 alasiri na kumalizika saa 2 usiku katika hoteli ya Peacock na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku.

Kwa mujibu wa famila ya marehemu ratiba kamili itahusisha matukio kadhaa yakiwemo historia ya Regia itakayowasilishwa na Mbunge David Kafulila,mada juu ya rushwa itakayowasilishwa na Takukuru na Ulemavu sio kutoweza itakayowasilishwa na Shida Salum mwenyekiti wa CHAWATA.

Pia Mh January Makamba atawasilisha mada ya nafasi ya kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia,makala za Regia na pia nasaha kutoka kwa wabunge Mh Zito Kabwe na John Mnyika,Hussen Bashe na mzee Mtema zitatolewa.

Marehemu Regia Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu Januari 14 mwaka jana baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupinduka na kusababisha kifo chake na baadaye kuzikwa mjini Ifakara katika mazishi yaliyokusanya watu wengi yaliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Wednesday, January 9, 2013

UBORESHAJI WA KILIMO CHA MPUNGA ULANGA/KILOMBERO


Na Senior Libonge,Kilombero

KITUO cha Utafiti wa Kilimo(KATRIN) kilichopo wilayani Kilombero mkoani Morogoro kimeamua kuboresha  mbegu ya mpunga aina ya Saro 5 kutokana na mbegu hiyo kupendwa zaidi na wakulima wengi nchini hasa kutokana na mchele wake kunukia vizuri.

Akizungumza na mkuu wa wilaya ya Kilombero baada ya kutembelea kituo hicho,Kaimu afisa mfawidhi wa kituo Dk Jerome Mghase amesema wakulima wengi wa mpunga nchini wanapendelea mbegu za Saro 5 kutokana na mchele wake kuwa na uhakika wa soko na wao kwa kutambua hilo wameamua kuboresha mbegu hiyo.



AKINA MAMA WAKIPALIA MPUNGA KATIKA ENEO LA IGAWA, Picha kwa Hisani ya Juma Mtanda Blog Archieve 


Dk Mghase amesema hiyo yote inatokana na mafanikio ya utafiti wa zao la mpunga ambapo licha ya kuboresha mbegu aina ya Saro 5 pia kituo kimewezesha upatikanaji wa mbegu nyingine zilizoboreshwa zikiwemo TXD 85,TXD 88 na NERICA za ukanda wa juu na milima zikiwemo Nerica 1 hadi 7 na pia WAB 450-12-2BL1-DV4.

Amesema pia kituo kimefanikiwa katika upatikanaji wa mbegu zenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa kimyanga ambazo ni Kalalu na Mwangaza huku pia teknolojia mbalimbali za uzalishaji wa mpunga zimetolewa kwa wakulima  zikiwemo kupanda kwa nafasi,matumizi bora ya mbolea,kiwango cha mbegu za kupanda,udhibiti wa magugu na muda muafaka baada ya kuvuna.



Kaimu afisa mfawidhi wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Katrin Dk Jerome Mghase akimpatia maelekezo mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala jinsi mbegu ya mpunga zinavyokubaliana na aina mbalimbali za udongo kabla ya kupelekwa mashambani.

Kaimu afisa mfawidhi huyo ameendelea kusema kuwa kituo hicho kwa sasa ni taasisi mahiri ya mpunga kwa ukanda wa afrika mashariki baada ya kuteuliwa mwaka 2008 kupitia mpango ujulikanao kama Eastern Africa Agriculture Productivity Program(EAAPP) na mradi huu unafadhiliwa na benki ya dunia.

Amesema katika mradi huo nchi ya Tanzania unahusisha zao la mpunga,Kenya(Maziwa),Uganda(Mihogo) na Ethiopia(Ngano) na mradi huu ulizinduliwa rasmi April 2010 na hadi sasa zaidi ya tafii 20 za kikanda zinaratibiwa na KATRIN.

Kwa mujibu wa afisa huyo amesema kuwa kituo hicho kwa sasa kinazalisha mbegu za mpunga ambazo huuzwa kwa wakala wa mbegu wa Taifa(ASA) ambao huzizalisha kwa wingi na kuuza kwa wakulima nchi nzima na pia kituo kinawapatia wakulima mmoja mmoja au kupitia vikundi kadri ya mahitaji yao.

Aidha kituo mbali ya utafiti wa zao la mpunga pia wamepewa jukumu la kutafiti aimba mbalimbali za mazao ya viungo kama vile Vanila,Tangawizi,Pilipili manga,Iliki,Mdalasini na Kokoa na utafii huo utawezesha wakulima kupata mazao mbadala ya biashara mbali na mpunga ambao hautoshelezi mahitaji yao ya kiuchumi.

Hata hivyo Dk Mghase amesema licha mafanikio hayo pia kituo hicho kina changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ambazo ni idadi ndogo ya watafiti na watumishi wengine,uchakavu wa miundombinu na vifaa,uvamizi wa maeneo ya kituo na wanajamii wanaokizunguka na ukosefu wa huduma muhimu hasa afya.



Mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala(mwenye suti)akimsikiliza mkufunzi wa kituo cha utafiti wa kilimo cha Katrin Benjamin Mfupe juu ya uboreshaji wa mbegu za mpunga ili kufanikisha dhima ya taifa ya  uzalishaji wa chakula mkoani Morogoro na jicho lipo wilayani Kilombero


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala amesema kuwa nchi nyingi zimeendelea kutokana na utafiti na wao kama serikali wana jukumu kubwa la kuzalisha katika kilimo ila hawataweza kufanikiwa bila kuona wataalamu wanashughulikiaje kilimo hicho.

Masala amesema serikali bado ina mkakati wa kuboresha taasisi zake ikiwemo Katrin na kwa kuona hilo wameamua kukiteua kituo hicho ili kufanya utafiti na kuzalisha mbegu bora zaidi ili kufanikisha mipango ya Famoghata na Sagcot huku pia akiwataka wataalamu hao kuwapatia elimu wakulima ili waweze kuzalisha mazao bora zaidi na kukuza vipato vyao.

Sunday, January 6, 2013

HALMASHAURI YA WILAYA YA ULANGA YALIPA MADENI HOSPITALI YA LUGALA


Na Senior Libonge, Ulanga

Halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, hatimaye imeanza kulipa madeni iliyokuwa ikidaiwa na hospitali ya Lugala iliyoko katika tarafa ya Malinyi wilayani humo baada ya kupata fedha zinazotokana na makusanyo ya ndani ya halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Furaha Lilongeri, halmashauri hiyo tayari imeandaa malipo ya zaidi ya Sh40 milioni kwa ajili ya kuilipa hospitali ya Lugala baada ya hospitali hiyo kutoa huduma ya bure kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.

Alisema kuwa halmashauri yake mwaka jana ilisaini mkataba na uongozi wa hospitali ya Lugala ili kuweza kutoa huduma bure kwa makundi hayo huku fedha za kulipia gharama hizo zikipangwa kupatikana na mfuko wa pamoja wa serikali kuu na mapato ya ndani ya nchi.

Hata hivyo, tathimini iliyofanywa na halmashauri ya wilaya ya Ulanga katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji wa mkataba huo kuanzia Julai mpaka Septemba 2012, halmashauri hiyo ilikuwa ikidaiwa jumla ya Sh62.1 milioni.

Lilongeri alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu hizo, ilibainika pia kuwa idadi ya wagonjwa waliokuwa wakitarajiwa kutibiwa katika hospitali hiyo kupitia mkataba huo iliongezeka mara dufu kiasi cha kutishia bajeti ya halmashauri hiyo.

Aliongeza kuwa uchanganuzi uliofanywa na halmashauri hiyo ulionyesha kuwa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo huenda ikaongezeka zaidi na kulifanya deni la halmashauri kupanda na kufikia wastani wa zaidi ya Sh248 milioni kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utekelezaji wa mkataba huo.

Mwenye kiti huyo alidai kuwa kama jinsi ambavyo halmashauri ilivyoadhimia na kuuomba uongozi wa halmashauri hiyo kufanya mazungumzo ya kulekebisha mkataba huo na kuufanya makata huo kuuruhusu wagonjwa kutibiwa baadhi ya magonjwa hususan watoto wenye umri wa miaka mitano na akinamama wajawazito na magonjwa mengine kutibiwa katika zahanati za serikali zilizopo.

“Tumekwisha andaa malipo ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya deni tunalodaiwa na baada ya kuwakabidhi fedha zao tutaomba maongezi yaweze kufanyika ili kuruhusu mkataba huo kufanyiwa marekebisho.



TAMADUNI ADHIMU ZA MAKABILA YA ULANGA KILOMBERO

KAMA HUJAOA TAFADHALI HARUSI YAKO KAFUNGIE KIJIJINI NA UALIKE SANGULA AU MANGONGU UKUZE KIPATO CHA VIJANA NA JIONEE TOFAUTI



MANYANGA SI MCHEZO TENA HASA ZILE ZA VIBUYU NAZO ZITAFUFULIWA. KAMA VILE MAKABILA MENGINE KAMA WANASAI WANAVYOWEZA KUTUMIA UTAMADUNI KUJILETEA KIPATO NA MAENDELEO VIVYO NA MAKABILA YA ULANGA/KILOMBERO YATAHAMASISHWA KUTUNZA MILA NA DESTURI NZURI KWA AJILI YA KUJILETEA MAENDELEO
MLULI HASA KUPITIA MWANZI TEKNOLOJIA USIYOWEZA KUIPATA SEHEMU YOYOTE DUNIANI PIA ITALINDWA KUPITIA KAZI ZA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

MOJA YA MAMBO MUHIMU AMBAYO ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE HAITA LIACHA NI KUTUNZA UTAMADUNI WA MAKABILA ASILIA YA ULANGA NA KILOMBERO HASA KUPITIA NGOMA ADHIMU YA SANGULA NA MANGONGO
UMOJA WETU KATIKA KAZI NI MUHIMU LAKINI PIA KATIKA TONGE, HATUANGALII LA NANI KUBWA ZAIDI ILI MRADI KILA MTU AMESHIBA
WAPOGORO NA WANDAMBA WASIPOKULA WALI WANAONA WAHAJALA, WATOTO WAKIFURAHIA PILAU 
MWAKA HUU 2013 TUPAMBANE NA HIZI KULE NYUMBANI, NYUMBA YA KIJANA ALIYEMALIZA DARASA LA SABA NA KUSHINDWA KUENDELEA NA SHULE...ANAJIANDAA KUOA



Utafiti juu ya Umuhimu wa kuanzishwa kwa Ulanga Community Resource Centre



SAFARI YA NYUMBANI MTIMBIRA MWAKA 2012 NA MKUTANO NA BAADHI YA WANAFUNZI KATIKA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA





WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA WAKIJADILI JUU YA UMUHIMU WA KUWA NA TAASISI KAMA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE



BWANA FRANCIS UHADI (KUSHOTO) AKIWA NA MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA AKIWA KWENYE MICHEZO SHULENI HAPO
MWALIMU NAE ALISEMA KUWA KUNA UMUHIMU MKUBWA WA KUANZISHA TAASISI KAMA HIYO

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA KATIKA PICHA NA FRANCIS UHADI WALIPOTEMBELEWA JIONI WAKATI WA MICHEZO. PAMOJA NAO NI MWALIMU WA MICHEZO. WANAFUNZI KWA UMOJA WAO WALIOMBA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE IANZISHWE HARAKA IWEZEKANAVYO ILI KUWAINUA KIELIMU
WANAFUNZI WAKISIKILIZA KWA MAKINI MCHADALA UKIENDELEA
SUALA LA DARAJA KATIKA MTO KILOMBERO LILIKUWA PIA NI SUALA LILILOJADILIWA NA KUTAKA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE IWAELIMISHE WANANCHI NJIA BORA YA KUDAI UJENZI WA DARAJA HILO
WANAFUNZI WAKIWA KWENYE BAISKELI WAKIWATAZAMA WENZAO WAKIWA KATIKA MICHEZO. USAFIRI WA BAISKELI NI NYENZO HUHIMU INAYOWAWEZESHA WANAFUNZI KUJA SHULE KWA WAKATI
KWA JINSI BARABARA ILIVYOMBAYA KWENDA NA GARI NDOGO PIA NI CHANGAMOTO KUBWA. HATA HIVYO TULIWEZA KUFIKA NA KURUDI SALAMA KWA KUWA MVU ZILIKUWA HAZIJAANZA KUNYESHA
HAIKUWA RAHISI KUWAPATA WANAFUNZI BILA KUPITIA KWA UONGOZI WAO WA SHULE. MWALIMU ALITUSAIDIA KUFIKISHA UJUMBE

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA WAKISILIZA KWA MAKINI MASWALI JUU YA UMUHIMU WA KUWEPO AU KUTOWEPO KWA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE. UTAFITI HUO ULIFANYIKA ILI KUJUA KAMA KUNA UMUHIMU WA KUWA NA TAASISI KAMA HIYO NA KAMA WANAFUNZI WANAONA KUTAKUWA NA FAIDA YOYOTE KWAO KWA KUANZISHWA KWAKE. WENGI WALIONESHA UHITAJI MKUBWA HASA KATIKA MASUALA YA KUWAWEZESHA KIELIMU





Tuesday, January 1, 2013

SALAMU ZA MWAKA MPYA KUTOKA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

KARIBUNI MGANDU



Na Francis Uhadi

Ndugu wapendwa Taasisi yetu ya Ulanga Community Resource Centre inawatakia mafanikio mema katika mwaka huu mpya wa 2013.


Kwa upande wetu tumefurahi kwa kuwa tumeweza kusajili Taasisi hii ambayo tunadhamilia kuifungua rasmi mwaka huu. Kama tukiwa wakweli tukilinganisha nyumbani kwetu Ulanga, Kilombero na Morogoro kwa jumla watu wetu ni maskini sana ingawa wana rasilimali nyingi zinazowazunguka. 


Kadhalika, tofauti na maeneo mengine kama vile Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza na hivi karibuni Mkoa wa Pwani, Lindi, Mtwara nk imekuwa na amsha amsha sana ya asasi za kiraia na kutokana na kazi hizo elimu na uelewa wa watu umeongezeka sana ikiwa ni pamoja na kuwachagua watu wenye uwezo na kuwawajibisha pale inapobidi.


Masika inaingia sasa, yale magari yanayotusaidia kama Morobest na AlySaedy karibu yataishia Ifakara. Kwetu sisi kama Ulanga Community Resource Centre tunaamini kuwa wananchi wanapoelimishwa juu ya haki zao na kuwa na taarifa sahihi ndipo wanapoweza kuzidai haki hizo na huu ndio hasa msingi wa kuanzishwa kwa Ulanga Community Resource Centre.


Daraja la mto Kilombero hadi leo kazi bado haijaanza ingawa kumekuwa na taarifa kuwa mkataba ulikwisha sainiwa. Ni nani anapaswa kulifuatilia hilo na kuhakikisha linatekelezwa?


Vunguvugu hili linatakiwa lianzie kwa vijana, tunafikiri mijadala yetu kwa mwaka huu 2013  ijielekeze kwenye mustakabali wa jamii inayoteseka kwa kukosa maendeleo kule nyumbani.  Hata hivyo hatuta weza kufikia lengo hilo kama si kwa kushirikiana, mwaka huu 2013 uwe ni mwaka wa kushirikiana zaidi na kukosoana inapobidi.


Tusiishie kufanya mijadala ya Facebook bila utekelezaji kwa vitendo hasa kwa kule nyumbani Ulanga/Kilombero.  Mwisho tunawatakia mwaka mpya wenye Mafanikio tele.