HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Wednesday, February 20, 2013

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 BAADHI YA SHULE KATIKA WILAYA YA ULANGA

Ndugu wapendwa, tunafahamu kuwa kwa matokeo ya Form 4 ya mwaka 2012 kuwa takriban asilimia 60 ya watahiniwa wamepata SIFURI. Katika hali hiyo kwa mazingira ya Ulanga ni mbaya zaidi. Tumejaribu kuweka links za baadhi ya shule hapo chini jioneeni wenyewe. 


BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA 

Pamoja na ubaya wa matokeo hayo, tunawapongeza baadhi ya vijana walioweza kupata angalau daraja la tatu pamoja na wale waliopata la nne wenye points zinazowawezesha hata kwenda ualimu. Kwa wengine ndo hivyo mambo yamekuwa magumu. Lakini tunapenda pia kuwa wakweli hapa, pamoja na miundo mbinu isiyoridhisha ya shule na kadahlika, wapo baadhi ya wanafunzi wa shule hizi hawakupenda kutumia nafasi yao vizuri ikiwa ni pamoja na walimu waliopo katika shule hizo. Mfano, wapo walimu au vijana ambao wapo vyuoni huwa wanajitolea kufundisha ama bure au kwa kuchangia kidogo sana, lakini mwitikio wa wanafunzi umekuwa duni sana. Mara nyigngi tumetembelea baadhi ya shule kama vile pale Mtimbira na kuongea na wanafunzi, bado mwamko wa kutumia muda wao kuhusu masuala ya shule ni mdogo sana. Itakumbukwa kuwa miaka ya 80 na 90 na miaka ya awali ya 2000 mambo ya masomo ya ziada ilikuwa ni ngumu sana kuyapata lakini sasa wapo vijana wengi waliohitimu elimu ya juu wanatoka maeneo tunayozungumza. Tunawaomba tufanye kazi ya ziada kuokoa jahazi hili linalozama. 

suala lingine linaloharibu maendeleo ya wanafunzi katika wilaya za ulanga na kilombero ni NGONO. Tunaomba tu tuwe wawazi hapa. Kuna hawa jamaa wanao nunua Mpunga na sasa vijana wa Boda Boda wanawamaliza wasichana katika Wilaya hizi. Lakini poa kuna watu wa mitaani na miongoni mwa wanafunzi wenyewe suala la ngono limekuwa likiendelea kwa kasi sana. Katika  hali kama hiyo kufeli kutaendelea. 

Mwisho kumeingia suala la USHAROBARO hasa wilaya ya Ulanga. Ni kituko, vijana wengi wa kiume wanatumia mda mwingi katika UNNECESSARY businesses kuliko kusoma. Hatutaweza kubadili hali hii ya kushindwa katika mitihani kama hatutakuwa na mabadiliko toka ndani. 

USHAURI WANGU

Kuna mambo mengi tunaweza kufanya lakini naomba ni yaache yote na nilizungumzie moja la wanafunzi wa elimu ya juu kufundisha katika shule mbalimbali Ulanga na Kilombero. Natoa mapendekezo kuwa tuandae orodha ya wanafunzi wote wanaotoka katika wilaya za Ulanga na Kilombero waliopo katika vyuo vikuu na colleges ikiwa ni pamoja na taaluma zao. Sisi tulio makazini tuanzishe MFUKO WA ELIMU ambao utawawezesha hao wanafunzi kwenda kufundisha wakati wa likizo na tukawapatia angalau nauli. Pia kwa wale wanaosoma ualimu wahamasishwe kuomba FIELD ATTACHMENT katika shule za Ulanga na Kilombero ili kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya hizo.

Hayo ni mawazo yangu, wewe una mawazo gani???? funguka sasa

Jionee matokeo ya Baadhi ya Shule




SOFI SECONDARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s4229.htm


http://www.necta.go.tz/matokeo2012/csee2012/data/s2469.htm



CLICK TO SEE THE RESULTS