HABARI KAMILI HII HAPA.
JESHI la polisi Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro
limelazimika kurudisha jumla ya sh 10 milioni zinazodaiwa kuporwa kwa mfugaji
wa jamii ya kisukuma baada ya kumuuwa kwa kupigwa risasi mdogoni hatua hiyo
ilikuja baada ya kususiwa maiti hiyo kwa siku mbili.
Hatua ya utekelezaji wa urudishaji wa pesa hizo
zilizokuwa zikilalamikiwa na ndugu wa mfugaji huyo aliyefahamika kwa jina la
Baya Katambi Kidiga ni sehemu ya makubaliano yaliofikiwa mbelee ya Mkuu wa
Wilaya ya Ulanga Francis Mitti na Mkuu wa jeshi la polisi Mkoani hapa Faustine
Shilogile, Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai mkoani hapa Hamisi Selemani, Mkuu
wa polisi Ulanga.
Sakata hilo la mauaji na uporaji linaloendelea
kulichafua jeshi la polisi Mkoani Morogoro limetokea tarehe 26, January 2013
katika Kitongoji cha Lugangeni Kijiji cha Ipera Asilia Tarafa ya Mtimbira
wilaya ya Ulanga Mkoani hapa.
Awali polisi hao walidaiwa kutekeleza mauaji hayo
majira ya saa 4 kwa kumpiga risasi marahemu huyo na kuuchukua mwili wake na
kuupeleka kituo cha afya Mtimbira haraka haraka kwa kutumia gari la polisi
linalodaiwa likishiriki katika operationi ya kukamata mifugi wilayani humo
kutoka kwenye hifadhi ya bonde la mto Kilombero.
Baadhi ya masharti ambayo polisi walitakiwa
kutekeleza ni kutoa ripoti ya kina ya uchunguzi wa kifo kutoka kwa daktari
ambao utabainisha kuwa marehemu Baya Kidinga (20) amefariki dunia kwa kupigwa
kwa risasi.
Hatua ambayo jeshi hilo lilitekeleza kwa kutoa
ripoti daktari alitoa riporti ya mauaji hayo yaliodhibitisha bila shaka kuwa
ameuwawa kwa kupigwa risasi ambayo ilikubaliwa.
Sharti la pili ambalo polisi walitakiwa kutekeleza
ni kujua ni kwanini mwili wa marehemu ulihamishwa toka katika eneo la tukio kwa
haraka bila hata kutoa fursa ya ndugu zake kuwepo na baadhi ya ndugu na
majirani waliokuwa waliotaka kufuatilia juu ya mkasa huo walizuiwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile alikuwa wa kwanza kuonja makali ya wananchi ambapo aliwasili majira
saa saa 5 asubuhi siku ya tukio na jopo la maafisa wa jeshi hili huku idadi ya
wafugaji wakiendelea kukusanyika kwa kuulizwa maswali yaliomshinda ikiwemo
kutakiwa kueleza kama operationi ya kuwaondoa wafugaji katika hifadhi ya bonde
la mto Kilombero ipo au imekwisha na eneo ambalo marehemu ameuwawa ndani ya
hifadhi ama laa.
Shilogile akijibu maswali hayo alisema kuwa
operationi anachojua yeye ilisitishwa katika wilaya ya Kilombero lakini kwa
wilaya ya Ulanga hilo hatakuwa na jibu la swali hilo lakini swahili litajibiwa
na mkuu wa wilaya ya Ulanga pindi atapofika.
“Poleni kwa msiba huu mimi nimekuja na timu ya
wenzangu akiwemo mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wetu lakini
natumaini kila kitu kitaenda sawa na kingine mimi nimekuja eneo la tukio kutaka
kujua ukweli wa tukio hili ili kubaini ukweli wenyewe ikiwemo nani amefanya
kosa na mpaka sasa askari wetu waliohusika katika tukio hilo tayari
tunawashikilia kwa ajili ya uchunguzi wa awali na wakibaini sheria itachukua
mkondo wake” alisema Shilogile.
Kamanda huyo ambaye alikabiliwa na maswali mengi
kutoka kwa wafugaji hao likimwemo la msemaji wa familia hiyo ya marehemu, Baya
Kidinga (20), (Madaha Shirinde) aliyeuliza kwa kutaka ufafanuzi wa kina kwa
kuuliza swali je askari aliyepata mafunzo anapaswa kufanya nini pindi
anapokabiliana na mtu mwenye silaha za asili ikiwemo fimbo ? ama kutuliza
ghasia au vurugu anapaswa kutumia bunduki kwa kupiga mwananchi katika eneo gani
?.
Akijibu maswali hayo Kamanda wa polisi Morogoro,
Shilogile alijibu kuwa anapaswa kumpiga mtu risasi kwa kutumia bunduki kwenye
miguu na kueleza kuwa yeye amefika eneo hilo na timu yake kwa lengo la kujua
mazingira ya tukio lililivyofanywa na askari baada ya kufanya uchunguzi na
kuwahoji walioshuhudia.
Majibu hayo ya kamanda yalizusha mzogo mkali
kutoka kwa wananchi hao na kuzalisha maswali mengine likimo la kuhoji kwanini
askari wako ametumia silaha kwa kumpiga marehemu risasi mdogoni kama amepata
mafunzo ?.
Kamanda huyo alieleza tena kwa umati wa wafugaji
hao kwa kusema kuwa kwa wakati huo atakuwa na jibu la swali hilo na kuongeza
hawezi kujua kilichompata askari huyo mpaka ametumia silaha kwa kumpiga risasi
marehemu jambo hilo tutalifanyia kazi baada ya kukabilika kwa uchunguzi
wao.
Maswali hayo hayakuweza kuwaridhisha umati wa
wananchi na upande wa familia ya marehemu na kumtaka kamanda huyo awasiliane na
mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti kwa kuhoji kwa nini wewe Kamanda
umetembea umabli mrefu kufika eneo la tukio na mkuu wako wa wilaya ambaye yupo
jirani ameshindwa kufika eneo la tukio ?.
Mzozo huo ulidumu kwa muda wa masaa mawili bila
kufikia muafaka katika siku ya pili baada ya tukio kutokea ambayo kamanda wa
polisi alishindwa kutimiza malengo yake, likiwemo kuwashawishi ndugu wa
marehemu wakubali kuutambua mwili wa marehemu, kupokea uchunguzi wa daktari na
kuchukua mwili wa marehemu jambo ambalo alilazimika kuwasiliana na mkuu wa
wilaya ili kufika eneo la tukio.
DC ULANGA.
Mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti aliwasili
katika eneo la tukio la mjira ya saa 10:30 alasiri na kuanza kuwapa pole umati
uliokuwa ukimsubiri ili kutatua kero za wananchi hao.
Miti baada ya kutoa pole kwa wafiwa alianza kutoa
ufafanuzi juu ya zana iliyojengeka kwa wananchi hao kuwa marehemu amepigwa
risasi katika zoezi la operesheni na kuwa askari hao hawakuwa katika operesheni
bali walikuwa katika zoezi la udhibiti na ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la
hifadhi mto wa Kilombero na kuwa wanaobainika hukamatwa na kutozwa faini kisha
kuwapa ovyo waliende tena katika bonde la mto Kilombero.
“tukio hili hakuna anayefurahia hata kidogo
niwaeleze kuwa operesheni haipo kilichopo sasa ni udhibiti na ufuatiliaji wa
mifugo katika bonde la hifadhi mto wa Kilombero na operesheni tayari ilishaisha
tangu januari mosi mwaka huu” alisema Miti.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya naye alikumbana na
maswali juu ya watendaji wake waliokuwa katika operesheni na udhibiti na
ufuatiliaji wa mifugo katika bonde la hifadhi mto Kilombero na kuwa daktari wa
mifugo wilaya Ulanga, Fredrick Sagamiko amekuwa akidaiwa kukiuka utaratibu wa
faini.
Mselengeti Mipawa (41) alimweleza mkuu wa wilaya
katika tukio hilo kuwa daktari huyo amekuwa akitoza faini kati ya sh60,000 hadi
100,000 pindi anapokamata mifugo badala ya faini iliyoidhinishwa na serikali ya
kiasi cha sh44,000 kwa ng’ombe mmoja jambo ambali wamekuwa wakilipia na
kuwarudisha nyumba katika harakati za maendeleo.
Mipawa alimweleza mkuu huyo wa wilaya kuwa daktari
huyo wa mifugo wilaya ya Ulanga, licha ya kukiuka utozaji wa faini pia amekuwa
akimakata na mifugo ambayo haiku kwenye listi ya ukamataji wa operesheni hiyo
wakiwemo kukamata mifugo wakiwemo kondoo, mbuzi na punda na kutozwa faini kubwa
kuanzia kiasi cha sh 700,000 na kuendelea kulinagana na uwingi wa mifugo hiyo.
Miti alisema kuwa baada ya kupata tuhuma zinazo
mwelekeza daktari wa mifugo wilaya Ulanga, Fredrick Sagamiko yeye atawasilisha
tuhuma hizo kwa mwajili wake ambaye ni mkurugezi wa halmashauri ya wilaya ya
Ulanga ili uchunguzi ufanyike na kama itabainika sheria itafuata mkondo wake.
Aliwaeleza umati huyo kwa kuwataka wafugaji waache
tabia ya kuwashambulia askari na kuwataka askari nayo kutotumia nguvu kubwa
wakati wa vurugu pindi inapotokea hiyo itasaidia kuendeleza ushirikiano mzuri
baina ya jeshi la polisi na wananchi.
Mkuu huyo alilazimika kuwashawishi ndugu wa
marehemu wakubaliane na ombi lao la kutaka wakatambue mwili wa marehemu na
kupokea uchunguzi wa daktari kisha kuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya
mazishi jambo ambalo lilishindikana kukubali ombi hilo kutokana na kutotimiza
madai yao.
Baada ya Kamanda wa polisi na mkuu wa wilaya
Ulanga kushindwa kuwashawishi ndugu wa marehemu kuchukua mwili wa ndugu yao
msafara wao uliondoka eneo hilo majira ya saa 12:30 jioni na siku ya pili ya
januari 28 mwaka huu ikifuatiwa na kutokubaliana hadi gazeti hili liondoka
katika eneo la tukio.
Awali Baba wa marehemu Katambi Jidiga alisema kuwa
marehemu alitokea mkoani Songea kuuza baadhi ya ng’ombe kwa ajili kulipa madeni
ya mifugo iliyokamatwa katika operationi, awali imetajwa mbuzi 100 alilipa
lakini saba, ngombe inadaiwa akikuwa akidaiwa 10 milioni na mara ya tatu ngombe
wake waliokamatwa na askari hao alikuwa akidaiwa sh milioni 3.