Na Senior Libonge,Ulanga
Serikali inakusudia kuanza ujenzi wa daraja la mto Kilombero ambalo linaunganisha wilaya za Kilombero na Ulanga katika Mkoa wa Morogoro katika kipindi cha mwaka huu wa fedha wa 2012/2013
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejiment ya utumishi wa Umma Celina Kombani, alitangaza kuanza kwa ujenzi huo wakati akizungumza na wananchi wa kata za Ketaketa,Mwaya,Ilonga na Ruaha zilizopo katika jimbo la Ulanga mashariki mkoani Morogoro.
Alisema kuwa tayari Serikali imeshapata fedha za kuanza ujenzi huo kinachofanyika hivi sasa ni kumpata mkandarasi ambaye atakamilisha ujenzi wake unatarajia kuanza katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha .
Waziri huyo alisema kuwa tayari Serikali ilishafanya upembuzi yakinifu katika mto kilombero kwa kutumia kampuni moja kutoka nchini Kenya ambayo ilitumia zaidi ya shilingi bilioni moja katika kazi hiyo.
Kutokana na hali hiyo Waziri Kombani aliwataka wakulima kuanza kuzalisha mazao kwa tija na kuweza kuyaweka sokoni ili kukabiliana na ushindani kipindi daraja hilo litakapokamilika.
Katika hatua nyingine huo huo Waziri Kombani amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuacha kuuza chakula walichokipata katika msimu wa kilimo uliopita ili kiweze kuwasaidia katika kipindi cha msimu wa masika ambao mara kadhaa wamekuwa wakikabiliwa na upungufu wa chakula.
Alisema katika kipindi hiki ni vema wananchi wakaelewa kuwa ni kipindi cha kujiwekea akiba ya chakula ili ije iwasaidie katika kipindi cha masika
Ni hatua nzuri. Binafsi naona italeta mianya ya maendeleo kwa wilaya yetu. Kwa maana rahisi itapanua wigo wa biashara kwa wilaya za ulanga na kilombero...
ReplyDelete