Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Tume ya kukusanya maoni kwa ajili ya mchakato wa Kupata Katiba Mpya leo inaendelea na Ziara yake katika Wilaya ya Kilombero na Asubuhi hii wapo Sanje katika ofisi ya kijiji Msolwa Ujamaa ambapo watakusanya maoni kwa wananchi wa kata hiyo.
Baadaye Saa nane mchana wataelekea Kidatu na watakuwa Mkamba Sokoni ambapo watakusanya Maoni kabla ya kukabidhiwa katika Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kuendelea kukusanya Maoni.
Tume hiyo iliingia Wilayani Kilombero ikitokea Wilaya ya Ulanga Tarehe 31 Agosti na kuanza kukusanya Maoni Ifakara Mjini Septemba Mosi asubuhi, mchana walielekea Mbingu, Septemba 2 walikuwa Chita asubuhi na Mchana walikuwa Mlimba kabla ya Septemba 3 kuwa Kiberege asb na mchana kuwa Mang'ula.
No comments:
Post a Comment