Henry Bernard Mwakifuna, Chita, Kilombero
Mabanda Sita yenye Mali zenye Thamani ya Shilingi Milioni 2 na Elfu 95 yameteketea katika ajali ya moto uliotokea Katika Kijiji cha Merera kilichopo Kata ya Chita Wilayani Kilombero.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Merera Bwana Odwin Mafulu amesema kuwa mabanda ya Migahawa, mabanda ya kuoneshea Video Magenge, kushonea nguo na yakuuzia vitu mbalimbali yameteketea kwa moto ulioanza saa Sita mchana.
Chanzo cha Ajali hiyo ya Moto hakijafahamika ambapo Afisa Mtendaji amesema kuwa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji hicho inaelendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Mbali ya hapo amesema kuwa kumekuwepo na Taarifa za awali ambazo hazina uhakika juu ya chanzo cha moto huo kuwa ni Mtoto Mdogo kuchezea Kiberiti katika banda moja na kusababisha mabanda mengine kuungua.
No comments:
Post a Comment