Henry Bernard Mwakifuna, Chita Kilombero
Jumla ya Shilingi Bilioni Moja Nukta sita zitatumika kwa ajili ya Utekelezaji wa programu ya mabadiliko ya tabia nchi katika Vijiji Sita vya Wilaya ya kilombero.
Katibu Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na uhifadhi wa Mazingira na Maendeleo katika Bonde la Mto Kilombero(KIVEDO) Hamza Kaposa amesema mradi huo unafanyika kwa ushirikiano wa Plan International chini ya ufadhili toka Serikali ya Ujerumani na utaendeshwa kwa muda wa miaka Minne.
Amesema Vijiji Sita vya Wilaya ya Kilombero vimeteuliwa kufuatia utafiti uliofanyika kutokana na kuharibika na mabadiliko ya Tabia nchi.
Amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Udagaji kilichopo Kata ya Chita, Mkangawalo Kata ya Mchombe, Mbingu Kata ya Mbingu, Kisegese na Namwawala Kata ya Idete na Mofu Kata ya Mofu.
Katika mradi huo KIVEDO wakishirikiana na Wananchi wa Vijiji Sita watajishughulisha katika Upandaji Miti,Hifadhi ya Mazingira na Maliasili na kuboresha upatikanaji wa Mazao na masoko yake.
Tayari KIVEDO wameshakabidhi Vifaa mbalimbali vitakavyotumika katika maandalizi ya kazi ya kuandaa Vitalu vya miti vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni Sita na Elfu Hamsini na nne.
Wakati huo huo Uharibifu mkubwa wa Mazingira unafanyika katika pori la Fusi Sangamani katika Safu ya Milima ya Udzungwa kijiji cha Makutano kata ya Chita.
Gasper Mkude, Mwenyekiti wa kitongoji cha Makutano,Chita amesema kuwa kutokuwapo kwa kamati ya usimamizi wa mazingira Kijijini hapo kunasababisha uharibifu wa Mazingira kuwa Mkubwa katika masitu huo.
Amesema kila Serikali ya kijiji inapopeleka majina ya Wananchi kwa ajili ya kupitishwa kuwa Wanakamati ya Mazingira wananchi wamekuwa wakiikataa Kamati inayoteuliwa, na hivyo kupelekea misitu kuteketea kwa hakuna ulinzi mathubuti katika msitu huo.
Uharibifu huo ni pamoja na Uvunaji wa Mbao na Uchomaji moto wa Misitu
No comments:
Post a Comment