Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
JUMLA ya Watu 120 wanataraji kupata Mafunzo ya Haki Elimu kwa Watoto Yatima na Wale Wanaoishi katika Mazingira Magumu katika Eneo la Kibaoni, Makero na Michenga Wilayani Kilombero.
Evenita Chamanga, Katibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women and Children Group amesema kuwa watakaopata Mafunzo hayo ni Wananchi na Viongozi wa Serikali kutoka katika maeneo hayo.
Amesema kuwa wameamua kufanya Mafunzo kwa maeneo ya Kibaoni, Makero na Michenga kwa kuwa asilimia 10 tu ya Watoto wanaoishi katika mazingira magumu ndiyo wamepata Elimu katika maeneo hayo.
Wakati huo huo Taasisi hiyo ya Women and Children Group Tarehe 24 Septemba 2012 itaanza mafunzo ya kuhusu haki elimu kwa Watoto Yatima na Wanaoishi katika Mazingira Magumu.
Mafunzo hayo yanataraji kufanyika katika Ukumbi wa Mazingira Kibaoni Ifakara Mjini na yamefadhiliwa na Foundation for Civil Society.
No comments:
Post a Comment