Na Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara
Tamasha la ngoma za Utamaduni kwa Makabila yaliyopo bonde la mto Kilombero limefanyika jumapili ya Kwanza ya Septemba na limeandaliwa na TUDECO(TUMAINI dEVELOPMENT and Counseling Trust) ambao ni wameliki wa kituo cha Redio cha Pambazuko.
Ngoma kutoka makabila ya Wilaya ya bUlanga na Kilombero zilikutana katika Ukumbi wa Makutano Club uliopo Ifakara Mjini ambayo ni makao Makuu ya Wilayanya Kilombero.
Tamasha hilo ni la Awamu litakuwa likifanyika kila siku ya nJumapili na Mwisho wa Mwezi mshindi atapata Laki 4 fedha Taslimu, wa Pili Kali 3 Unusu na Mshindi wa Tatu Laki 3.
Akifungua Tamasha la Kwanza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero Ramadhani Kiombile ameipongeza TUDECO kwa kubuni tamasha ambalo linakutanisha makabila ya Bonde la Kilombero.
No comments:
Post a Comment