BAADHI YA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI MTIMBIRA |
Pamoja na ubaya wa matokeo hayo, tunawapongeza baadhi ya vijana walioweza kupata angalau daraja la tatu pamoja na wale waliopata la nne wenye points zinazowawezesha hata kwenda ualimu. Kwa wengine ndo hivyo mambo yamekuwa magumu. Lakini tunapenda pia kuwa wakweli hapa, pamoja na miundo mbinu isiyoridhisha ya shule na kadahlika, wapo baadhi ya wanafunzi wa shule hizi hawakupenda kutumia nafasi yao vizuri ikiwa ni pamoja na walimu waliopo katika shule hizo. Mfano, wapo walimu au vijana ambao wapo vyuoni huwa wanajitolea kufundisha ama bure au kwa kuchangia kidogo sana, lakini mwitikio wa wanafunzi umekuwa duni sana. Mara nyigngi tumetembelea baadhi ya shule kama vile pale Mtimbira na kuongea na wanafunzi, bado mwamko wa kutumia muda wao kuhusu masuala ya shule ni mdogo sana. Itakumbukwa kuwa miaka ya 80 na 90 na miaka ya awali ya 2000 mambo ya masomo ya ziada ilikuwa ni ngumu sana kuyapata lakini sasa wapo vijana wengi waliohitimu elimu ya juu wanatoka maeneo tunayozungumza. Tunawaomba tufanye kazi ya ziada kuokoa jahazi hili linalozama.
suala lingine linaloharibu maendeleo ya wanafunzi katika wilaya za ulanga na kilombero ni NGONO. Tunaomba tu tuwe wawazi hapa. Kuna hawa jamaa wanao nunua Mpunga na sasa vijana wa Boda Boda wanawamaliza wasichana katika Wilaya hizi. Lakini poa kuna watu wa mitaani na miongoni mwa wanafunzi wenyewe suala la ngono limekuwa likiendelea kwa kasi sana. Katika hali kama hiyo kufeli kutaendelea.
Mwisho kumeingia suala la USHAROBARO hasa wilaya ya Ulanga. Ni kituko, vijana wengi wa kiume wanatumia mda mwingi katika UNNECESSARY businesses kuliko kusoma. Hatutaweza kubadili hali hii ya kushindwa katika mitihani kama hatutakuwa na mabadiliko toka ndani.
USHAURI WANGU
Kuna mambo mengi tunaweza kufanya lakini naomba ni yaache yote na nilizungumzie moja la wanafunzi wa elimu ya juu kufundisha katika shule mbalimbali Ulanga na Kilombero. Natoa mapendekezo kuwa tuandae orodha ya wanafunzi wote wanaotoka katika wilaya za Ulanga na Kilombero waliopo katika vyuo vikuu na colleges ikiwa ni pamoja na taaluma zao. Sisi tulio makazini tuanzishe MFUKO WA ELIMU ambao utawawezesha hao wanafunzi kwenda kufundisha wakati wa likizo na tukawapatia angalau nauli. Pia kwa wale wanaosoma ualimu wahamasishwe kuomba FIELD ATTACHMENT katika shule za Ulanga na Kilombero ili kuinua kiwango cha elimu katika Wilaya hizo.
Hayo ni mawazo yangu, wewe una mawazo gani???? funguka sasa
Jionee matokeo ya Baadhi ya Shule
St. May’s
Mang’ula http://196.44.162.25/necta2012/data/s3823.htm
MTIMBIRA SECONDARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s1575.htm
MKULA SECONDARY http://www.ajira.go.tz/matokeo2012/csee2012/data/s1238.htm
ITETE SECONDARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s2473.htm
NAWENGE SECONDARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s1535.htm
SOFI SECONDARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s4229.htm
http://www.necta.go.tz/matokeo2012/csee2012/data/s2469.htm
KASITA SEMINARY http://www.jamiiforums.com/matokeo2012/data/s0117.htm
CLICK TO SEE THE RESULTS
No comments:
Post a Comment