Henry Bernard Mwakifuna, Mlimba-Kilombero
Madiwani, Watendaji wa Halmashauri, Watendaji wa Vijiji na Kata na Wataalamu katika Wilaya ya Kilombero wamehimizwa kusimamia Miradi inayohudumia Wananchi kutengenezwa kwa kukidhi Viwango.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Joel Nkaya Bendera amesema kuwa thamani ya fedha zinazotolewa na Serikali ilingane na Miradi husika.
Amesema kumekuwa na ubadhirifu wa fedha katika miradi ya kijamii ambapo thamani halisi ya fedha hailingani na Miradi husika.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amewahimiza Wananchi kushiriki ipasavyo katika shughuli za maendeleo na hususani ujenzi wa Madarasa.
Amesema kwa Mwaka huu Mkoa wa Morogoro unahitaji Madarasa 288 kwa ajili ya kadirio la Wanafunzi 33,000 wanaotaraji kufaulu, kwa Wilaya ya Kilombero Jumla ya vyumba vya Madarasa 27 vinahitajika kwa ajili ya wanafunzi watakaofaulu kwa mwaka huu.
Mheshimiwa Bendera alikuwa akiongea na Wananchi wa Kata ya Mlimba katika Ziara yake Wilayani Kilombero, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi Mlimba
No comments:
Post a Comment