Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [TAKUKURU] Wilayani Kilombero imepokea jumla ya malalamiko 35 kutoka sehemu mbalimbali za Wilaya hiyo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Agosti mwaka huu ambayo hadi sasa yanaendelea kufanyiwa kazi katika hatua mbalimbali za kiuchunguzi.
Taarifa iliyotolewa kwa Waandishi wa Habari na Afisa wa Takukuru Bw.Festo Mdede imeeleza kuwa hadi sasa kuna kesi tano [5]za kukamatwa na Rushwa ambazo bado zinaendelea kusikilizwa Mahakamani.
Mbali ya Kesi hizo Afisa huyo amesema kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [w]Kilombero inatarajia kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea ujasiri wa kutoa ushirikiano katika suala la kuzuia na kupambana na Rushwa ndani ya Wilaya hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa mbali na kutoa elimu kwa wananchi taasisi imejiwekea mikakati ya kufanya Warsha fupi ili kupokea mawazo na ushauri kutoka kwa wananchi kwa lengo la kujenga ushirikiano utakao- saidia kurahisisha kazi ya kuzuia na kupambana na Rushwa .
Ametoa Wito kwa Wafanyakazi wa nyanja mbalimbali kufuata sheria za kazi na kutoruhusu kutoa wala kupokea Rushwa bali ni kupambana kikamilifu kuzuia Rushwa ili wawe mfano mzuri na wa kuigwa katika jamii.
No comments:
Post a Comment