Na Senior Libonge, Mahenge
WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe ameahadi kutoa kiasi cha shilingi milioni 42 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji katika Mji wa Mahenge uliopo katika tarafa ya vigoi wilayani ulanga mkoani Morogoro.
Mji wa Mahenge unakabiliwa na uhaba wa maji kutokana na kutokana na miundombinu yake kuchakaa ulihaidiwa kumalizika kwa tatizo hilo na Rais Jakaya Kikwete alipotembelea wakati wa ziara yake mapema mwaka 2009.
Katika kutatua tatizo hilo la maji,Rais Kikwete alitoa kiasi cha shilingi milioni 200 ili kujengwa kwa miundombinu ya maji ambapo ilibainika ili kukamilisha mradi huo kulikuwa kunahitajika kiasi hicho cha fedha.
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya ya Ulanga, iliyosomwa na kaimu mkuu wa wilaya hiyo Prisca Shewali,Mbunge wa jimbo hilo la Ulanga Mashariki Celina Kombani alisema kuwa wizara ya maji imeahidi kulimaliza tatizo la maji kwa kuleta fedha za kumalizia mradi wa ujenzi
Alisema pamoja na mradi huo kuongezeka gharama lakini waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe amuahidi kuwa mara fedha zitakapoingia wizarani kwake kipaumbele kitakuwa ni katika mji wa mahenge.
Kombani ambaye pia ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejamenti ya Utumishi wa Umma,alisema kuwa kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha kukamilisha kabisa mradi huo mkubwa wa maji na hivyo kumaliza kabisa tatizo hilo la ukosefu wa maji.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa miundombinu ya maji ambayo inaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali ya tarafa ya vigoi mhandisi wa maji wilaya ya ulanga Patrice Jerome, alisema mpaka sasa wameshafikia katika hatua ya usambazaji wa mabomba ambayo yamekamilika katika maeneo mbalimbali.
Mradi huo wa maji uliahidiwa na Jakaya Kikwete wakati wa ziara zake alizofanya wilayani Ulanga ambapo awali mradi huo ulikuwa ulikuwa na gharama ya shilingi milion 200 ambapo kwa sasa inadaiwa kupanda na kufikia shilingi milioni 300.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment