Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Wananchi waliovamia eneo la Hifadhi katika vijiji vya Mofu,Ihenga,Ikwambi Wilayani Kilombero wametakiwa kuhama katika maeneo hayo na kusitisha kufanya shughuli zozote za kiuchumi.
Abdul Mteketa, Mbunge wa Jimbo la Kilombero (CCM) amesema kuwa wale wote waliovamia eneo hilo waliache na kuendelea kubaki eneo hilo ni kusababisha Uharibifu mkubwa wa mazingira na kukaidi agizo la serikali lililotaka wakazi wote waliopo eneo la hifadhi kuondoka ifikapo Septemba 7 mwaka huu.
Bwana Mteketa alikuwa akiongea na Wananchi wa kata ya Mofu katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mofu Kata ya Mofu akiwa na lengo la kuwashukuru Wananchi kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilombero.
Katika Ziara hiyo Mheshimiwa Mteketa ametoa Vitabu 80 vya masomo ya Sayansi katika Shule ya Sekondari ya Mofu na vifaa vya Michezo Jezi pamoja na Mipira Mitatu katika Vijiji vya Mofu na Idete.
No comments:
Post a Comment