Shule ya Sekondari Ifakara (Machipi), ikionekana kwa mbali |
Na Henry Bernard Mwakifuna, IFAKARA
Bwana Ally Mahachi, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Machipi Kata ya Michenga Wilayani Kilombero anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani humo kwa tuhuma ya wizi wa fedha za Wananchi Shilingi Milioni Saba na Elfu Arobaini(7,040,000).
Mtendaji huyo anashikiliwa na jeshi hilo tangu sept 4mwaka huu baada ya wananchi kuunda tume ya uchunguzi wa fedha za miradi iliyopo na inayotarajiwa kuanza na kugundua baadhi ya miradi mtendaji amewadanganya Wajumbe fedha zilizolipwa.
Baadhi ya wajumbe wa Serikali ya kijiji hicho wameeleza kuwa kuna Fedha zilitolewa na Mfuko wa Jimbo la Kilombero kwa ajili ya Uchimbaji wa Visima vya Maji na uuzwaji wa eneo la ujenzi wa Mnara tangu mwaka 2011, hata hivyo hadi sasa fedha hizo hazijulikani zilipo.
Njia ya kuelekea Mnarani |
Wajumbe hao wamesema kuwa Bwana Mhachi alifanya udanganyifu alipokuwa anatoa taarifa katika kijiji hicho cha Machipi kuwa amepokea shilingi laki saba(700,000) kwa ajili ya eneo la mnara hali ambayo siyo kweli. Uchunguzi wa Tume hiyo umegundua kuwa fedha zilizolipwa ni shilingi milioni 5,290,000/=na fedha zilizotolewa na mfuko wa jimbo ni shilingi milioni 1,750,000/= Jeshi la Polisi limethibitisha kukamatwa kwa Mtendaji huyo Bwana Mahachi akituhumiwa kula fedha za wananchi na upelelezi utakapo kamilika atafakishwa Mahakamani
Sehemu iliyouzwa kwa ajili ya ujenzi wa Mnara |
No comments:
Post a Comment