Henry Bernard Mwakifuna- Ifakara
Serikali Wilaya ya Kilombero imesema itafanya Utaratibu wa Kupitia Mikataba yote ya Wawekezaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amesema suala la msingi ni kujiridhisha na aina ya Mikataba iliyofanywa, kulinda Rasilimali zetu na Kusaidia kuepusha Migogoro kati ya Wawekezaji na Wanachi.
Amesema Mikataba iliyosawa na iliyoridhiwa itaendelea kuwa kama ilivyokubaliwa lakini ile ambayo ina mashaka taratibu zikifuatwa yaweza kusitishwa.
Bwana Masala ameyasema hayo alipokuwa akiongea na Wananchi wa Mwaya Mang’ula katika mkutano wa hadhara ambapo amesema Wananchi wanapaswa kunufaika katika ajira zinazotokana na Wawekezaji waliowekeza katika maeneo yao.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amewapongeza Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji katika Wilaya ya Kilombero kwa kushiriki na Kusimamia vilivyo Zozi la Sensa ya Watu na Makazi.
Amesema ingawa kuna mapungufu ya hapa na pale lakini zoezi la sensa kutokana na usaidi mzuri wa Wenyeviti hao limeenda vizuri ndani ya Wilaya yake.
Baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza ni pamoja na uhaba wa Dodoso na baadhi ya Makarani kupangiwa maeneo makubwa ya kuhesabu watu.
No comments:
Post a Comment