Na Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Abdul Mteketa anatarajia kugawa Vitabu Vya Masomo ya Sayansi na Vifaa vya Michezo vyenye Thamani ya Shilingi Milioni Kumi na nane na Laki nane pindi atakapomaliza Ziara yake Jimboni mwake.
Akiongea na Redio Pambazuko Mheshimiwa Mteketa amesema ameleta vitabu 500 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Kumi na Tano (15,000,000/) Amesema kuwa vitabu hivyo ni vya masomo ya Biolojia, Fizikia, Hisabati na Kemia ambapo tayari ameshaanza kuvigawa katika Shule ya Sekondari ya Mofu.
Kwa upande wa Vifaa vya Michezo ameleta Jezi seti 20 Mipira 20 vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni TATU NA Laki Nane (3,800,000/) na tayari vifaa hivyo vimeanza kugawiwa kwa vilabu mbalimbali vya mpira wa Miguu Wilayani Kilombero.
No comments:
Post a Comment