Na Senior Libonge, Ulanga
Halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, hatimaye
imeanza kulipa madeni iliyokuwa ikidaiwa na hospitali ya Lugala iliyoko katika
tarafa ya Malinyi wilayani humo baada ya kupata fedha zinazotokana na makusanyo
ya ndani ya halmashauri hiyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Furaha
Lilongeri, halmashauri hiyo tayari imeandaa malipo ya zaidi ya Sh40 milioni kwa
ajili ya kuilipa hospitali ya Lugala baada ya hospitali hiyo kutoa huduma ya
bure kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
Alisema kuwa halmashauri yake mwaka jana ilisaini mkataba
na uongozi wa hospitali ya Lugala ili kuweza kutoa huduma bure kwa makundi hayo
huku fedha za kulipia gharama hizo zikipangwa kupatikana na mfuko wa pamoja wa
serikali kuu na mapato ya ndani ya nchi.
Hata hivyo, tathimini iliyofanywa na halmashauri ya wilaya
ya Ulanga katika kipindi cha miaka mitatu ya utekelezaji wa mkataba huo kuanzia
Julai mpaka Septemba 2012, halmashauri hiyo ilikuwa ikidaiwa jumla ya Sh62.1
milioni.
Lilongeri alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu hizo,
ilibainika pia kuwa idadi ya wagonjwa waliokuwa wakitarajiwa kutibiwa katika
hospitali hiyo kupitia mkataba huo iliongezeka mara dufu kiasi cha kutishia
bajeti ya halmashauri hiyo.
Aliongeza kuwa uchanganuzi uliofanywa na halmashauri hiyo
ulionyesha kuwa idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali hiyo huenda
ikaongezeka zaidi na kulifanya deni la halmashauri kupanda na kufikia wastani
wa zaidi ya Sh248 milioni kwa kipindi cha mwaka mmoja wa utekelezaji wa mkataba
huo.
Mwenye kiti huyo alidai kuwa kama jinsi ambavyo
halmashauri ilivyoadhimia na kuuomba uongozi wa halmashauri hiyo kufanya
mazungumzo ya kulekebisha mkataba huo na kuufanya makata huo kuuruhusu wagonjwa
kutibiwa baadhi ya magonjwa hususan watoto wenye umri wa miaka mitano na
akinamama wajawazito na magonjwa mengine kutibiwa katika zahanati za serikali
zilizopo.
“Tumekwisha andaa malipo ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu
ya deni tunalodaiwa na baada ya kuwakabidhi fedha zao tutaomba maongezi yaweze
kufanyika ili kuruhusu mkataba huo kufanyiwa marekebisho.
No comments:
Post a Comment