KARIBUNI MGANDU |
Na Francis Uhadi
Ndugu wapendwa Taasisi yetu ya Ulanga Community
Resource Centre inawatakia mafanikio
mema katika mwaka huu mpya wa 2013.
Kwa upande wetu tumefurahi kwa kuwa
tumeweza kusajili Taasisi hii ambayo tunadhamilia kuifungua rasmi mwaka huu.
Kama tukiwa wakweli tukilinganisha nyumbani kwetu Ulanga, Kilombero na Morogoro
kwa jumla watu wetu ni maskini sana ingawa wana rasilimali nyingi
zinazowazunguka.
Kadhalika, tofauti na maeneo mengine kama
vile Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Mwanza na hivi karibuni Mkoa wa Pwani, Lindi,
Mtwara nk imekuwa na amsha amsha sana ya asasi za kiraia na kutokana na kazi
hizo elimu na uelewa wa watu umeongezeka sana ikiwa ni pamoja na kuwachagua
watu wenye uwezo na kuwawajibisha pale inapobidi.
Masika inaingia sasa, yale magari
yanayotusaidia kama Morobest na AlySaedy karibu yataishia Ifakara. Kwetu sisi
kama Ulanga Community Resource Centre tunaamini kuwa wananchi wanapoelimishwa
juu ya haki zao na kuwa na taarifa sahihi ndipo wanapoweza kuzidai haki hizo na
huu ndio hasa msingi wa kuanzishwa kwa Ulanga Community Resource Centre.
Daraja la mto Kilombero hadi leo kazi bado haijaanza
ingawa kumekuwa na taarifa kuwa mkataba ulikwisha sainiwa. Ni nani anapaswa
kulifuatilia hilo na kuhakikisha linatekelezwa?
Vunguvugu hili linatakiwa lianzie kwa
vijana, tunafikiri mijadala yetu kwa mwaka huu 2013 ijielekeze kwenye
mustakabali wa jamii inayoteseka kwa kukosa maendeleo kule nyumbani. Hata hivyo hatuta weza kufikia lengo hilo kama si
kwa kushirikiana, mwaka huu 2013 uwe ni mwaka wa kushirikiana zaidi na
kukosoana inapobidi.
Tusiishie kufanya mijadala ya Facebook bila utekelezaji
kwa vitendo hasa kwa kule nyumbani Ulanga/Kilombero. Mwisho tunawatakia
mwaka mpya wenye Mafanikio tele.
No comments:
Post a Comment