HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Sunday, September 29, 2013

UCRC yaendesha mafunzo ya Wasaidizi wa Kisheria (Paralegal) Mtimbira

Na Francis Uhadi


UCRC ni Taasisi ya Kiraia iliyoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2012 kama Kampuni isiyo na hisa kwa ajili ya kufanya kazi za kiraia ikiwa na usajili namba 96145 na makao yake makuu Mahenge Mjini.

Pamoja na masuala mengine, UCRC inalenga kujenga uwezo wa katika masuala ya haki za ardhi na haki rasilimali na utatuzi wa migogoro inayotokana na rasilimali hizo. Vile vile UCRC inalenga kuwawezesha wananchi wanaoishi vijijini kupata msaada wa kisheria kupitia usaidizi wa kisheria.  UCRC inaamini kuwa Wananchi wakiwezeshwa kupata taarifa sahihi juu ya masuala mbalimbali wataweza kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali za jamii ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha viongozi wao  na hivyo kuleta maendeleo.

UCRC ikiwa ni Taasisi changa na ikiwa bado katika kipindi cha kutafuta fedha kwa ajili ya kujiendesha, imeandaa mafunzo ya siku 6 kwa Wasaidizi wa Kisheria (Paralegals). Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo vijana ili waweze kutumika katika jamii kama wasaidizi wa kisheria katika masuala mbalimbali yanayoikabili jamii.


SAFU YA UONGOZI WA KITUO CHA USAIDIZI WA KISHERIA MTIMBIRA


M/kiti wa Paralegal Ndg. Cloud Masekesa
Katibu wa Paralegal Bi Maria Mhaville
Mweka Hazina wa Paralegal Bi Jackline Luselo


Awali matangazo yalitolewa makanisani, misikitini, na maeneo mbalimbali kuwataka vijana waliomaliza kidato cha nne na wenye uwezo wa kujieleza na kuchambua masuala mbalimbali wajitokeze. Zoezi la kuwapata vijana hao lilichukua takriban mwezi na siku kadhaa. Vijana zaidi ya 40 walijitokeza hata hivyo wengi walifikiri hii ni kazi ya kulipwa mshahara. Waliposikia kuwa hakina mshahara wengi waliondoka na wengine walichujwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Mhe. Diwani wa Kata ya Mtimbira Ndg. Richard Likalangu akifungua mafunzo ya Wasidizi wa Kisheria yaliyoanza siku ya Jumatatu Tarehe 23 Septemba 2013. Mafunzo hayo yanatarajia kumalizika tarehe 2 Octoba 2013

Kwa kuwa Taasisi haijapata fedha kutoka kwa mfadhili yeyote, shughuli hii imegharimiwa na waanzilishi wa Taasisi hiyo. Jumla ya vijana 8 ambapo Wasichana ni 3 na Wavulana 5 wamepata mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yatchukua muda wa majuma mawili ambapo awali vijana hao walifundishwa dhana nzima ya Usaidizi wa Kisheria na Miiko yake, jinsi ya kuenenda kama msaidizi wa kisheria na maadili katika usaidizi wa Kisheria.

Vijana hao pia walifundishwa Sera na Sheria mbalimbali zikiwemo Sheria za Ardhi za mwaka 1999 na mfumo wa utatuzi wa Migogoro ya Ardhi. Pia katika juma la kwanza wamefundishwa juu ya Haki za Binadamu pamoja na sharia ya makosa ya Jinai.

Katika juma la pili ambalo linaanza kesho tarehe 30 Septemba vijana hao watafundishwa sheria za Miradhi, Watoto na Haki za Wanawake na Watoto

Ni matarajio yetu kuwa mafunzo haya watatoa vijana ambao watatumika katika kutoa ushauri wa Kisheria kwa wanachi  ili kusaidia kutatua migogoro mbalimbali na hivyo kuleta ufanisi kwa kuwafanya wananchi kupata haki zao. 

Katika picha ni Mhe. Diwani wa Kata ya Mtimbira na Vijana wanoandaliwa kupata mafunzo ya Usaidizi wa Kisheria mara baada ya kufungua rasmi mafunzo hyo katika ukumbi wa Mikutano wa Kata ya Mtimbira

Baadhi ya Waidizi wa Kisheria mara baada ya kumaliza mafunzo katika wiki ya kwanza.

Shukrani zetu za dhati kabisa ziwafikie viongozi mbalimbali wa Serikali kwanza pale Mtimbira ambapo kabla ya mafunzo haya mwandaaji alijitahidi kuonana na Mheshimiwa Diwani Ndg Richard Likalangu, Asisa Mtendaji Kata Ndugu Rajab Mgululi, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mtimbira Bi Rehema Salumu na Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Mtimbira kwa lengo la kutambulisha kwao dhana ya Usaidizi wa Kisheria. Pamoja nao Katibu wa Baraza za Kata pia alishiriki katika mafunzo.

Mwitikio ambao umepatikana kwa viongozi hao ni wa kuigwa katika maeneo mengine kwani wote kwa ujumla wao walifurahishwa sana na kuanzishwa kwa Taasisi hii lakini pia kuleta mafunzo ya usaidizi wa kisheria. Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mtimbira alisema kuwa ni matarajio yake kuwa kuanzishwa kwa kituo cha Usaidizi wa Kisheria Mtimbira kutapunguza mlundikano wa kesi zisizo za lazima kufikishwa Mahakamani. Hivyo aliwataka vijana waliofundishwa kuchapa kazi kwa weledi na wananchi kukitumia kituo hiki ili kiwe msaada kwao.

Kwa namna ya pekee, kama sehemu ya Mchango wao wa awali, Afisa Mtendaji Kata ya Mtimbira Ndg. Rajab Mgululi alitoa bure ukumbi wa Kata ili kufanyia mafunzo. Pia kwa kushirikiana na Mhe. Diwani pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtimbira wameahidi kutoa jengo moja litumike kama ofisi ya awali ya Wasaidizi wa Kisheria. Hii ni hatua kubwa sana katika kufanikisha kazi hii ya usaidizi wa Kisheria katika Ulanga.

Ni malengo ya Taasisi kuanzisha vituo vya usaidizi wa kisheria maeneo mengi zaidi ikiwa na uwezo.

Tunakaribisha maoni, ushauri na michango mbalimbali ya hali na mali ili Taasisi hii iweze kusimama. Kama utapenda kuchangia au kutoa mawazo yako au maoni yako usisite kutuandikia: ucrc2012@gmail.com au kutupigia simu +255 755831152

UCRC- Lean.Analyse.Take Action


No comments:

Post a Comment