HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Sunday, January 13, 2013

Tamasha kubwa kumuenzi Regia Mtema laja


Na Senior Libonge, Ifakara

WAKATI familia ya aliyekuwa mbunge wa viti maalum jimbo la Kilombero marehemu Regia Mtema ikiandaa tarehe 14 Januari mwaka huu kuwa ni siku ya Regia kwa kuandaa hafla kubwa jijini Dar es Salaam,pia shughuli maalum zitafanyika wilayani Kilombero ambapo ndiko marehemu alipokuwa akitumikia wananchi wa jimbo hilo.


Aliyekuwa Mbunge wa Kilombero (Viti Maalum CHADEMA) Marehemu Regia Mtema

Akizungumza na Blog blog hii mjini Ifakara,mratibu wa shughuli hizo wilaya ya Kilombero Antony Kamonalelo amesema kuwa amepewa jukumu hilo kutoka kwa famila ya marehemu ambao wameanzisha Regia Mtema Foundation na shughuli kubwa zitakayofanyika wilayani hapa ni zoezi la upandaji miti,usafi wa mazingira na matembezi ya mshikamano.

Kamonalelo amesema kuwa shughuli hizo zitaanza tarehe 16 mwezi huu kwa wananchi kupanda miti na shughuli itaanza katika shule ya msingi Maendeleo na siku inayofuata litafuatia zoezi la usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mji wa Ifakara na viunga vyake hasa katika vituo vya kuhudumia watoto wenye matatizo mbalimbali,hospitali ya rufaa ya Mt.Francis na soko kuu la Ifakara.

Kwa mujibu wa Kamonalelo tarehe 18 ndio itakuwa mwisho wa shughuli hiyo ambapo kutakuwa na matembezi ya mshikamano yatakayoanzia katika mzunguko wa Kibaoni na kuelekea katika makabuli ya kwa Mkuya katika kijiji cha Lipangalala ambako ndiko alipozikwa na wakishafika hapo shughu itakayofuatia ni kufanya usafina kisha kuwasha mishumaa ikiwa ni ishara ya kumkumbuka kipenzi cha wana Kilombero.

Amesema shughuli zote hizo zitaongozwa na mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala hivyo kutoa wito kwa wananchi wote wilayani Kilombero bila kujadi itikadi za kisiasa na kidini kujitokeza kwa wingi katika shughuli zote za siku tatu kutokana na marehemu alikuwa mtu wa watu.

Huku shughuli za kumkumbuka marehemu Regia Mtema zikitarajia kufanyika hivyo wilayani Kilombero jijini Dar es Salaam shughuli maalum itafanyika Januari 14 katika hoteli ya Peacock ambapo Regia Mtema Foundation wamesema kuwa kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia marehemu.

Taarifa zilizosambazwa kwa vyombo vya habari na familia ya marehemu zimeeleza kuwa katika siku hiyo maalum wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki na hafla itaanza saa 9 alasiri na kumalizika saa 2 usiku katika hoteli ya Peacock na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku.

Kwa mujibu wa famila ya marehemu ratiba kamili itahusisha matukio kadhaa yakiwemo historia ya Regia itakayowasilishwa na Mbunge David Kafulila,mada juu ya rushwa itakayowasilishwa na Takukuru na Ulemavu sio kutoweza itakayowasilishwa na Shida Salum mwenyekiti wa CHAWATA.

Pia Mh January Makamba atawasilisha mada ya nafasi ya kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia,makala za Regia na pia nasaha kutoka kwa wabunge Mh Zito Kabwe na John Mnyika,Hussen Bashe na mzee Mtema zitatolewa.

Marehemu Regia Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu Januari 14 mwaka jana baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupinduka na kusababisha kifo chake na baadaye kuzikwa mjini Ifakara katika mazishi yaliyokusanya watu wengi yaliyoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment