Henry
Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero
Kitongoji
cha Ifakara mjini katika Kipindi cha Julai hadi Oktoba kimevuka lengo kwa
ukusanyaji wa michango ya maendeleo kutoka kwa jamii kwa muujibu wa Taarifa ya
Kamati ya Maendeleo ya Kata.
Taarifa
ya Michango ya Maendeleo ya Kata ya Ifakara Mjini kwa mwaka huu, iliyotolewa
katika kikao cha Kamati ya Maendeleo ya Kata(KMK) cha Hivi Karibuni, imeeleza
kuwa kitongoji cha Ifakara mjini Kimepangiwa kukusanya michango ya maendeleo
kutoka kwa Jamii shs.4,776,000/= kutoka nguvu kazi 1,592 iliyopo, lakini
iimekusanya jumla ya shs.4,974,000/=na kuvuka lengo la shs.198,000/=.
Taarifa
hiyo imezidi kueleza kuwa kitongoji cha Mkuya kimekusanya mchango wa maendeleo kutoka kwa jamii shs.
1,806,000/= wakati lengo walilopangiwa ni kukusanya shs.1,812,000/= kutoka
nguvu kazi 604 iliyopo katika kitongoji hicho.
Kitongoji
cha Nduna kwa Muujibu wa Tarifa,hakijafanya vizuri katika zoezi la ukusanyaji
wa Michango ya Maendeleo, ambapo lengo wamepangiwa kukusanya shs.5,235,000/=
kutoka nguvu kazi 1745 iliyopo katika kitongoji hicho, lakini imekusanya jumla
ya shs.2,766,000/= na inadaiwa shs.2,469,000/= ambazo bado hazijachangwa.
Taarifa inaonesha Kitongoji cha Nduna kina nguvu
kazi 823 ambayo bado haijachangia michango yao ya Maendeleo hadi kufikia Oktoba
15 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment