Henry Bernard Mwakifuna,
Mchombe-Kilombero
KUTOKUWAPO kwa utaratibu mzuri
unaotumika kuwasimamia ili kuhakikisha Wafugaji Wavamizi wanatoka nje ya Wilaya
ya Kilombero imekuwa Changamoto mojawapo katika Operesheni Okoa Bonde la
Kilombero.
Bwana Madaraka Amani,
AfIsa Wanyamapori Wilaya ya Kilombero amewambia waandishi wa Habari
waliotembelea operesheni hiyo kuwa wavamizi wanaotozwa faini na kuamriwa
kuondoka nje ya Wilaya hii wamekuwa wanazunguka zunguka ndani ya Wilaya hiyo na
kisha kurudi kufuatia kutokuwapo Utaratibu mzuri.
Amesema kuna tetezi za suala hilo na
Watakaobainika watapelekwa moja kwa moja Mahakamani kwani watakuwa wamevunja
Sheria na kukiuka maagizo ya Serikali.
Ameongeza kuwa Wafugaji Wavamizi
awali waliekezwa waende Lindi ambapo walitengewa maeneo na aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bwana Said Mecky Sadiq kwa zaidi ya Ng’ombe Laki moja
ambapo Takwimu zinaonesha ni N’gombe Elfu Ishirini na mbili tu ndiyo walioenda
huko.
Sababu kubwa anabainisha Bwana
Madaraka ni kuwa Bonde la Kilombero lina malisho bora yenye Virutubisho kwa
Mifugo inayopelekea Mifugo kama N’gombe kuzaa kila Mwaka hivyo kupelekea
Wafugaji kukahidi kuondoka.
Wakati huo huo, Bwana Madaraka
Amani amesema kuwa Sheria Tisa zinatumika katika operesheni okoa Bonde Tengefu
la Kilombero.
Amezitaji
Sheria hizo kuwa ni Sheria ya Mazingira, Sheria ya Wanyamapori,
Sheria ya Misitu na Sheria ya Ardhi ya Vijiji.
Nyingine ni
Sheria ya Uhamishaji wa Mifugo, Sheria ya Kuweka Alama Mifugo na Sheria ya
Mipango ya Matumizi bora ya Ardhi.
Operesheni
Okoa Bonde Tengefu la Kilombero lenye Ukubwa wa Kilometa 7,697 likihusisha
Vijiji 228 limeanza Tangu Mwishoni mwa Mwezi Uliopita na katika Wilaya ya
Kilombero ilianzia katika Tarafa ya Mlimba na kwa sasa ipo Kata ya Mchombe.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Elias Masala amesema kuwa Sheria kuu
zinazotumika katika Operesheni hii ni ile ya Wanyamapori kipengele cha 116 (2)
kisemacho Afisa amepewa kutoza faini ya kiwango kisichopungua Elfu 20 na
kisichozidi shilingi Milioni 10 kwa kosa moja.
Sheria ndogondogo za Kilimo na
Mifugo chini ya Halmashauri za mwaka 2007 sheria kifungu cha 10 kinachosema
faini isizidi shilingi Laki Tatu ni sheria ya pili inayotumika katika
operesheni Okoa Bonde la Kilombero.
Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kilombero kwa sasa wanatoza Faini ya Kati ya Shilingi Elfu 10 na Elfu 40 kwa
kosa moja.
No comments:
Post a Comment