Henry Bernard
Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.
WANACHAMA 927 wa
Mfuko wa Mzunguko wa Shirika lisilo la Kiserikali la Camfed wana akiba ya jumla
ya Shilingi 81,964,000 ambazo zipo kwa ajili ya kukopeshana.
Bi.Tukaeje Habibu, Afisa
Mradi Camfed Tanzania, akitoa Taarifa ya Mwaka ya Mfuko wa Mzunguko amesema
Wanachama hao wana Jumla ya Shilingi Milioni 32.4 na Camfed imewapatia msaada
wa Shilingi milioni 49,520,000.
Amesema kuwa mfuko huo
umeweza kuwanufaisha Wanachama kutoka Wilaya Kumi nchini Tanzania na tayari
wanachama wameanza kuchukua Mikopo kutoka kwenye Mfuko huo.
Ameongeza kuwa
changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni baadhi ya Viongozi wa Vikundi
vinavyofadhiliwa na Shirika hilo kula fedha huku akizitaja Wilaya za Kilolo,
Kilosa na Kilombero zikiongoza kwa Utafunaji wa Fedha hizo.
Kwa upande wa Kilolo Viongozi
Watatu wametafuna Jumla ya Shilingi Milioni 2,140,000, kwa upande wa Kilombero kiongozi
mmoja ametafuna 453,000 na Kilosa kiongozi mmoja ametafuna Laki
190,000.
Kwa upande wake Nasikiwa
Duke, Afisa Mradi wa Young Women wa Shirika la Camfed akitoa
Ripoti ya Mwaka amesema kuwa Shirika hilo mpaka sasa linafanya kazi na Shule
540 likiwa na Miradi aina mbili ambayo ni kumsaidia Mtoto wa Kike na
kumwendeleza kiuchumi.
Viongozi hao wa Camfed
Shirika lenye Makao Makuu Nchini Uingereza linalofanya kazi na Nchi Tano kwa
sasa ikiwemo Tanzania waliyasema hayo walipokuwa katika Mkutano wa Mwaka
uliofanyika Ifakara, Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na
Wanachama kutoka Wilaya Kumi nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment