Henry Bernard Mwakifuna,
Ifakara-Kilombero.
Ng'ombe wakiwa wanaondoka kutoka maeneo ya Bonde Tengefu la Kilombero, pichani Mfugaji akiwa ametangulia mbele eneo la KIjiji cha Njage, Wilayani Kilombero.
JUMLA ya Mifugo Elfu Hamsini(52,000)
na Mbili inatarajiwa kuondolewa katika Bonde la Hifadhi la Kilombero.
Akizungumza Ofisini kwake na
Wanahabari waliokuwa wakitembelea Zoezi la Operesheni Okoa Bonde la Kilombero,
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amesema kuwa mpaka kufikia sasa Mifugo Elfu 21,375 imeuzwa na wenye
mifugo katika Minada ya maeneo yaliyotengwa na Serikali kwa kuhifadhia mifugo
iliyokamatwa.
Mifugo 3,546 imetozwa Faini, kila
mfugo umetozwa shilingi Elfu 10 huku Mifugo 2,565 imesafirishwa nje ya Wilaya
ya Kilombero.
Lengo kubwa la Operesheni Okoa Bonde
la Kilombero ni kuhakikisha Mifugo yote iliyozidi kuondoka katika Bonde Tengefu
la Kilombero.
Amesema Changamoto kubwa
inalolikumba zoezi hili ni faini kuonekana si Tatizo kwa Wafugaji na Halmashauri kupitia Sheria
ndogo ndogo imepandisha Faini mpaka kufikia shilingi Elfu 20 kwa Ng’ombe.
Ameongeza kuwa operesheni ilipangwa
kufanyika kwa siku 4 lakini kutokana na Ugumu wa kazi yenyewe imeongezwa siku mpaka
vijiji vyote vyenye idadi kubwa ya Mifugo vitakapopitiwa.
Operesheni okoa bonde la Kilombero
ilifunguliwa Tarehe 30 mwezi Oktoba Rasmi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Bwana Said Mecky Sadiq na ukamataji Rasmi ulianza Oktoba 31.
No comments:
Post a Comment