Henry Bernard
Mwakifuna, Lupiro-Ulanga
JUMLA ya Shilingi
Milioni 6,900,000/ zinahitajika kwa ajili ya umaliziaji wa Madarasa
Mawili katika shule ya Sekondari Lupiro iliyopo katika kata ya Lupiro Wilayani
Ulanga.
Diwani wa Kata hiyo Bwana
Nassoro Mchalange, amesema kuwa fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya
umaliziaji wa madarasa mawili ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi
wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Amesema kuwa
kukamilika kwa Madarasa hayo kutatoa fursa kwa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza
ambao wanatarajiwa kujiunga mwezi Januari mwaka 2013 .
Kutokana na kuishiwa
kwa fedha za umaliziaji wa Madarasa hayo Bwana Mchalange ameiomba Halmashauri
ya Wilaya kuwasaidia fedha hizo ili waweze kukamilisha lengo hilo kwani hatua
iliyobakia ni kupiga lipu ili madarasa yaweze kuwa tayari kutumika.
No comments:
Post a Comment