Henry Bernard
Mwakifuna, Ifakara-Kilombero.
JUMLA ya Shilingi
Milioni 544 sawa na Asilimia 84.8 ya lengo zimekusanywa na Halmashauri ya
Wilaya ya Kilombero kutokana na Ushuru katika kipindi cha Mwezi
Julai hadi Septemba mwaka huu huku lengo likiwa ni kukusanya Shilingi Milioni
647.
Taarifa ya Kamati ya
Fedha iliyotolewa katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi hivi Karibuni
imeeleza kuwa ukusanyaji wa ushuru katika wilaya hiyo umeshuka .
Katika kipindi cha
Julai hadi Septemba mwaka huu, Halmashauri hiyo imekusanya ushuru kutoka
kampuni ya Kilombero Plantation Limited (KPL) iliyopo kata ya Mngeta
shs. milion 16 tu wakati lengo lilikuwa kukusanya shs. milion 30 kila mwezi.
Taarifa hiyo imezidi
kueleza kwa upande wa Minada katika kipindi hicho Halmashauri hiyo
imekusanya ushuru shs. milion 2 tu, lengo lilikuwa kukusanya shs. milion 7,
ushuru wa Soko imekusanya shs. milion 3 wakati lengo ilikuwa
kukusanya shs. milion 23, ushuru wanyumba za kulala wageni imekusanya shs.
milion 17,748,050 ni sawa na asililimia 17 lengo lilikuwa kukusanya shs. milion
98,776,000|= na ushuru wa miwa imekusanya shs. milion 18 ni sawa na
asilimia 14 lengo lilikuwa kukusanya shs milion 127.
Wakati huo huo Wajumbe
wa Baraza hilo wamewataka Maafisa Watendaji wa Kata 21 waliopo katika Wilaya ya
Kilombero kufanya kazi ya ziada ya kukusanya ushuru ili kuiletea mapato makubwa
Halmashauri hiyo ili iweze kuleta maendeleo kutokana na miradi inayopangwa
kutekelezwa.
Wamesema Watendaji wa
Kata mwishoni mwa mwaka jana wamepewa Pikipiki ili kufuatilia ukusanyaji wa
ushuru katika kata zao lakini matokeo yake mapato yatokanayo na ushuru
yameshuka.
Kati ya Kata 21, Kata
za Idete na Mofu kwa muujibu wa Taarifa ya Kamati ya Fedha hazikufanya
Vizuri katika Zoezi la Ukusanyaji Ushuru katika Kipindi hicho cha Julai hadi
Septemba.
Mbali ya hilo Wajumbe
wa Kamati ya Fedha wametakiwa kubuni mbinu mbadala ya kuingizia mapato
Halmashauri ya Wilaya, huku kamati hiyo ya Fedha ikitoa Pendekezo la kulirudisha geti
la Idete ili mapato yaweze kuongezeka, lakini wajumbe wa Baraza
hilo wamekataa pendekezo hilo.
No comments:
Post a Comment