Henry Bernard Mwakifuna,
Ifakara-Kilombero.
MKUU wa Wilaya ya Kilombero Bwana
Hassan Masala amesema kiongozi yoyote atakayewaficha Wavamizi wa Bonde
la Kilombero atachukuliwa hatua za Kisheria.
Amesema kuna taarifa kutoka kwa
Wananchi kuwa kuna baadhi ya Viongozi wa Vijiji wamekuwa wakiwakingia Kifua
Wafugaji kwa kuwapa taarifa za siku ambayo zoezi litafanyika katika maeneo yao
na kuwaficha Wavamizi na Wakulima walioingia katika mipaka ya Bonde Tengefu la
Kilombero.
Ameomba ushirikiano kutoka kwa
Wananchi ili kuweza kuwabaini wale wote wanaokwamisha zoezi hili la Uhifadhi wa
Bonde hili huku akitilia mkazo kuwa Zoezi si la Mkuu wa Wilaya.
Wakati huo huo Mkuu huyo wa
Wilaya amesema kuwa Mifugo mingi kwa kiasi kikubwa imeanza kuondoka Wilayani
Kilombero.
Ametilia mkazo kuwa si mifugo yote
inatarajiwa kuondolewa Wialayani humo bali ile isiyo na Chapa na iliyozidi
kulingana na Eneo lililotengwa kwa malisho.
Operesheni okoa Bonde la Mto
Kilombero iliyopangwa kuisha baada ya siku Nne itaendelea mpaka Viji vyote
vyenye Mifugo mingi kubainika na ni zoezi endelevu.
No comments:
Post a Comment