Na Henry Bernard Mwakifuna, Uchindile-Kilombero
JUMLA ya Vijana 97 katika Kata ya Uchindile wanatarajiwa kumaliza Mafunzo ya Mgambo mwanzoni mwa mwezi wa Novemba 2012.
Akisoma Risala ya Wanamgambo Mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala, Afisa Mteule Daraja la II ambaye pia ni Mshauri wa Mhgambo Wilaya ya Kilombero Abel Daniel Luhwago amesema kati ya Vijana hao ambao wametimiza Wiki 13 za Mafunzo kwa Sasa, Vijana 81 ni wa Kiume na 16 ni Wa kike.
Amesema kuwa walipoanza kuandikisha jumla ya Vijana 250 walijitokeza lakini Utaratibu ni Vijana 100 tu ndiyo walichukuliwa huku Kijana mmoja wa kiume akishindwa kuendelea na Mafunzo kutokana na ajali ya moto aliyoipata na Wasichana Wawili mmoja akitoroshwa na mwingine hajulikani alipo.
Ameomba Vijana hao wa Mgambo wapewe kipaumbele katika fursa zinapojitokeza, wapatiwe Unifomu kila intake inapoanza na kufundishwa soma la Uraia ambalo mpaka sasa bado hawajafundishwa.
Mafunzo hayo ya Wiki 16 yamefanyika ikiwa imepita miaka 26 kwa mara ya Mwisho kufanyika katika Kata ya Uchindile mwaka 1986.
No comments:
Post a Comment