Henry Bernard Mwakifuna,
Itete-Ulanga
UVAMIZI wa Makazi, Kilimo na Mifugo
ni sababu kubwa zinazopelekea kutoweka kwa baadhi ya Wanyama katika Hifadhi ya
Bonde Tengefu la Kilombero.
Bwana Hassan Masala, Mkuu
wa Wailaya ya Kilombero akisoma Risala ya Hali Halisi ya Bonde Tengefu la
Kilombero katika uzinduzi wa Operesheni Okoa Bonde la Kilombero iliyofanyika
hii leo Tarehe 30/10/2012 katika Kata ya Itete Wilayani Ulanga amesema kuwa
Wanyama waliokuwapo katika Bonde hilo wamepungua kwa asilimia kubwa .
Amesema kuwa kulikuwa na Nyati
35,301 Mwaka 1991 lakini Mwaka 2009 Sensa ya Wanyama hao imebakia ni 1462 ni
asilimia 4 tu ya wanyama hao, Mwaka 1991 kulikuwa na Tembo 1848 lakini Sensa ya
Mwaka 2009 wamebakia Tembo 1,535.
Wakati Wanyama adimu aina ya Sheshe
ambao ni jamii ya wanyama wanaopatikana sehemu 18 tu Duniani ikiwemo Kilombero
wamebakia 18,161 Mwaka 2009 kutoka 36,569 Mwaka 1991 kwa muujibu wa Takwimu
zilizofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori nchini (TAWIRI).
Bonde Tengefu la Kilombero ni Makazi
ya Asilimia 75 ya Sheshe wote wanaopatikana Duniani na Wito umetolewa kuweza
kuwalinda wanyama hao wanaotoweka kwa kasi Ulimwenguni.
Operesheni Okoa Bonde la Kilombero
imezinduliwa leo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Said Mecky
Sadiq, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment