Na Henry Bernard Mwakifuna- Ifakara
Afisa Tarafa Kata ya Ifakara Bi Hawa Lumuli Mposo amewataka wakazi wa Wilaya ya Kilombero kuyatunza mazingira yanayo wazunguka pamoja na kuchunguza makazi yao ili kuepukana na tatizo la majanga.
Bi.Hawa ameeleza kuwa ni vyema kupanda miti mingi ili kuzuia kimbunga,kuacha kilimo cha kuhamahama,pia ni vyema kuzuia mwendo kasi na ujazo wa abiria katika vyombo vya usafiri ili kuzuia majanga ya ajari za barabarani.
Aidha Bi. Hawa amewataka watu kuchunguza nyaya za umeme katika nyumba zao ili kupunguza maafa ya moto na kuwataka wananchi wawe na vifaa vya asili kwa ajili ya kuzimia moto.
Pia amesema Tatizo la mafuriko linasababishwa na watu wanao chimba mchanga ndani ya mto nakuzuia mifereji ya kupitishia maji kutoka mito midogomidogo kwenda kwenye mto mkubwa wa Kilombero watu wanatumia mifereji hiyo kama sehemu ya kutupia taka mto ukijaa unasababisha mafuriko na kuleta majanga.
No comments:
Post a Comment