Henry Bernard Mwakifuna, Namhanga Ulanga
ZAIDI ya Ngombe na Mbuzi 20 wamekufa kwa kukosa maji katika Kitongoji cha Mbenja, kijiji cha Namuhanga Wilayani Ulanga.
Nkuba Ngwandu, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wafugaji cha Mbenja Livestock cooperative amesema Mifugo hiyo imekufa kutokan na Serikali Wilayani Ulanga kukataza kunywesha Maji mifugo yao katika Mto Mnjeta.
Mbali ya Tatizo hilo Wafugaji hao wamelalamikia Mipaka iliyowekwa na Serikali kuwa ipo ndani ya makazi yao.
Baadhi ya Wafugaji wamesema kuwa wameingia katia eneo la Mbenja kihalali baada ya kuomba maombi yao kwa serikali ya kijiji cha Namuhanga na kukubaliwa kuishi katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Namuhanga Bwana Iddi Lihogoya amekiri serikali kuwakataza Wafugaji kunywesha mifugo kyao katika Mto Mnjeta na Kuongeza kuwa Wafugaji hao wameingia kihalali katika kijiji hicho baada ya kuandika barua ya kuomba kuishi katika eneo la Mbenja na wananchi wa kijiji hicho kukubali.
Kwa upande wake Bwana Francis Miti , Mkuu wa Wilaya ya Ulanga amekiri Serikali kuwakataza Jamii ya Wafugaji wa eneo la Mbenja, kunywesha Mifugo yao katika Mto Mnjeta kwa kuwa tayari Maeneo hayo yapo katika Eneo la Hifadhi ambapo Shughuli zozote za Kuichumi ikiwa pamoja na Ufugaji hairuhusiwi kuingia katika Eneo hilo.
Amewataka Wafugaji kuchimba Mabwawa ya kunyweshea mifugo yao ili kuokoa mifugo yao inayokufa kwa kukosa maji ambapo hapo awali wamekuwa wakitegemea kunywesha mifugo yao katika mto mnjetwa.
Amesema wafugaji wajitokeze kuchimba mabwawa ya maji na serikali inaweza kuwasaidia katika kuchimba mabwawa ya maji baada ya nguvu zao kuonyesha kwanza.
No comments:
Post a Comment