Henry Bernard Mwakifuna, Ifakara-kilombero
KIKUNDI Cha Ngoma za Asilia cha Twende na Wakati cha Iragua Wilayani Ulanga kimeibuka na Ushindi wa Kwanza katika Fainali ya Ngoma za Utamaduni kwa Makabila yenye Asili ya Wilaya za Ulanga na Kilombero.
Mratibu Mwenza wa Mashindano hayo Bi. Vaileti Mbwilo ameuambia Mtandao huu kuwa Washindi hao waliojinyakulia Shilingi laki 2 na T-shirt 15 huku Wakisubiri Laki 2 nyingine kutokana na Ahadi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero Ramadhani Kiombile kuahidi kuongeza Laki 2 kwa Mshindi wa Kwanza hadi wa Tatu wamevipiku Vikundi vingine Sita vya Utamaduni vyote kutoka Wilayani Kilombero.
Washindi wa Pili ni kundi la Maji Marefu kutoka Katindiuka Wilayani Kilombero waliojinyakulia Shiliki Laki Moja na Nusu na T shirt 15 huku wakisubiri fedha Laki Mbili nyingine za Ahadi.
Washindi wa Tatu ni kundi la Lumumba kutoka Mangwale Wilayani Kilombero waliopata Laki Moja, T-Shirt 15 na Kusubiri Ahadi ya Shilingi Laki 2 za Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombero.
Vikundi vingine vilivyoingia hatua ya Fainali ni Saga na Kukoboa cha Kibaoni, Gunia Tupu Halisimani cha Mlabani,Fuka Fuka cha Lipangalalal na Ya Kale ni Dhahabu vyote kutoka Wilayani Kilombero.
Katika mashindano hayo yaliyoanza Septemba 2 katika hatua ya Nusu Fainali yaligubikwa na Huzuni kufuatia kifo Cha Mpiga Ngoma Mahiri wa Kundi la Maji Marefu la Katindiuka Marehemu Hadji Mtumbika aliyeanguka muda mfupi na kupoteza fahamu na kufa baada ya Kikundi chake kutoka jukwaani na kupoteza maisha.
Kwa muujibu wa Kaka wa Marehemu aliyefahamika kwa jina la Shaaban Mtumbika amesema kuwa mdogo wake amekufa kifo cha kawaida na kusiwe na Imani zozote juu ya hilo kwa nduguye alikuwa na Matatizo ya Moyo, uvimbe Tumboni na Presha waliyoigundua miezi 3 kabla ya kukutwa na Mahuti.
Marehemu alizikwa kijijini kwao Katindiuka nje kidogo ya Mji wa Ifakara.
Mpaka Taarifa hii inakwenda mtandaoni Vikundi hivyo bado havijapata Fedha Laki mbili ilyokuwa imeahidiwa kwa kikundi kitakachoshika nafasi ya kwanza , ya pili na ya Tatu ahadi iliyotolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero siku ya Ufunguzi wa Mashindano hayo.
Shindano hilo la kukuza utamaduni kwa Wenyeji wa Makabila ya Wilaya za Ulanga na Kilombero liliandaliwa na Kituo cha Redio Pambazuko FM Ifakara wakishirikiana na Makutano Club na yameendeshwa Kila jumapili kwa Mwezi mzima wa Septemba.
No comments:
Post a Comment