Henry Bernard Mwakifuna, Sanje-Kilombero
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amepongeza hatua iliyofikiwa katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Ardhi uliojitokeza kati ya Mwekezaji na Serikali ya Kijiji cha Sanje katika Wilaya hiyo.
Akitoa maelezo baada ya kupitia mapendekezo yaliyomo katika waraka wa mapendekezo ya suluhu ya mgogoro huo Mkuu huyo amesema kuwa atasaidia kupata Wataalamu ili kufanya tathimini ya Athari zinazoweza kutokea kufuatia Mto Sanje uliokuwa umehama katika njia yake ya asili na kumega eneo la serikali ya kijiji na kwenda katika eneo la mwekezaji.
Wataalamu kutoka idara ya Ardhi, mazingira na Mipango miji wameagizwa kwenda kufanya tathimini ya athari na nini cha kufanya ili kuweza kunusuru hali ya eneo la Mto Sanje linalomeguka.
Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa ajili ya kupata suluhu ya Tatizo la Mpaka kufuatia Mto Sanje kuhama eneo lake la Asili kati ya mapendekezo yake ni Kufanyika kwa tathmini ya Kimazingira ya mwenendo wa Mto unapojaa na kupungua ili kuchukuliwa hatua zinazostahili.
Taarifa hiyo yenye Mapendekezo Sita iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Afisa Tarafa ya Mang'ula Victor Ndiva imependekeza msingi uliochimbwa ufukiwe kwa usaidizi wa Mzee Mohamedi Khalfani (Mwekezaji) kwa kuwa ndiyo chanzo cha Wananchi na Viongozi kufikishwa Mahakamani.

No comments:
Post a Comment