SERIKALI Wilayani Kilombero
imetangaza kwa Wafugaji wavamizi walioshauriwa kuondoka waanze kufanya hivyo
kabla ya Oparesheni maalumu ya kuwaondoa kuanza Rasmi Mwisho wa Mwezi Oktoba.
Bwana Hassan Masala,Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero katika Tangazo alilolitoa amesema kuwa wale wote
Wafugaji wenye mifugo mingi waliovamia maeneo yasiyoruhusiwa waondoke mapema
kabla ya tarehe 30 Oktoba 2012 ambapo oparesheni maalum itaanza.
Ametanabaisha kuwa Wafugaji wavamizi
ni wale walioingia kijijini bila ya kupokelewa na Serikali ya kijiji na
Kuthibitishwa na Mkutano wa Kijiji huku pia kukiwa na kundi jingine la Wafugaji
lenye Mifugo ambayo haijapigwa Chapa na kutambuliwa na Serikali kufuatana na
eneo la Malisho lililotengwa kwa Kijiji husika.
Wataalamu wa Idara ya Mifugo wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero wametenga maeneo ya Malisho kwa Kila Kijiji
chenye Wafugaji huku eneo hilo likipimwa kwa idadi maalumu ya Mifugo
inayotakiwa kuwepo kutokana na ukubwa wa eneo hilo.
Mbali ya Suala la Wafugaji wavamizi
Mkuu wa Wilaya amewataka Wakulima waliovamia eneo la Hifadhi ambalo kisheria
haliruhusiwi kufanyika shughuli za Kibinadamu waondoke mara moja sanjari
na Wafugaji wavamizi.
Serikali ilitangaza ifikapo Septemba
7 kuwa Mwisho wa kuondoa mifugo kwa Hiari Katika Bonde la Mto Kilombero lakini
kutokana na shughulili za Kitaifa za Sensa na Mchakato wa kupata Katiba Mpya
zoezi la kuwaondoa kwa nguvu likasogezwa mbele na kwa sasa limeandaliwa rasmi
kuanza mmwisho wa Mwezi huu.
No comments:
Post a Comment