Na Henry Bernard Mwakifuna, Uchindile-Kilombero
JUMLA ya Shilingi Milioni 29,649, 750/ ikiwa na Fedha na Nguvu kazi zimetumika kwa ajili ya Kukarabati Zahanati ya Kata ya Uchindile iliyopo Wilayani Kilombero.
Peter Magokola, Mganga Kiongozi wa Zahanati ya Uchindile amemweleza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassana Masala alipotembelea jengo la Zahanati hiyo kuwa Nguvu kazi ya Wananchi Tangu Mwaka 2010 ni Matofali, Mchanga,Kokoto na huduma nyingine thamani yake Milioni 4,240,000/ wakati Fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ni Milioni 22,409,750/ hadi kukamilika kwa Zahanati hiyo.
Awali akisoma Risala ya Wanakijiji wa Kata ya Uchindile Mratibu wa Elimu wa Kata hiyo Mwalimu Maiko Mwangosi amesea katika Kipengele cha Elimu kuna upungufu katika Idara ya Afya ya Mtumishi wa Maabara huku mwitikio hafifu wa Jamii katika kuchangia mfuko wa Jamii wa Afya (C.H.F).
Zahanati ya Uchindile inayohudumia vijiji vya Lugala,Uchindile na Kitete ina Watumishi 3 tu wa Afya, katika katika kata hiyo yenye wakazi wanaokadiriwa 2302.
No comments:
Post a Comment