Henry Bernard Mwakifuna, Mang’ula-Kilombero
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unadaiwa Shilingi Milioni 6,137,822 kams mslipo ya Wanachama ywake katika kituo cha Afya cha Mang’ula.
Akiotoa taarifa ya Kituo cha Afya Mang’ula mbele ya Mkuu wa Wailaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala, Mganga Kiongozi wa Kituo hicho Daktari EUGEN SHIRIMA amesema moja kati ya Changamoto kubwa ni Mfuko huo kuchelewesha kulipa malipo ya fedha wanazodaiwa.
Amesema mbali ya changamoto hiyo ukosefu wa Gari la Wagonjwa katika Kituo hicho inasababishwa wagonjwa wa Rufaa kucheleweshwa kusafirishwa na wakati mwingine kupoteza masisha.
Gari la Wagonjwa lilolokuwa likitumika kituoni hapo la kwanza lilipata ajali na la pili limeharibika takribani miezi Mitatu sasa.
Ukosefu wa Wodi kwa ajili ya Wanaume na Mipaka ya Kituo cha Afya kuvamiwa ni changamoto nyingine zinazokikabili kituo cha Afya Mang’ula.
No comments:
Post a Comment