Na Senior Libonge, Ulanga
MADIWANI wa kambi ya upinzani katika
baraza la halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro jana walilazimika
kutoka nje na kususia kikao cha baraza hilo kufutia hoja ya kutaka diwani wa
mteule wa viti maalum kupitia tiketi ya chama cha wananchi
(CUF),Maricena Mchanga, kutupiliwa mbali na baraza hilo.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa
5.00 asubuhi muda mfupi mara baada ya mwenyekiti wa baraza hilo, Furaha
Lilonge, kufungua kikao hicho na kutaka madiwani kupitisha agenda za kikao
hicho na baada ya hapo hoja ya kupishwa kwa diwani huyo ilijitokeza.
Kujitokeza kwa hoja hiyo pia
kulifuatia mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Isabera Chilumba, kusema
kuwa katika agenda za hikao hicho kulisahaulika agenda zingine mbili za
kuapishwa kwa diwani huyo na kupokea ujumbe kutoka tume ya utumishi wa umma
ambao ulitaka kuzungumza na baraza hilo.
Hoja ya mkurugenzi huyo ilizua
mabishano baina ya madiwani wa halmashauri hiyo huku upande wa madiwani kutoka
chama tawala chama cha mapinduzi (CCM), wakitaka kanuni za uendeshaji wa kikao
cha baraza zizingatiwe kwa madai kuwa kuapishwa kwa diwani huyo kulipaswa
kufanyika kabla ya kufunguliwa kwa kikao hicho na kwamba kikao hicho kwa vile
kilikwisha anza hakikuwa sahihi kutumika kumuapisha.
Kauli hiyo aliyotolewa na diwani wa
wa kata ya Mawasiliano katika tarafa ya Mahenge, Mwanaidi Mkalimoto, na
kupingwa vikali na kambi ya upinzani ikiongozwa na diwani wa chama cha
demokrasia na maendeleo (Chadema), Said Tilla, ambaye alitaka haki ya diwani
huyo mteule izingatiwe.
Hata hivyo, malumbano hayo
yalimlazimu mwanasheria wa halmashauri hiyo, Bahati Kikoti, kutoa ufafanuzi
kuwa kanuni za wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI),
kuhusu uapishwaji wa madiwani zinaeleza kuwa diwani ataapishwa kabla ya kikao
chake cha kwanza na kushauri kuwa bado agenda ya kuapishwa kwa diweani huyo
ingeingizwa katika agenda za kikao hicho.
Licha ya kutoa ufafanuzi huo wa
mwanasheria, lakini mwenyekiti alisimamia hojas yake kwa kusema kuwa agenda ya
kuapishwa kwa diwani huyo mteule haitaingizwa miongoni mwa agenda hizo kutokana
na kanuni za uendeshaji wa baraza hilo kwa madai kuwa kwa kuwa madiwani
walikwisha pitisha agenda hizo agenda za ziada hazitaruhusiwa.
Hatua hiyo ya mwenyekiti wa
halmashauri iliwalazimu madiwani tisa wa kambi ya upinzani kunyanyuka na kutoka
nje wakipinga kuondolewa kwa hoja hiyo.
Diwani wa kata ya Lupiro (Chadema),
Nassoro Mcharange ameiambia blog hii kuwa maamuzi yaliyotolewa na mwenyekiti wa
halmashauri hiyo hayakuwa sahihi kwa vile diwani mteule alifika katika baraza
hilo kufutia barua ya halmashauri yenye kumbukumbu namba UDC/ADM/E.20/4/35
ikimtaka diwani huyo mteule kuhuzulia kikao hicho ili kuapishwa na kushiriki
kikao.
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Sofi katika tarafa ya Beatus Daud, kupitia tiketi ya TLP, alilalamikia maamuzi
yanayotolewa na mwenyekiti huyo kwa mdai kuwa amekuwa akiegemea kwenye chama
chake cha CCM.
Hata hivyo, mwenyekiti wa
halmashauri hiyo akijibu tuhuma hizo alisema kuwa uendeshaji wa baraza hilo
amekuwa akiufanya kwa kuzingatia kanuni za uendeshaji baraza tofauti na madai
yanayotolewa na madiwani wa kambi ya upinzani.
Akitoa ufafanuzi wa madiwani hao
kususia kikao hicho na kutoka nje alisema kuwa yako makosa yaliyofanywa na
halmsahuri hiyo juu ya uteuzi wa diwani mteule huyo kwa maelezo huwa chama cha
CUF kinadiwani mmoja wa kuchaguliwa hivyo hakikuwa na sifa ya kuwa na diwani wa
viti maalum.
Alidai kuwa chama cha Chadema na TLP
vimekuwa na sifa hiyo kutokana na kuwa na madiwani watatu kila kimoja na CCM
ilipata madiwani wanane wa viti maalum kwa kuwa na madiwani 24 wa kuchaguliwa
na wabunge wawili na kwamba kwa sifa ya diwani watatu kukiwezesha chama kupata
diwani wa viti maalum basi sifa hiyo ilikuwa ni CCM kuongezewa diwani mmoja na
siyo CUF.
“Tatizo linaonekena liko kwenye
uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa kuipotosha tume ya uchaguzi kuipatia
taarifa zilizoiwezesha tume kumteua diwani wa CUF, haki hiyo ilikuwa ni ya CCM
hivyo CCM wanapaswa kuidai haki hiyo,” alisema Lilongeli.
Naye diwani mteule aliyetarajiwa
kuapishwa katika baraza hilo, Mchwanga, alisema kuwa kutokjuapishwa kwake
katika kikao hicho kumemsikitisha kwa vile aliandikiwa barua na halmsahuri
kuhusu uteuzi uliofanywa na tume ya uchaguzi Agosti 14, mwaka huu na kumtaka
kuhuzulia kikao hicho ili aweze kuanza kutekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment