Na Henry Bernard Mwakifuna, Itete-Ulanga
WATUMISHI
watakaohusika na Operesheni Okoa Bonde la Kilombero wametakiwa kutenda Haki kwa
Kufuata Sheria.
Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Bwana Saidi Mecky Sadiq amesema kuwa suala
la uonevu na ukihukwaji wa sheria halina nafasi katika zoezi la
kuwaondosha Wafugaji na Wakulima Wavamizi kuwa watakaobainika watachukulia
Hatua kali dhidi yao kwa muujibu wa Sheria.
Amewataka
Maaskari watakaoendesha Operesheni hiyo kutotumia Nguvu isiyo ya Lazima kupita
kiasi huku akiwataka pia Wananchi nao kutochukua sheria mkononi kwa Silaha za
jadi ili kuepusha mapambano baina yao.
Bwana Sadiq
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam alikuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi
wa Operesheni Okoa Bonde la Kilombero iliyofanyika katika Kata ya Itete
Wilayani Ulanga.
Wakati huo huo Mifugo
itakayokamatwa ndani ya Hifadhi ya Pori Tengefu la Kilombero itapigwa Mnada kwa
Muujibu wa Sheria.
Bwana Hassan Masala, Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero akisoma Taarifa ya Hali Halisi ya Bonde la Kilombero
amesema Mifugo hiyo pamoja na ile isiyosajiliwa na kupigwa Chapa itauzwa na
Serikali kwa kufuata utaratibu wa Kisheria ulioandaliwa.
Amesema Vituo 11 vimetengwa kwa
Wilaya za Ulanga na Kilombero kwa ajili ya kuhifadhia Mifugo itakayokamatwa kwa
kukihuka utaratibu.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Kilombero
alikuwa akisoma Taarifa iliyoandaliwa juu ya Hali Halisi ya Bonde la Mto
Kilombero linalojumiisha Wilaya za Ulanga na Kilombero Mkoani
Morogoro.
No comments:
Post a Comment