HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Friday, September 7, 2012

Afisa Mtendaji Kata Kibaoni kizimbani kwa ubadhilifu

Na Senior Libonge,Kilombero

BAADA ya kujisalimisha mwenyewe katika ofisi ya mkuu wa wilaya,hatimaye afisa mtendaji wa kata ya Kibaoni wilayani hapa Joachim Lyembela leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya na kusomewa shitaka la upotevu wa fedha za halmashauri kiasi cha shilingi milioni 36.

Akisomesha shitaka hilo na mwendesha mashtaka msaidizi wa polisi Nassoro Bahame,imeelezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kati ya Disemba 2011 na Juni 2012 huko maeneo ya Kibaoni mjini Ifakara kwa kuchukua kiasi hicho cha fedha kutoka kwa mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kilombero.

Hata hivyo licha ya kukana shitaka hilo hakimu mfawidhi wa wilaya Paulo Kimicha ameiharisha kesi hiyo hadi Septemba 20 mwaka huu itakapotajwa tena baada ya ushahidi kutokamilika na mtuhumiwa amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaokuwa na mali isiyoamishika yenye thamani ya shilingi milioni 10.

Mtendaji huyo ambaye kwa miezi miwili hivi sasa alitoroka amejisalimisha mwenyewe Septemba 3 mwaka huu majira ya asubuhi katika ofisi ya mkuu wa wilaya na kukutana naye mwenyewe mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala ambaye naye baada ya mahojiano mafupi alimkabidhi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa mahojiano zaidi.

Tuhuma anazokabiliana nazo ni ubadhirifu mkubwa uliofanyika katika ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Kibaoni nah ii inatokana na ziara iliyofanywa na Masala katika shule hiyo na kujionea hali mbaya ya usimamizi wa ujenzi wa madarasa sita ya shule hiyo ambayo kwa sehemu kubwa michango yake ilitokana na nguvu za jamii pamoja na fedha kutoka serikalini kupitia halmashauri ya wilaya.

Baada ya kuona shule ikiwa katika hali hiyo huku mtendaji akikimbia, mkuu wa wilaya alitoa agizo kwa polisi kumkamata mtendaji huyo popote pale atakapopatikana ili kujibu tuhuma za matumizi ya makusanyo toka kwa wananchi bila ya kutunza kumbukumbu zozote,kukosekana kwa baadhi ya  stakabadhi za kukusanyia michango,kufanya matumizi bila idhini wala kushirikisha kamati ya ujenzi wa sekondari.

Aidha ukaguzi uliokuwa umefanyika shuleni hapo umebaini mtendaji huyo anadaiwa kiasi cha shilingi milioni 8,508,500 toka kwa watoa huduma na wasambazaji wa vifaa mbali mbali huku halmashauri ikitenga kiasi cha shilingi milioni 36 kwa ajili ya kusaidia umaliziaji na ukamilishaji wa madarasa sita katika shule ya sekondari ya kata hiyo.

Imeelezwa kuwa fedha hizo zilihifadhiwa katika akaunti ya maendeleo ya shule ya sekondari na kuchukuliwa kwa awamu chini ya maelekezo ya mtendaji huyo hata hivyo pesa hizo hazikutumika kwa kuzingatia taratibu za fedha za serikali na kulikuwa na utaratibu usioeleweka na hatarishi katika kuchukua na kutunza fedha hizo na hali hiyo iliyopelekea baadhi ya madarasa kati ya hayo sita kutokamilika na kwa yale yaliyokamilika kuwa chini ya kiwango.

Mapungufu hayo ni pamoja na kuezekea bati kwa kutumia mbao za mnazi na mbao  zilizokuwa zimeshaanza kuharibika lakini pia mbao zenyewe kuwa na vipimo visivyostahili na hali ambayo ingepelepelekea athari kubwa kwa watoto pindi madarasa hayo yangeruhusiwa kutumika na ilibidi mkuu wa wilaya kuagiza kusimamishwa kwa matumizi ya majengo hayo mpaka pale marekebisho yatakapofanyika na kwa mujibu wa wataalamu wa ujenzi jumla ya shilingi milioni 39  zinahitajitajika ili kugharamia zoezi hilo.

 Hata hivyo  katika sakata hilo pia mkuu wa wilaya amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kuwachukulia hatua baadhi ya wataalamu wake akiwemo Mhandisi wa ujenzi wilaya, afisa elimu ufundi na Afisa elimu sekondari wilaya  kwa kuacha mambo yanaharibika bila usimamizi wala ushauri hali iliyopelekea hasara kwa serikali.

Kwa sasa mtendaji huyo yupo mahabusu katika kituo cha polisi wilaya kwa uchunguzi zaidi na atapandishwa kizimbani mara baada ya uchunguzi wa tuhuma zake kukamilika kutokana na uzito wa suala lenyewe.

No comments:

Post a Comment