HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Tuesday, September 4, 2012

WAFUGAJI “WAVAMIZI” BONDE LA MTO KILOMBERO MWISHO SEPTEMBA 7

Henry  Bernard Mwakifuna, Ifakara-Kilombero


Serikali Wilayani Kilombero imetangaza hadi kufikia Septemba 7 mwaka huu 2012 itakuwa mwisho kwa Wafugaji Wavamizi na Wakulima waliovamia eneo la Hifadhi wawe wameondoka.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amesema kuwa Tangazo rasmi lilikuwa Mwisho ni Agosti ya 31 lakini kwa kugundua kuwa kuna Wananchi wanaweza kutoa Visingizio basi Serikali  imetoa hadi Septemba 7 kuwa itakuwa ni siku muafaka kwa Wafugaji Wavamizi na Wakulima waliovamia eneo la Hifadhi kuondoke.

Ameongeza kuwa hivi Karibuni Helikopta ya Kampuni ya M/S SWALA OIL & GAS LTD inayozunguka Anga la Kilombero kwa ajili ya kufanya Utafiti wa Uwepo wa Mafuta imegundua kuwapo N'gombe 8000 na Watu zaidi ya 2000 waliojificha Porini katika Bonde la Mto Kilombero.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Kilombero Bwana Everist Mmbaga akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Chisano kata ya Chisano amesisitiza kuwa zoezi hili harirudi nyuma na Serikali imejipanga kutumia Magari na Helkopta kuweza kubaini Mifugo iliyofichwa.

Amekemea baadhi ya Wafugaji kujaribu kuhamishia Mifugo Wilaya ya Jirani ya Ulanga ameonya kuwa zoezi hilo  ni la Wilaya zote zilizopo katika Bonde la Mto Kilombero.

Saidi kapate mmoja kati ya Wafugaji wa Kijiji cha Mgudeni, Mkangawalo Mchome amesema kuwa Zoezi la kutambua Mifugo  Vamizi linaloendelea Wilayani nKiolombero si Halali na limewashtua.

Wakati huo huo Tangazo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii limesisistiza kuwa ifikapo Tarehe 8 Septemba 2012 nguvu itatumika kuwaondoa wale wote walio kwenye pori Tengefu la Kilombero ambao watakuwa bado hawajaondoka.

Wizarardhi  pia imewapongeza Wananchi waliokubali kuhama kwa hiari yao kutoka Pori Tengefu la Kilombero baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

MBALI ya hilo Maafisa kutoka Idara ya Ardhi Wilayani Kilombero wanaendelea na zoezi la kuweka Alama ya Ushahidi (Witnes Mark) kutenganisha Ardhi ya Hifadhi na nyingineyo.

Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Kilombero ulishuhudia maofisa hao katika Misitu ya Jamii ya Kibasila kijiji cha Mofu wenye ukubwa wa Hekta 783.09 na Msitu wa Jamiii wa Mwokovu, Mchombe wenye Ukubwa wa hekta 747.78 wakiweka alama hizo.

No comments:

Post a Comment