HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Friday, September 7, 2012

"Wavamizi" bonde la Mto Kilombero mwisho leo

Na Senior Libonge,Kilombero/Ulanga
Leo ndio siku ya mwisho kwa wavamizi wote waliovamia eneo tengefu la bonde la Kilombero lililopo katika wilaya za Kilombero na Ulanga mkoani Morogoro kutoka kwa hiari eneo hilo kabla ya nguvu kutumika kuwaondoa wavamizi wote waliopo maeneo hayo.
Katika uhamasishaji wa mwisho kwa wavamizi hao kutoka maeneo hayo wakuu wa wilaya za Kilombero na Ulanga wametembelea maeneo mbalimbali katika wilaya zao kuwataka wavamizi hao kutoka maeneo hayo kabla serikali kuchukua hatua zaidi.
Nilifanikiwa kutembea na mkuu wa wilaya ya Kilombero katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili kujionea zoezi hilo linavyoendelea na jana tulikuwepo katika kata za Chita na Mofu ili kujionea uharibifu wa mazingira na pia kuongea na wananchi juu ya hatua ambazo serikali itachukua baada ya wale wavamizi watakaokaidi amri halali ya serikali.
Lakini tukiwa Chita tulikutana na jambo jipya la uharibifu wa misitu mikubwa ya milima ya Udzungwa inayofanywa na majangiri walioamua kuamia maeneo hayo kwa ajili ya kupasua mbao kutokana na misitu hiyo kushamiri misitu mikubwa yenye kila aina ya miti ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo inayoleta mandhari nzuri ya hewa na mvua katika maeneo ya kata nzima ya Chita.
Diwani wa kata hiyo Hassan Kidampa alisema uharibifu huo unafanywa na wananchi wachache wanaoshirikiana na maafisa wa maliasili ambao upasua mbao hizo kwa lengo la kuziuza na kila ukiwafuatilia ili kuwakamata wahusika hao maafisa wa maliasili uwakingia kifua ili wasichukuliwe hatua.
 Kidampa kwa kuona hali hiyo ikizidi siku hadi siku ilibidi amuombe mkuu wa wilaya kufika eneo hilo ili kujionea hali halisi na ilibidi mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala kufika katika kata hiyo na kuamua kuupanda mlima Udzungwa ili kujionea uharibifu wa misitu katika milima hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo imebaki kuwa pekee yenye nuru mkoani Morogoro baada ya milima ya Uluguru kuteketea baada ya kuvamiwa na wananchi na kufanya shughuli zilizopigwa marufuku katika milima hiyo ikiwemo ukataji miti,uchomaji mkaa na kilimo.
Ilibidi tuchukue zaidi ya saa moja kufikia kambi mbili za upasuaji mbao ambazo tulikuta miti imeshakatwa na tayari inasubiri kupasuliwa mbao ila wahisika walikimbia baada ya kusikia sauti ya timu yetu ikiingia katika msitu huo mnene ambapo shughuli ilikuwa pevu ya kupanda mawe na kufukuzana na nyoka wakali waliokuwepo maskani yao.
 Hata hivyo Masala aliliagiza jeshi la polisi kuwasaka kisha kuwakamata wahusika wote wanaoendeleza uharibifu katika msitu huo na watakaopatikana hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na zoezi hilo lilianza mara moja kwa polisi kwa kushirikiana na uongozi wa kata kuanza operesheni ya kuwasaka watuhumiwa baada ya kutajiwa majina yao.
Baada ya kutoka hapo Chita majira ya saa 8 ilibidi tuanze safari ya kuelekea kijiji cha Ikwambi kilichopo kata ya Mofu huko tulikuwa na mkutano na wananchi ambao walimweleza mkuu wa wilaya mambo mengi ila tatizo kuwa walimweleza mkuu huyo kuwa ni mipaka iliyowekwa na wataalamu wa ardhi na maliasili inayotenga ardhi ya kijiji na hifadhi ambapo wamesema kuwa imeingilia mipaka halali ya kijiji.
Wanakijiji hao wamesema kuwa mipaka hiyo mipya imeingia ndani zaidi ya mipaka ya kijiji na kusema kuwa mipaka hiyo itawafanye wakose maeneo ya kilimo kwani sehemu kubwa ya eneo la kilimo imeingizwa katika eneo la hifadhi hivyo kumuomba mkuu wa wilaya kuwasaidia ili kuwapatia ardhi ya kutosha kwa kilimo.
Hapo ndipo Masala alipowaambia uamuzi unaochukuliwa na serikali utawakera baadhi ya wananchi huku wengine ukiwafurahisha ila ukweli kuwa serikali haipendi kuona mwananchi wake anaumia na kusema kuwa mipaka iliyowekwa ni halali kwani wataalamu wametumia kifaa maalum cha kutambua mipaka yaani GPS.
Masala aliwataka wananchi wote wanaodai maeneo yao yameingiliwa waonyeshe stakabadhi zao kama kweli maeneo hayo ni halali kwao lakini hakuna hata mwananchi aliyeonyesha stakabadhi wala risiti na hapo inaonyesha kuwa wengi wao walivamia maeneo ya ardhi.
Akizungumzia operesheni itakayoanza hivi karibuni Masala alisema zoezi hilo litaanza kesho(terehe 8) katika maeneo yote yaliyozuiwa kufanyika shughuli zozote za mifugo na kilimo na kusema kuwa maeneo hayo yaachwe ili bonde hilo lirudi katika hali yake ya zamani kwa kuwa na wanyama wengi mfano sheshe na pia samaki wa aina mbalimbali akiwemo mjongwa.
Masala amesema kwa siku za karibuni imebainika kuwa bado wapo wavamizi zaidi ya 3000 katika maeneo hayo na mifugo zaidi ya 8000 waliojificha katika misitu minene lakini amesema hata wakijificha wapi watapatikana kwani zoezi litakuwa la anga na ardhini na mifugo itakayokamatwa itapigwa mnada na fedha zitapelekwa katika kijiji husika ili kufanya shughuli za maendeleo.
Shime kwa wananchi wa bonde la Kilombero kuwataja wavamizi wote waliopo maeneo hayo ili kurudisha hadhi ya bonde letu na wale wakulima walime maeneo yetu ya asili na sio hifadhi huku wafugaji halali kupunguza mifugo yao ili kwendana na maeneo yaliyopo na mifugo iliyozidi waiuze ili kwendana na maisha ya kisasa kwa kujenga nyumba za kisasa za biashara ama kununua magari.

No comments:

Post a Comment