HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Thursday, September 27, 2012

Mbuge Mteketa awataka wananchi Kilombero kuwajibika

Na Senior Libonge, Kilombero
MBUNGE wa jimbo la Kilombero Abdul Mteketa amewataka wakazi wa wilaya ya Kilombero kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuachana na zana kuwa serikali itashughulikia kila kitu.
Sambamba na hilo Mteketa pia amewaambia wananchi hao kuwa wawapuuze viongozi wa kisiasa wanauzunguka katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya hiyo kwa kuwarubuni wananchi kuwa wasichangie fedha za miradi mbalimbali na kusema kuwa watu hao wamefilisika kisiasa.
Akizungumza na wananchi wa kata za Mngeta na Mbingu wilayani humo,Mteketa amesema kuwa wakati wa kutegemea bure bure hivi sasa umekwisha ni wajibu wa kila mwananchi kuchangia maendeleo yake na serikali itasaidia pale inapoona inabidi kusaidia.
Ametolea mfano kuwa huduma za msingi kama ujenzi wa shule na zahanati ni wajibu kwanza wananchi kuchangia nguvu zao na shughuli ya umaliziaji inafanywa na serikali na hiyo ipo hata katika nchi zilizoendelea.
Amesema kuwa mwananchi ama kikundi kitakachokuwa tayari kuchukua mkopo kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya jamii yeye yupo tayari kusaidia ila wahusika wawe tayari kuchangia angalau nusu ya gharama ya mkopo huo.
Kauli hiyo ya Mteketa ameitoa baada ya wananchi wa kijiji cha Mkangalo kata ya Mngeta kushindwa kumalizia kukusanya tofari za ujenzi wa nyumba ya daktari wakati zahanati ya kijiji ikiwa imekamilika huku madawa toka serikalini yakiwa yamekwisha letwa.
Pia wananchi hao walimshangaza mbunge huyo kwa kushindwa kulima nyasi zilizozunguka zahanati hiyo kwa madai kuwa serikali ndiyo inapaswa kufanya usafi katika eneo hilo licha ya diwani wa kata ya Mngeta  Felician Kigawa kuwataka wakazi hao kufanya usafi huo.
Kuhusu baadhi ya wananchi kuzunguka na kuwadanganya wananchi,Mteketa amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu hao kwani uwaongopea mambo mengi kwa kuona kama wananchi wa jimbo hilo sio waelewa.
Amesema wakati wa siasa kwa sasa umekwisha na yeye ni mbunge halali wa jimbo hilo hadi mwaka 2015 na kuwataka wananchi kuwaogopa wanasiasa hao kama ukoma kwani hawana jipya badala ya kumwaga sera za vyama vyao wao umwaga matusi kwa lengo la kujenga chuki kati ya wananchi na serikali.
Katika ziara zake jimboni humo licha ya kutoa shukrani na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi pia mbunge huyo amekua akitoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali na pia utoa vitabu vya masomo ya sayansi.

No comments:

Post a Comment