HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Monday, September 3, 2012

WANANCHI wa kata za Chita, Mngeta na Mlimba wataka Viongozi wa Vijiji walipwe

Na Senior Libonge, Kilombero
WANANCHI wa kata za Chita, Mngeta na Mlimba wilayani hapa wametaka serikali itenge bajeti ili kuwalipa mishahara na marupurupu mengine wenyeviti wa vitongoji na vijiji  kutokana na kazi kubwa wanazozifanya badala ya kujitolea.

Wamesema kuwa wenyeviti hao ni watendaji muhimu wa serikali katika ngazi za vitongoji na vijiji na hivyo kufanya kazi kwa kujitolea ni kutowatendea haki na kunawakatisha tama.

Mmoja wa wananchi hao, Cosmas Kibiki, amesema kuwa viongozi wote wanaochaguliwa na wananchi kuanzia rais, mbunge na diwani wanalipwa mishahara, posho na marupurupu mengine lakini wenyeviti wa vitongoji na vijiji wanasahaulika.

Kwa upande wake mkazi wa kijiji cha Mlimba A, Mussa Gili, amesema kuwa kuwalipa mishahara na marupurupu viongozi hao kutapunguza wimbi la rushwa katika ngazi hizo za utawala kutokana na ujira watakao upata na ambao utaweza kuongeza ari ya utendaji wao wa kazi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wenyeviti wamekuwa wakishirikiana na watendaji wao kuhujumu mali za vijiji kama vile ardhi kutokana na kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato na kwamba ikiwa serikali ilikubali watendaji wa vijiji walipwe ingefanya vivyo hivyo kwa wenyeviti wao.

Hata hivyo, Geofrey Ngiyi, akichangia maoni yake katika katiba amesema kuwa mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata yatazamwe upya kwa vile yamekuwa ndiyo msingi wa migogoro ya ardhi katika vijiji.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na wengi wa wajumbe wa mabaraza hayo kutokuwa na elimu ya kutosha ya utatuzi wa migogoro ya ardhi ha hivyo kushauri kuwa katika ibainishe kuwa wajumbe wa mabaraza hayo wawe wasomi wenye utaalam wa kutatua migogoro hiyo.

Ngoyi amesema kuwa watu wengi wamekuwa wakipoteza haki zao za kumiliki ardhi kutokana na maamuzi mabovu ya mabaraza hayo na kutokana na umasikini wa watanzania waliowengi wamekuwa wakishindwa kupeleka kesi hizo katika mahakana za ardhi.

No comments:

Post a Comment