HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Wednesday, October 10, 2012

Mgogoro wa Ardhi Sanje watatuliwa

  Henry Bernard Mwakifuna, Sanje-Kilombero  
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Bwana Hassan Masala amepongeza hatua iliyofikiwa katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa Ardhi uliojitokeza kati ya Mwekezaji na Serikali ya Kijiji cha Sanje katika Wilaya hiyo.
 
Akitoa maelezo baada ya kupitia mapendekezo yaliyomo katika waraka wa mapendekezo ya suluhu ya mgogoro huo Mkuu huyo amesema kuwa atasaidia kupata Wataalamu ili kufanya tathimini ya Athari zinazoweza kutokea kufuatia Mto Sanje uliokuwa umehama katika njia yake ya asili na kumega eneo la serikali ya kijiji na kwenda katika eneo la mwekezaji.
 
Wataalamu kutoka idara ya Ardhi, mazingira na Mipango miji wameagizwa kwenda kufanya tathimini ya athari na nini cha kufanya ili kuweza kunusuru hali ya eneo la Mto Sanje linalomeguka.
 
Kamati iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero kwa ajili ya kupata suluhu ya Tatizo la Mpaka kufuatia Mto Sanje kuhama eneo lake la Asili kati ya mapendekezo yake ni Kufanyika kwa  tathmini ya Kimazingira ya mwenendo wa Mto unapojaa na kupungua ili kuchukuliwa hatua zinazostahili.
 
Taarifa hiyo yenye Mapendekezo Sita iliyosainiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Afisa Tarafa ya Mang'ula Victor Ndiva imependekeza  msingi uliochimbwa ufukiwe kwa usaidizi wa Mzee Mohamedi Khalfani (Mwekezaji) kwa kuwa ndiyo chanzo cha Wananchi na Viongozi kufikishwa Mahakaman
i.

No comments:

Post a Comment