HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Wednesday, October 10, 2012

Ulanga/Kilombero wapania kuboresha Kilimo

Na Senior Libonge,Kilombero

MAAFISA ugani 7 kutoka katika vijiji vilivyo chini ya mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi wilayani Kilombero wanapatiwa mafunzo kuhusu dhana ya shamba darasa.

Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika mjini Ifakara na yanaendeshwa na wawezeshaji kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilombero chini ya ufadhili wa asasi ya uhifadhi wa mazingira na maendeleo katika bonde la Kilombero(KIVEDO).

 Kwa mujibu wa mwezeshaji wa mbinu ya shamba darasa kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilombero Juliana Njombo amesema lengo la mafunzo hayo ni kutaka washiriki kuweza kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendesha shamba darasa katika maeneo yao.

 Juliana amesema maafisa hao ugani wanatoka katika vijiji vya Mofu,Namawala,Kisegese,Mbingu,Udagaji,Mkangawalo na kijiji jirani cha Ihanga  na kusudio la kuendesha mafunzo hayo ni kutekeleza sera ya wizara ya kilimo,ushirika na chakula ya kuwa na shamba darasa kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao.

Amesema kiwilaya wameamua kuanzisha mashamba hayo darasa ikiwa ni mbinu ya kuendesha kilimo ambayo ni rafiki wa mazingira kwani wanatumia pembejeo za viwandani pale inapobidi.

Mwezeshaji huyo amesema mafunzo hayo wataalamu watatumia mbinu husishi ambapo unazuia wadudu na magonjwa kwa kutumia mbinu ya kibailojia mfano kwa kutumia mdudu ambaye ni adui wa mdudu mharibifu wa mazao au mbinu za asili za uzalishaji mazao.

Amesema zao lililopewa kipaumbele ni zao la mpunga kwani pia ni zao lililopewa kipaumbele na wilaya na taifa hasa baada ya wilaya kupewa jukumu la kuzalisha zao la mpunga na pia zao la mpunga limechaguliwa na wadau wa sekta ya kilimo wilayani kwenye mpango wa kuendeleza sekta hiyo.

 Hata hivyo Juliana amesema matarajio yao baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo ni kila afisa ugani kuanzisha shamba darasa katika eneo lake ambalo atakuwa anafanya kazi na kikundi cha wakulima wasiopungua 25.

 Na baada ya msimu kuisha wanatarajia wakulima watakaofunzwa nao kuanzisha mashamba darasa katika sehemu zao na hiyo yote ni kufuatia kufuata kanuni za mbinu husishi za uzalishaji mazao ambazo ni kustawisha mazao yenye afya shambani,mkulima kutembelea shamba lake mara kwa mara,kuhifadhi wadudu rafiki wa mkulima na mkulima kuwa ndiye mtaalamu.

No comments:

Post a Comment