HONGERA ULANGA COMMUNITY RESOURCE CENTRE

photos

Welcome to UCRC

About Me

Ulanga Community Resource Centre is a not-for-profit company limited by guarantee which was initiated with the aim of capacitating the resident peoples of Ulanga and Kilombero Districts and Tanzania in general to secure the right information and hold their duty bearers accountable in a bid to promote sustainable community development. UCRC as well aims at promoting educational activities in Ulanga District through facilitation of necessary educational resources in the area which include well equipped libraries and study centers. UCRC also works on land and natural resource rights for the marginalized rural people in Tanzania which also include sustainable use of such resources. It also provides legal aid and assistance to the poor, particularly women, children, the disabled and other disadvantaged groups in the society on different themes including land and gender.

Monday, October 1, 2012

Uchaguzi CCM Kilombero wamalizika

Na Senior Libonge,Kilombero

UCHAGUZI wa viongozi mbalimbali ndani ya chama tawala Chama cha Mapinduzi(CCM) umemalizika na wengi wa viongozi waliopita wametetea nafasi zao akiwemo mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Kilombero.

Katika uchaguzi uliofanyika juzi katika uwanja wa Taifa mjini Ifakara viongozi watatu wa juu wa chama hicho wametetea nafasi zao akiwemo mwenyekiti wake Abdallah Kambangwa,Katibu wa siasa na uenezi Pelegrin Kifyoga na katibu wa uchumi Rajabu Kiwanga.

Kinyang'anyiro kikali kilikuwa katika nafasi ya uwenyekiti ambapo Kambangwa alikuwa anachuana vikali na aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya Cyprian Kifyoga ambapo hadi majira ya saa 5 usiku ndipo dalili za ushindi kwa Kambagwa zilipoanza kujulikana na hiyo ilitokana na ukubwa wa makundi kwa pande zote mbili.

Kambangwa alifanikiwa kupata kura zaidi ya 800 huku Kifyoga akipata kura zaidi ya 400 na matokeo hayo yalitangazwa majira ya saa 7 usiku baada ya zoezi la kuhesabu kura kuwa gumu hasa kutokana na uwingi wa wajumbe.

Nafasi nyingine zilikuwa za mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ambapo Haruni Kondo amefanikiwa kushinda huku nafasi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa wakichaguliwa mkuu wa wilaya ya Kilombero Hassan Masala,Jaji mstaafu Edward Mwesiumo,Mwenyekiti wa halmashauri Ramadhani Kiombile,katibu wa vijana wilaya Mariam Mwande na Watende Kondo.

Kwa upande wa wajumbe wa kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya wilaya walipenya katika nafasi hiyo ni pamoja na Edward Masolwa,Isaya Magungu na Alex Holela hao ni kwa upande wa wanaume na upande wa wanawake ni Mercy Minja na Watende Kondo.

Licha ya vioja vya hapa na pale lakini uchaguzi huo ulifanyika vizuri ila baada ya matokeo wengi wao hawakuamini matokeo hayo kwa kudhani kuwa sura mpya ndizo zingeshika nafasi lakini yote kwa yote walisema kuwa ushindi ni wana ccm wote na kinachofuta ni kuvunja makundi na kukiimarisha chama.

No comments:

Post a Comment